Album 10 bora katika historia ya muziki wa Bongo Fleva

Baada ya kutengeneza list ya nyimbo 10 bora za muziki wa kizazi kipya leo tujadili album 10 bora katika historia ya muziki wa kizazi kipya, list hii haitaangalia nyimbo moja tu ya kwenye album bali ubora wa kazi zote zilizomo katika album hiyo husika ya msanii....

1. MACHOZI, JASHO NA DAMU (Professsor J)

kwa mtu yeyote anaefahamu muziki kwa hakika hatashangaa au kubishana na kuona kuwa album ya mzee wa mitulinga inakamata nambari moja katika list yetu, ndani ya hii album utaelimika, utaburudika na pia utacheka, hii ni album bora kabisa katika historia ya muziki wa Tanzania.

2. A.K.A MIMI (Albert Mangwea)

ilisomba tuzo ya album bora wakati imetoka, ukitaka ujue ubora wa hii album kumbuka hata vibao vilivyokuwemo, baadhi ni mikasi, ghetto langu, she got a gwan na vingine vingi na vyote vilihit, kwa maneno machache unaweza kuuita "Thriller" ya bongo, kama hujawahi kuisikiliza kaitafute hupaswi kuacha kuisikiliza album hii kama unapenda burudani

3 UBINAADAM KAZI (Juma Nature)

haya sasa hapa utakutana na mtoto iddi, hakuna kulala na vibao vingine vingi vikali mno, juma kassim kiroboto akiwa katika ubora wake alitoa hii album bora kabisa

4 ELIMU DUNIA (Daz Baba)

hapa utapata elimu ya bure kabisa isiyohitaji ada, nikutajie vibao vichache tu kama mrembo no 8, elimu dunia, wife na vingine mchanganyiko mkali kabisa

5 Kamanda (Daz Nundaz)

hawa majamaa wakiwa katika ubora wao walitoa singo na vibao vilivyokonga nyoyo za wakubwa na wazee, unaikumbuka barua??, hakika hii inastahili kuwemo katika 5 bora

6 STAREHE (Ferooz)

hii hapa najua haihitaji maelezo mengi , jina la album lenyewe ni moja ya hit kubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya muziki, vibao vipo vingine vikali vingi sana kama jirushe, Boss...bonge la album hili

7 SAUTI YA DHAHABU ( T.I.D)

Mzee mnyama ukipenda muite Warioba akiwa katika ubora wake alitoa hii album yenye nyimbo kama Zeze, siamini, siku kama hizi, mrembo na vibao vingine vingi vikali

8 MACHOZI (LADY JAY D)

huwezi kumtaja jide bila kutaja album yake ya kwanza, kwa hakika hii album inakamilisha umalkia wake wa bongofleva na ubinti machozi wake...

9 MARIA SALOME ( Saida Karoli)

hii album ilimtoa kuwa supastaa wa kijijini hadi kuwa supastaa wa afrika mashariki, siwezi sema mengi ila hii ni moja album zilizouza sana nchini na ni nzuri mno

10 Fahari Yako (Mr Ebbo)

MI mmasai bwana , sitaki tena pombe na nyimbo zingine kibao utazikuta humu, Mr ebbo anakamilisha list yetu

Je, umekubaliana na hii list? Kama hujakubaliana nayo hebu weka yako tuone

Umemuacha Sugu? Umewaacha GWM? Soggy Doggy je? East Coast team. Afande Selle je? Sollo Thang je? Balozi? Ijapokua TAKEU ilikuwa na mambo ya kitoto lakini Mr. Nice huwezi kumsahau, kama ambavyo wagosi wa kaya huwez kuwaacha. Sasa majina hayo niliyoyataja Revisit hiyo list yako uone katika hao ukiwaongeza list itakaaje. Kwa mfano Ngwea japo alikuwa mzuri lakini hakustahili kuwa kwenye list kwani yeye ni zao la katikati la Bongo Flavor, hakuwemo katika ile Bongo Flavor ya mwanzoni kabisa enzi zile za Hard Blasters Crew, Gangwe Mob, Sugu, alikuta njia ishafunguliwa na wadau. Na ndo maana tunasema hawa watoto wadogo licha ya mafanikio wanatakiwa wawashukuru sana haea wakongwe kwani walifanyakaz ya ziada kuufanya muziki huo uitwao Bongo Flavor kutambulika

