KIDUDU
JF-Expert Member
- Sep 17, 2012
- 2,554
- 1,920
Poleni sana watu wa Arusha, hili janga kila mmoja ajizatiti kivyake bila kuogopa tukajifanya ngangari hakika watu watakufa sana. Serikali haiwezi kushindwa kuzika itazika hata tukifa milioni 7, kikubwa ni sisi kujilinda wenyewe.Arusha tunajifia tu na ugonjwa wa kukosa kupumua. Oh! Lord have Mercy
Kuna kisa kile cha Njiro, pia kuna kingine nimesikia jioni hii kuna maiti juzi kati imechukuliwa usiku Sakina walioona wameona
Hao maofisa afya ndiyo wamemtonya Albert kuwa hali ni tete watu wanakufa kama mchezo.Ni vema Wakili angeliwashirikisha maofisa afya ili kubaini uhalisia wa hali mbaya.
Kwa kweli Arusha vifo vipo. Naskia Rama wa Raha advertising nae ni mgonjwaArusha tunajifia tu na ugonjwa wa kukosa kupumua. Oh! Lord have Mercy
Kuna kisa kile cha Njiro, pia kuna kingine nimesikia jioni hii kuna maiti juzi kati imechukuliwa usiku Sakina walioona wameona
Ana hati miliki.Hatakamatwa na police kweli huyu
Jr
Msando ameiamini sana sanitizer kwa kitendo cha kushikana mikono.Naona utaratibu kushikana mikono bado wanautumia
Barakoa 100...Wakili wa Kijitegemea, Alberti Msando ametoa msaada wa barakoa 100 pamoja na vitakasa mikono 100 kwa waandishi wa habari Mkoa wa Arusha ili kujikinga na maambukizi ya Covid-19 kutokana na kazi yao kuwa na mwingiliano wa watu.
Akikabidhi msaada huo leo kwenye Ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha(APC) kupitia kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Claud Gwandu, Msando alisema wanahabari ni watu muhimu katika kutafuta habari hivyo hatua ya kuwapatia barakoa na vitakasaa mikono itawawezesha kupambana na ugonjwa huo.
Alisema wanahabari ni watu muhimu katika kutoa taarifa sahihi za kudhibiti ugonjwa huo ikiwemo kuelimisha jamii juu ya maambukizi ya ugonjwa wa Korona ikiwemo kuhakikisha wanafuata taratibu zote zinazotakiwa katika kujikinga na ugonjwa huo.
Alisema wanahabari wananchango mkubwa katika utoaji wa taarifa zao ikiwemo kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi licha ya ugonjwa huu wa Korona kuwepo kwa jamii.
"Lazima mchukue tahadhari ya ugonjwa huu wa Corona kwa kuandika habari sahihi na kutoa habari kwa wananchi hivyo ni lazima muandike habari ili wananchi wajue "
Naye Mwenyekiti wa APC, Gwandu alishukuru kwa msaada huo kwa wanahabari ambao utawasaidia kujikinga na ugonjwa huo na kutoa rai kwa wadau wengine kujitoa kusaidia wanahabari katika kupambana na ugonjwa huu wa Corona.
Pia wanahabari wengine wa Mkoa wa Arusha Lillian Joel Uhuru na Cynthia Mwilolezi wa Nipashe walishukuru kwa msaada huo ambao utawasaidia kujikinga na maambukizi ya Covid - 19.
Ends....
View attachment 1433259View attachment 1433260View attachment 1433261
Sent using Jamii Forums mobile app
Wanauza wapi bei hio mkuu?Kama hivyo hata mimi naweza kusaidia mtaa wangu.Barakoa 100...
Barakoa 1=Tshs 250.
Vitakasa mikono 1= 350.
Amejitahidi kwa waandishi wetu hao wa bahasha za kupigia brush viatu vyao.
Sent using iphone pro max
Duuh! AiseeHawa ndio wale anavaa balakoa (mask), halafu havai condom.
Barakoa 100...
Barakoa 1=Tshs 250.
Vitakasa mikono 1= 350.
Amejitahidi kwa waandishi wetu hao wa bahasha za kupigia brush viatu vyao.
Sent using iphone pro max
Ukweli ni kuwa watu wanakufa na serikali imekaa kimya kama vile nothing is happening.CCM tumfukuze huyu mamluki wa Zitto, anapingana na mwenyekiti wetu kuhusu kutia watu hofu
Hana hoja badala ya kujiuliza ni nini kimefanya waandishi wamekuwa waoga analeta story za kuwapa moyo, wakipata matatizo atawasaidia? Serikali ya chama chake ndio imekandamiza uhuru wa habari mpaka tumefika hapa. Hakuna habari, ni sifa tu kwa serikali. Watu wakijaribu kutafuta na kutupatia habari wanapigwa kesi zisizo na dhamana. Afanye yeye, uzuri siku hizi channel za kufikia wananchi ni smartphone na internet yako.acheni siasa chafu...ebu msikilize hoja zake