jsenyinah
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 249
- 338
Ukianza kuzungumzia historia ya Tanzania, jina la "Babu Samunge" si geni akilini mwa waTanzania na nchi za ukanda ya Afrika ya Mashariki, hasa baada ya kujizolea umaarufu wake mkubwa "wa ghafla" baada ya kuanzisha tiba yake ya asili maarufu kama "kikombe cha babu".
Kikombe hiki cha Babu Samunge kilikusanya maelfu ya wananchi toka maeneo mbalimbali ya nchi ya TZ na nchi jirani; viongozi wa serikali, watumishi mbalimbali, raia wa kawaida, wagonjwa toka mahospitalini ambao kwa namna moja au nyingine 'tuliaminishwa' kuponywa na dawa hiyo ya TZS 500 tu.
Ni kama mshumaa ulizima ghafla, babu huyu kama alitoweka ghafla mithili ya kunyauka kwa maua. Kimya kikatawala.
Yu wapi huyu Babu Samunge na kikombe chake cha TZS 500?