Itakumbukwa kabisa zaman muziki ulikuwa ni wa dansi tu. Wakati Bongo flavor inaingia haikuwa ya wabana pua, ilikuwa ni rap/ hiphop. R&B yake ilikuwa ni akina Mr Paul na baadae nyimbo kama Girl friend wa TID( Wimbo huu unajulikana kama sound track ya mwanzo kabisa katika Bongo Movie)
 
Andaa 50 bora ili kina Sugu na GWM wawepo.

Umemuacha Sugu? Umewaacha
GWM? Soggy Doggy je? East Coast team. Afande Selle je? Sollo Thang je?
Balozi? Ijapokua TAKEU ilikuwa na mambo ya kitoto lakini Mr. Nice huwezi
kumsahau, kama ambavyo wagosi wa kaya huwez kuwaacha. Sasa majina hayo
niliyoyataja Revisit hiyo list yako uone katika hao ukiwaongeza list
itakaaje. Kwa mfano Ngwea japo alikuwa mzuri lakini hakustahili kuwa
kwenye list kwani yeye ni zao la katikati la Bongo Flavor, hakuwemo
katika ile Bongo Flavor ya mwanzoni kabisa enzi zile za Hard Blasters
Crew, Gangwe Mob, Sugu, alikuta njia ishafunguliwa na wadau. Na ndo
maana tunasema hawa watoto wadogo licha ya mafanikio wanatakiwa
wawashukuru sana haea wakongwe kwani walifanyakaz ya ziada kuufanya
muziki huo uitwao Bongo Flavor kutambulika

Itakumbukwa kabisa zaman muziki ulikuwa ni wa dansi tu. Wakati Bongo
flavor inaingia haikuwa ya wabana pua, ilikuwa ni rap/ hiphop. R&B
yake ilikuwa ni akina Mr Paul na baadae nyimbo kama Girl friend wa TID(
Wimbo huu unajulikana kama sound track ya mwanzo kabisa katika Bongo
Movie)
 
Umemuacha Sugu? Umewaacha GWM? Soggy Doggy je? East Coast team. Afande Selle je? Sollo Thang je? Balozi? Ijapokua TAKEU ilikuwa na mambo ya kitoto lakini Mr. Nice huwezi kumsahau, kama ambavyo wagosi wa kaya huwez kuwaacha. Sasa majina hayo niliyoyataja Revisit hiyo list yako uone katika hao ukiwaongeza list itakaaje. Kwa mfano Ngwea japo alikuwa mzuri lakini hakustahili kuwa kwenye list
kwani yeye ni zao la katikati la Bongo Flavor, hakuwemo katika ile Bongo Flavor ya mwanzoni kabisa enzi zile za Hard Blasters Crew, Gangwe Mob, Sugu, alikuta njia ishafunguliwa na wadau. Na ndo maana tunasema hawa watoto wadogo licha ya mafanikio wanatakiwa wawashukuru sana haea wakongwe kwani walifanyakaz ya ziada kuufanya muziki huo uitwao Bongo Flavor kutambulika

Itakumbukwa kabisa zaman muziki ulikuwa ni wa dansi tu. Wakati Bongo flavor inaingia haikuwa ya wabana pua, ilikuwa ni rap/ hiphop. R&B yake ilikuwa ni akina Mr Paul na baadae nyimbo kama Girl friend wa TID( Wimbo huu unajulikana kama sound track ya mwanzo kabisa katika Bongo Movie)

we unapendekeza album IPI haifai
 
1. Nikupe nini by GK.
2. Machozi, Jasho na Damu by Pro. J
3. a.k.a Mimi by Ngwea.
4. Mkuki Moyoni by Afande Selle.
5. Nitakufaje by GK.
6. Binti by Jide.
7. Mwanafalsafani by FA.
8. Elimu dunia by Daz Baba.
9. Albam ya kwanza ya Dully (Jina limenitoka)
10. Ulimwengu ndio mama by J-Mo.

sitaki kuamini album ya Gk umeiweka kuwa in bora kushinda a.k.a Mimi..!!

au tuhesabu hits nini mkuu..?? hiyo album ya GK INA hits gani?
 
