Alianza Mukama, Kinana then Nape

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,502
86,050
Kuna gazeti liliripoti miezi michache iliyopita kuwa Mzee Mukama ameamua kutunza heshima yake kwa kujiengua nafasi yake hapo NEC itakapokaa baaade mwaka huu, habari ile ilipingwa sana ila baada ya Taarifa zile hatujawahi kumsikia Mzee wa Msutachi tena, hajawahi kuongea lolote zaidi ya miezi sasa, lakini katikati ya GIZA hili kama kile kilichosemwa ni uongo au ukweli Mzee Kinana ambaye pia kuna taarifa kuwa hakupendezewa kabisa na mkutano wa CCM pale Jangwani miezi michache iliyopita nakwamba pia alitoa tahadhari juu ya kuwataja wapinzani katika mkuatano ule, nae pia Kaamua kukaa kando, japo huyu kawa jasiri kuweka kwa barua na kwa sauti kuwa anakaa kando (sababu za kukaa kando zibaki kama zilivyo, suala ni kwamba amekaa kando).

Biashara ya kupinga MAELEZO ya Kinana inaendelea bado lakini cha kushangaza katikati ya mabishano hayo dhidi ya kauli ya Kinana ameibuka tena Kijana wa Kijani mwenye Afya tele Ndugu yangu na rafiki yangu Mheshimiwa NAPE, huyu naye kuna taarifa hapa jamvini na baadhi ya vyombo vya habari kuwa hatagombea tena NEC. ukweli ni kwamba hiii nayo si dalili njema sana, kuna taarifa za ziada nyuma ya taarifa hizi? Ni zipi hizo?

Updates:
Wazee weneye hekima na mikwara na Vijana wenye maono na uchungu kwa nchi yao watimuliwa NEC-CCM; Maneno ya Mzee Mkapa yatimia mapema kuliko ilivyotarajiwa kuwa Wazee wanaonekana kuwa hawana busara na ushauri wao hauzingatiwi tena....
Hakuna anaejua kwa sasa..... Who is next? ukiachilia mbali kukaa kimya kwa Mzee Makamba, Kingunge na Fresh Comment ya Mzee Mkapa (kuwa Wazee hawathaminiwi mawazo yao) Kuna nini jamani huko CCM?
Je huu ndio mwisho wa CCM?
 
Ni mtazamo wangu tu, mimi si mtu wa siasa jamani. Thanks
 
Naomba kuelimishwa tu, hivi Mukama na Nape kama sekretariet ya CCM hawaingii moja kwa moja kwenye NEC kutokana na nyadhifa zao? hapa naona mleta mada unatulisha matango pori tu. hivi inawezekana vipi kikao cha NEC kikae bila Secretarieti?
 
Mpwa ka kweli sijui jibu la swali lako ila nilichaofanya nikuanukuu tu kauli zao na matendo yao, ni hicho kama si hivyo basi wao kutokana na kauli zao na matendo yao ndio watakua wanatulisha KASA na sio tango pori tena, thanks
Naomba kuelimishwa tu, hivi Mukama na Nape kama sekretariet ya CCM hawaingii moja kwa moja kwenye NEC kutokana na nyadhifa zao? hapa naona mleta mada unatulisha matango pori tu. hivi inawezekana vipi kikao cha NEC kikae bila Secretarieti?
 
kwa vyovyote vile iwavyo, kwa namna yoyote ile, mi naomba ccm ife ili hao waliomo watoke nje ya hilo kundi ovu waanze maisha mapya. huwezi jua pengine watatubu madhambi yao na kuokoka. hakika kukaa kwenye hilo genge ni kuendelea na dhambi ambayo unaweza usipate muda wa kutubia, mwishowe mauti yatakukuta humohumo ukiwa na dhambi lukuki za kuwadhulumu watanzania rasilimali zao, kuwaongopea kila uchaguzi, kuwalaghai kwa kuwapa chumvi, sukari, t-shirts wakati wa uchaguzi halafu wakishakupigia kura unawakanyaga kwa kushindwa hata kuwapatia dawa hospitalini na madawati,vitabu na waalimu kwenye shule huku wewe ukipeleka wanao na wewe mwenyewe nje ya nchi kutibiwa na kusoma, mbaya zaidi unajilipa mshahara unaotaka halafu wengine kama waalimu na madaktari wakitaka nyongeza unawaua achilia mbali kuwatishia. NI WAKATI MUAFAKA WA WEWE ccm KUFA.
 
Magamba kwishinei!!!!!!!!!!!!! na Chadema hiyoooooooooooooo!!! Mungu tujalie hivyo nchi yetu ikombolewe.
 
Jana Kaka Alfani anasema kuwa CCM haitakufa na ipo daima, na wanaoitakia CCM mabaya watakufa wao, hadi nikatetemeka mwili niakjua labda amesoma hii post yangu na sasa ananiwinda, ikabidi nipige goti nakusali sala yangu ya mwisho, Dear CCM sina ugomvi na nyie jamani
 
Mpwa una visa wewe !
 
kwa vyovyote vile iwavyo, kwa namna yoyote ile, mi naomba ccm ife ili hao waliomo watoke nje ya hilo kundi ovu waanze maisha mapya. huwezi jua pengine watatubu madhambi yao na kuokoka. hakika kukaa kwenye hilo genge ni kuendelea na dhambi ambayo unaweza usipate muda wa kutubia, mwishowe mauti yatakukuta humohumo ukiwa na dhambi lukuki za kuwadhulumu watanzania rasilimali zao, kuwaongopea kila uchaguzi, kuwalaghai kwa kuwapa chumvi, sukari, t-shirts wakati wa uchaguzi halafu wakishakupigia kura unawakanyaga kwa kushindwa hata kuwapatia dawa hospitalini na madawati,vitabu na waalimu kwenye shule huku wewe ukipeleka wanao na wewe mwenyewe nje ya nchi kutibiwa na kusoma, mbaya zaidi unajilipa mshahara unaotaka halafu wengine kama waalimu na madaktari wakitaka nyongeza unawaua achilia mbali kuwatishia. NI WAKATI MUAFAKA WA WEWE ccm KUFA.

Baada ya CDM
 
Ni mtazamo wangu tu, mimi si mtu wa siasa jamani. Thanks

Nakubaliana na mtazamo wako Elli, kwani hata ukiangalia picha ya juzi ya mkutano wa cc ya magamba utaona kabisa kuwa Mukama yupo yupo tu na anangojea uchaguzi uishe akabidhi ofisi kwa katibu mkuu mwingine na ndio maana hakuvaa hata nguo zao za kijani kama wenzake!! Kuhusu Nape ni wazi kuwa kwa vyovyote vile hawezi kuchaguliwa kwa kura za wanachama wenzie kwa jinsi alivyokihodhi hicho chama chao kwa kauli zake za kuwagawa wenzie hivyo anaona kuliko kuabika afadhali ajiengue mapema!! Kinana afadhali amesoma alama za nyakati na ameng'atuka kwani he is past his EXPIRY date; he is no longer useful to the magambas na ndio maana hata kwenye uchaguzi wa rais wa 2010 koba la fedha lilishikwa na familia ya mkweree na sio chama!!
 
Back
Top Bottom