Alifanya kazi saiti kwa pesa yake, sasa simu haipokelewi na bosi haonekani

Atoe notice ya kufanya ubomoaji au aende mahakamani
Akibomoa ushahidi wa gharama za ujenzi utapotea. Atadai nini sasa na kazi ameiharibu. Hapo anatakiwa kwenda mahakamani kufungua kesi ya madai sababu wao ndio walimshawishi kuanza ujenzi huku wakiahidi kuandaa mkataba.
 
Naiona changamoto ya conflict of interest. Lakini kwa kuanzia aongee na DED wake kwanza. Akishindwa amcheki RAS akibounce hapo kuna route ntakushauri later.

kwa kuwa jengo limeisha aandike barua ya kukabidhi kazi kwa sababu bila kukabidhi itaonekana kazi haijakubalika na kutoa mwanya wa kuzungushwa kulipwa. Awaandikie sasa kwa sababu shule zinazojengwa kwa mradi wa SEQUIP zinatakiwa kuwa zimekamilika na kuanza kutumika January. Akichelewa kukabidhi msala utakuwa kwake kwa kuwa itaonekana kashindwa kazi. Aongee na Eng. vizuri pia kwa sababu huyo ndie kashikilia kamba hapo.

Na inavyoonekana tayari Mwalimu Mkuu, Engineer na Afisa Elimu walishakula cut bila kumshirikisha kwa kufikiri wa tam fix tu kwa sababu hela za hiyo miradi zipo mashuleni tayari.

Mwambie asiwe mnyonge.
Ushaur mzur mkuu. Ntampa kesho asome atafanyia kaz hilo
 
Kuna jamaa huko mikoa ya magharibi alipewa tenda kubadilisha madirisha kwenye kituo cha afya na kuweka ya aluminum, akafanya kazi yake vizuri sana na akamaliza. Sasa kulipwa ikawa issue, jamaa alivyoona usumbufu umezidi akaenda kung'oa madirisha yote ya aluminum aliyoweka. Aisee jamaa wakamfanyia figisu wakamkamata na kumbambikia makosa na akawekwa ndani. Haya mambo yana uonevu mkubwa sana sometimes.
Baada ya kuwekwa ndani ikawaje?
 
Kuna la kujifunza hapa! Naanza na maelezo na ushauri wangu nimeutoa chini kabisa na lazima utamsadia huyo jamaa yako akiufanyia kazi!

Du! Ama kweli kuna wafanyakazi maofisini wanadhani wanaishi kwa kupendana!

Katika ofisi ile, kuanzia boss mpaka wanakamati wote ni wababaishaji tu!

Yaani mtu anaomba tenda ofisi anayofanyia kazi? Alitakiwa atafute mtu mwingine kama kivuli ndio inakuwa rahisi hata kudai kwa fujo!

Je, mchakato wa manunuzi uliendaje? Je, malipo yanaandikwa kwa jina la jamaa?

Angekuwa ni mtu wa mtaani anaenda na mkwara pale ofisini kubomoa vifaa vyake au kwenda kulalamika kwa viongozi wa juu! Sasa mfanyakazi huyo wa hiyo ofisi ataenda kulalamika wapi? Itaonekana wanatakatisha pesa!

Ushauri wangu! Akubali ameishayakanyaga, hivyo anatakiwa afanye jambo hili:

AENDE KWA BOSS KWA UPOLE AMWAMBIE KWAMBA, AFANYE JUU CHINI INJINIA APITISHE NA MALIPO YATOKE NA ATAMPA BOSS CHOCHOTE KITU.

NB; Wakubaliane kabisa kiwango cha pesa atakachompa boss. Halafu jamaa yako inaonekana ni mpole mpole sana!

Bila ya hivyo atasubiri sana!
 
Back
Top Bottom