Album bora kabisa kuwahi kutokea kwenye bongo fleva ni hizi....

1. Ulimwengu ndio mama - Jmoe
2. Nini Chanzo - Juma Nature
3. Aka Mimi - Ngwair
4. Mkuki Moyoni - Afande sele
5. Mwanafalsafani - MwanaFA
6. Machozi Jasho na damu - Prof Jay
7. Funga kazi - HBC
8. Binti - Jide
9. Propaganda - Fid Q
10 . 1st album ya Q Chief jina limenitoka

album ya Q-chillah inaitwa mwanamnyonge..

hiyo mwanafalsafani imeizidi mini Sauti ya dhahabu ya TID...?
 
Umemuacha Sugu? Umewaacha GWM? Soggy Doggy je? East Coast team. Afande Selle je? Sollo Thang je? Balozi? Ijapokua TAKEU ilikuwa na mambo ya kitoto lakini Mr. Nice huwezi kumsahau, kama ambavyo wagosi wa kaya huwez kuwaacha. Sasa majina hayo niliyoyataja Revisit hiyo list yako uone katika hao ukiwaongeza list itakaaje. Kwa mfano Ngwea japo alikuwa mzuri lakini hakustahili kuwa kwenye list kwani yeye ni zao la katikati la Bongo Flavor, hakuwemo katika ile Bongo Flavor ya mwanzoni kabisa enzi zile za Hard Blasters Crew, Gangwe Mob, Sugu, alikuta njia ishafunguliwa na wadau. Na ndo maana tunasema hawa watoto wadogo licha ya mafanikio wanatakiwa wawashukuru sana haea wakongwe kwani walifanyakaz ya ziada kuufanya muziki huo uitwao Bongo Flavor kutambulika

Itakumbukwa kabisa zaman muziki ulikuwa ni wa dansi tu. Wakati Bongo flavor inaingia haikuwa ya wabana pua, ilikuwa ni rap/ hiphop. R&B yake ilikuwa ni akina Mr Paul na baadae nyimbo kama Girl friend wa TID( Wimbo huu unajulikana kama sound track ya mwanzo kabisa katika Bongo Movie)

Mheshimiwa.... Haijalishi mtu kaanza game lini... Tuangalie ubora wa album... Kuanza game zamani hakukufanyi uwe na album nzuri kushinda wa aliyekukuta..

Album ya ngwair ukisema haistahili kuwemo... Utakuwa ni mshangao maana ni the best selling album kwa upande wa wanamuziki wa Rap ukiacha mauzo yake pia ina hits kibao na ni bora sana kiasi kwama kwa vyovyote vile mtu atakavyopanga list ya album bora za muziki wa Bongo kama atazingatia viwango lazima iingie top 5
 
Pangeni vyovyote lakin album hizi zisikosekane
Machozi jasho na damu,Album ya TID (Yenye zeze),A.K.A mimi ya Ngwair.

Mkipata nafasi zaid muwekeni na Duly sykes.
 
Pangeni vyovyote lakin album hizi zisikosekane
Machozi jasho na damu,Album ya TID (Yenye zeze),A.K.A mimi ya Ngwair.

Mkipata nafasi zaid muwekeni na Duly sykes.

Album ya TID ynye zeze nimeiweka inaitwa sauti ya Dhahabu... Hizo zingine zote ulizotaja zipo.. Sema kwa maoni yangu ya Dully imeshindwa kuingia TOp 10
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom