Album 10 bora katika historia ya muziki wa Bongo Fleva

1. Nikupe nini by GK.
2. Machozi, Jasho na Damu by Pro. J
3. a.k.a Mimi by Ngwea.
4. Mkuki Moyoni by Afande Selle.
5. Nitakufaje by GK.
6. Binti by Jide.
7. Mwanafalsafani by FA.
8. Elimu dunia by Daz Baba.
9. Albam ya kwanza ya Dully (Jina limenitoka)
10. Ulimwengu ndio mama by J-Mo.

Album ya kwanza ya Dully ilikuwa inaitwa History Ya Kweli
 
  • Thanks
Reactions: me1
Album bora kabisa kuwahi kutokea kwenye bongo fleva ni hizi....

1. Ulimwengu ndio mama - Jmoe
2. Nini Chanzo - Juma Nature
3. Aka Mimi - Ngwair
4. Mkuki Moyoni - Afande sele
5. Mwanafalsafani - MwanaFA
6. Machozi Jasho na damu - Prof Jay
7. Funga kazi - HBC
8. Binti - Jide
9. Propaganda - Fid Q
10 . 1st album ya Q Chief jina limenitoka

First Album ya Q Chiller ilikuwa inaitwa Mwana Mnyonge
 
  • Thanks
Reactions: me1
Baada ya kutengeneza list ya nyimbo 10 bora za muziki wa kizazi kipya leo tujadili album 10 bora katika historia ya muziki wa kizazi kipya, list hii haitaangalia nyimbo moja tu ya kwenye album bali ubora wa kazi zote zilizomo katika album hiyo husika ya msanii....

1. MACHOZI, JASHO NA DAMU (Professsor J)

kwa mtu yeyote anaefahamu muziki kwa hakika hatashangaa au kubishana na kuona kuwa album ya mzee wa mitulinga inakamata nambari moja katika list yetu, ndani ya hii album utaelimika, utaburudika na pia utacheka, hii ni album bora kabisa katika historia ya muziki wa Tanzania.

2. A.K.A MIMI (Albert Mangwea)

ilisomba tuzo ya album bora wakati imetoka, ukitaka ujue ubora wa hii album kumbuka hata vibao vilivyokuwemo, baadhi ni mikasi, ghetto langu, she got a gwan na vingine vingi na vyote vilihit, kwa maneno machache unaweza kuuita "Thriller" ya bongo, kama hujawahi kuisikiliza kaitafute hupaswi kuacha kuisikiliza album hii kama unapenda burudani

3 UBINAADAM KAZI (Juma Nature)

haya sasa hapa utakutana na mtoto iddi, hakuna kulala na vibao vingine vingi vikali mno, juma kassim kiroboto akiwa katika ubora wake alitoa hii album bora kabisa

4 ELIMU DUNIA (Daz Baba)

hapa utapata elimu ya bure kabisa isiyohitaji ada, nikutajie vibao vichache tu kama mrembo no 8, elimu dunia, wife na vingine mchanganyiko mkali kabisa

5 Kamanda (Daz Nundaz)

hawa majamaa wakiwa katika ubora wao walitoa singo na vibao vilivyokonga nyoyo za wakubwa na wazee, unaikumbuka barua??, hakika hii inastahili kuwemo katika 5 bora

6 STAREHE (Ferooz)

hii hapa najua haihitaji maelezo mengi , jina la album lenyewe ni moja ya hit kubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya muziki, vibao vipo vingine vikali vingi sana kama jirushe, Boss...bonge la album hili

7 SAUTI YA DHAHABU ( T.I.D)

Mzee mnyama ukipenda muite Warioba akiwa katika ubora wake alitoa hii album yenye nyimbo kama Zeze, siamini, siku kama hizi, mrembo na vibao vingine vingi vikali

8 MACHOZI (LADY JAY D)

huwezi kumtaja jide bila kutaja album yake ya kwanza, kwa hakika hii album inakamilisha umalkia wake wa bongofleva na ubinti machozi wake...

9 MARIA SALOME ( Saida Karoli)

hii album ilimtoa kuwa supastaa wa kijijini hadi kuwa supastaa wa afrika mashariki, siwezi sema mengi ila hii ni moja album zilizouza sana nchini na ni nzuri mno

10 Fahari Yako (Mr Ebbo)

MI mmasai bwana , sitaki tena pombe na nyimbo zingine kibao utazikuta humu, Mr ebbo anakamilisha list yetu

Je, umekubaliana na hii list? Kama hujakubaliana nayo hebu weka yako tuone

Ulimwengu ndiyo mama iko wapi!? Historia ya Kweli je!? Wapi Albam ya Mb Dog!?
 
  • Thanks
Reactions: me1
1.a.k.a mimi
2.wachuja nafaka/Mzee wa busara
3.machoz jasho proff
4.ubinadamu kazi- the best selling album of all time in tanzania
5.lady jay D,
 
sitaki kuamini album ya Gk umeiweka kuwa in bora kushinda a.k.a Mimi..!!

au tuhesabu hits nini mkuu..?? hiyo album ya GK INA hits gani?
Sijaitaja kwa kuwa ina hits ngapi, ila nimeitaja kwa kuwa kila nilipokuwa nikiisikiliza sikuwa napeleka mbele hata wimbo mmoja.
 
Baada ya kutengeneza list ya nyimbo 10 bora za muziki wa kizazi kipya leo tujadili album 10 bora katika historia ya muziki wa kizazi kipya, list hii haitaangalia nyimbo moja tu ya kwenye album bali ubora wa kazi zote zilizomo katika album hiyo husika ya msanii....

1. MACHOZI, JASHO NA DAMU (Professsor J)

kwa mtu yeyote anaefahamu muziki kwa hakika hatashangaa au kubishana na kuona kuwa album ya mzee wa mitulinga inakamata nambari moja katika list yetu, ndani ya hii album utaelimika, utaburudika na pia utacheka, hii ni album bora kabisa katika historia ya muziki wa Tanzania.

2. A.K.A MIMI (Albert Mangwea)

ilisomba tuzo ya album bora wakati imetoka, ukitaka ujue ubora wa hii album kumbuka hata vibao vilivyokuwemo, baadhi ni mikasi, ghetto langu, she got a gwan na vingine vingi na vyote vilihit, kwa maneno machache unaweza kuuita "Thriller" ya bongo, kama hujawahi kuisikiliza kaitafute hupaswi kuacha kuisikiliza album hii kama unapenda burudani

3 UBINAADAM KAZI (Juma Nature)

haya sasa hapa utakutana na mtoto iddi, hakuna kulala na vibao vingine vingi vikali mno, juma kassim kiroboto akiwa katika ubora wake alitoa hii album bora kabisa

4 ELIMU DUNIA (Daz Baba)

hapa utapata elimu ya bure kabisa isiyohitaji ada, nikutajie vibao vichache tu kama mrembo no 8, elimu dunia, wife na vingine mchanganyiko mkali kabisa

5 Kamanda (Daz Nundaz)

hawa majamaa wakiwa katika ubora wao walitoa singo na vibao vilivyokonga nyoyo za wakubwa na wazee, unaikumbuka barua??, hakika hii inastahili kuwemo katika 5 bora

6 STAREHE (Ferooz)

hii hapa najua haihitaji maelezo mengi , jina la album lenyewe ni moja ya hit kubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya muziki, vibao vipo vingine vikali vingi sana kama jirushe, Boss...bonge la album hili

7 SAUTI YA DHAHABU ( T.I.D)

Mzee mnyama ukipenda muite Warioba akiwa katika ubora wake alitoa hii album yenye nyimbo kama Zeze, siamini, siku kama hizi, mrembo na vibao vingine vingi vikali

8 MACHOZI (LADY JAY D)

huwezi kumtaja jide bila kutaja album yake ya kwanza, kwa hakika hii album inakamilisha umalkia wake wa bongofleva na ubinti machozi wake...

9 MARIA SALOME ( Saida Karoli)

hii album ilimtoa kuwa supastaa wa kijijini hadi kuwa supastaa wa afrika mashariki, siwezi sema mengi ila hii ni moja album zilizouza sana nchini na ni nzuri mno

10 Fahari Yako (Mr Ebbo)

MI mmasai bwana , sitaki tena pombe na nyimbo zingine kibao utazikuta humu, Mr ebbo anakamilisha list yetu

Je, umekubaliana na hii list? Kama hujakubaliana nayo hebu weka yako tuone

mkuuu album ya Mr nice haiwez kosa apo kwa kigezo cha kutamba enzi izoo
 
Kuna album ya mandojo na domokaya sijui jina...huwez iacha hio ilikua na hit.song zote, taswira, wanok nok,niaje,...na ngoma nyingne kibao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom