Al-Jazeera walipoenda undercover na kufanya kazi za Polisi wa Tanzania (Video ya Mauaji ya Albino)

huyu mwandishi ni mnigeria aisee..sisi waandishi etu wanafanya nini? lol!! hawana ujasiri au hawana elimu
 
Wadau ni aibu ya hali ya juu dunia sasa hivi inawatch mauaji ya Albino na mateso yao in general. Kuna picha hazijawahi kuonyeshwa na local TV station yeyote. Ni aibu hata kuangalia natamani kuzima TV but kinachoniweke niendelee ni kupata zaid details zilizofichwa na local medias. Watch now aibu hizi.
 
Anas Aremeyaw Anas muandishi wa habari za uchunguzi kutoka Ghana aliyekuwa anafanya kazi za uchunguzi kwa niaba ya Aljazeera film yake itatangazwa na aljazeera, hii ni habari mbaya sana kwa Tanzania. Anaeleza hatari zinazowakuta albino wa Tanzania.

Kilichonishangaza si mauaji ya albino ambayo yamezoeleka bila hatua madhubuti za kuwalinda kufanywa, bali ni matumizi ya viuongo vyao kushinda uchaguzi. Anas anasema kuwa mikono, miguu au kichwa cha albino hutumiwa na wanasiasa katika kutengeneza dawa ya kujipatia ushindi katika uchaguzi.

Hili la dawa ya ushindi kwenye uchaguzi ndilo limenistua sana, kama ni kweli wanasiasa wanahusika na basi ni dhahiri vita hii haiwezi kuwa rahisi kama wanaotakiwa kuwalinda albino ndiyo watumiaji wakubwa wa viungo vyao.

Nafikiri sasa umefika wakati kuwamulika wanasiasa wote katika vita dhidi ya mauaji ya albino. Hii ni habari mbaya sana kwa Tanzania kama ina ukweli ndani yake. Msikilize Anas katika mahojiano yake hapa chini

[video]http://news.peacefmonline.com/news/201112/83727.php[/video]

NB: I appreciate the efforts by authorities to combat the problem. Ila nafikiri sasa wasiangalie wauaji tu waangalie na wateja wao including wanasiasa washirikina. Iwe kama philosophy ya ugaidi, kuwa uki-fund gaidi na wewe ni gaidi. Ukifund(nunua) au kutumumia viungio vya albino na wewe ni muuaji wa albino.
 
Last edited by a moderator:
Anas Aremeyaw Anas muandishi wa habari za uchunguzi kutoka Ghana aliyekuwa anafanya kazi za uchunguzi kwa niaba ya Aljazeera film yake itatangazwa na aljazeera, hii ni habari mbaya sana kwa Tanzania. Anaeleza hatari zinazowakuta albino wa Tanzania.

Kilichonishangaza si mauaji ya albino ambayo yamezoeleka bila hatua madhubuti za kuwalinda kufanywa, bali ni matumizi ya viuongo vyao kushinda uchaguzi. Anas anasema kuwa mikono, miguu au kichwa cha albino hutumiwa na wanasiasa katika kutengeneza dawa ya kujipatia ushindi katika uchaguzi.

Hili la dawa ya ushindi kwenye uchaguzi ndilo limenistua sana, kama ni kweli wanasiasa wanahusika na basi ni dhahiri vita hii haiwezi kuwa rahisi kama wanaotakiwa kuwalinda albino ndiyo watumiaji wakubwa wa viungo vyao.

Nafikiri sasa umefika wakati kuwamulika wanasiasa wote katika vita dhidi ya mauaji ya albino. Hii ni habari mbaya sana kwa Tanzania kama ina ukweli ndani yake. Msikilize Anas katika mahojiano yake hapa chini

[video]http://news.peacefmonline.com/news/201112/83727.php[/video]

[video]http://www.aljazeera.com/programmes/africainvestigates/2011/11/201111185428766652.html[/video]

Kwanza napenda pia kukupongeza wewe kwa kazi nzuri ya kuleta habari hii hapa jamvini, watawala wetu haya wao ni kama hayawahusu wapo bussy kuongezeana posho na kuiba mali za watanzania. Nampongeza sana Journalist wa Ghana kumulika haya maovu ili dunia nzima ione pengine hata mkuu wa kaya atakoso guts za kutabasamu x 2 kila wakati wakati hali ya nchi ni mbaya sana. Well done all kwa kuelimisha jamii. Lets make this forum an engine for change.
 
Ina maana viungo vya Albino ndo vimewaweka CCM madarakani?

If so, huo ushindi ni batili kabisa!
 
What I also found interesting ni kuwa mwandishi wa Nigeria ndiye aliyeenda anda cover; ukiona Vick Mtetema sidhani kama kuna waandishi wetu wakubwa ambao waliwahi kwenda kuzama kama alivyofanya huyu jamaa. Au hatuna vifaa na uwezo - hadi tuwezeshwe?

Mwanaijiji wewe kichwa chao cha habari kilenda mbali kwenye hii coment sasa ndi nilichotak kuuliza.

Hawa Alazajera wanatumia vifaa gani au binadamu wenye uwezo gani amabo taaisis zetu za kama TBc hazina .

Aisee inasikitisha sana.
 
Mwandishi ni mghana si mnigeria

Ila hii ni aibu kwa kitengo cha uchunguzi polisi na hata vyombo vyetu vya habari
 
So scary, halafu eti kuna watu wanajaribu kulazimisha hoja kwamba Tanzania ya leo imeendelea maradufu!!!!! This is just one aspect ya wale maadui wetu wakuu.......sasa tujiulize tumeongeza na mwingine ufisadi tutatoka hapo?
 
Mwanaijiji wewe kichwa chao cha habari kilenda mbali kwenye hii coment sasa ndi nilichotak kuuliza.

Hawa Alazajera wanatumia vifaa gani au binadamu wenye uwezo gani amabo taaisis zetu za kama TBc hazina .

Aisee inasikitisha sana.

Where is Jerry Muro? Tatizo intelligence yetu ina function kinyume, iko makini ku react dhidi ya yeyote anayeonekana tishio kwa watawala, usalama wa wananchi wameuweka rehani..!
 
Mwandishi ni mghana si mnigeria

Ila hii ni aibu kwa kitengo cha uchunguzi polisi na hata vyombo vyetu vya habari
Ni aibu kwa taifa mkuu, nina uhakika kabisa kuna wabongo waliko nje ya Tanzania wanakuwa kwenye situation ambapo wanaona wakijitambulisha wametoka bongo sintofahamu nyingi na maswali kibao,kama huna muda nashauri usiseme ni mbongo.

How can you be proud to be a Tanzanian under these circumtances?
 
Nakumbuka wakati wa kesi za wale Watanzania maskini walioshatkiwa kwa tuhuma za mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, huko Shinyanga katika utetezi wao walisema walikuwa wakitumwa na 'Mwarabu' kwa ahadi ya mamilioni ya fedha. Nway lakini pia, kama baadhi yao walikiri, kwa nini upelelezi haukwenda extra miles kujua soko lao na kitu gani hasa kilisababisha wao kujua kuwa kuna demand, hivyo inahitajika supply. Yu wapi yule mwarabu na mamilioni yake! Yako wapi matokeo ya kura za maoni juu ya mauaji ya albino iliyowahi kufanyika, I guess 2009? Yule Mbunge wa CCM kutokea Kigoma ambaye hata mamla za chama wilaya na mkoa zilisema kuwa watu wa kijijini kwake wana suspect anahusika na mauaji haya, yuko wapi leo kama si bungeni na wale wote walioleta madai hayo kushambuliwa badala ya tuhuma kuchunguzwa? Wanajuana.
 
Amua mwenyewe... tulihitaji Al-Jazeera kwenda this deep.

MM pole sana kwa kuumiza kichwa juu ya jeshi letu la polisi,binfsi siwezi kulaumu jeshi la polisi kwa udhaifu uliopo,naamini uwezo wa jeshi la polisi kufanya kazi unatokana na AMIRI JESHI MKUU je ? anajua nini jeshi la polisi linatakiwa kufanya ili kulinda RAIA wa nchi yake ? sidhani kama anajua kabisa,YEYE anajua kazi ya jeshi la POLISI ni kulinda AMANI,AMANI inayotakiwa kulinda ni kuhakikisha wananchi wasiwabugudhi viongozi wao wafanyapo UFISADI hata kukiuka sheria za nchi,hivyo Jukumu kubwa la JESHI la POLISI ni kuhakikisha wakubwa hawabughuziwi na wananchi niwe kwa maandamano ya kudai haki au lah,Kuna wakati inakuwa aibu kwa sisi wenye marafiki wasio waafrika kwa haya wanayoyasikia na kuyaona yakitendeka nchi mwetu. Nina rafiki alisikia juu ya mauaji ya albino aliniuliza swali kuwa POLISI yenu haijui kuwa albino wanauawa ? akauliza inawezekanaje auawe wa kwanza,wapili,watatu... huku jeshi la polisi kusiwe na watu waliowajibika kwa kushindwa jukumu lao la msingi ambalo ni kulinda usalama wa raia na mali zao.

sikuwa na jibu kwani hata mimi ni sehemu ya raia wa nchi hii,kwa namna moja rafiki yangu anafikiri watanzania wote wanafikiri na kuona kama binadamu wanavyotakiwa,ni aibu kwa sababu pamoja na mapungufu hayo watz walio wengi huwaambii kitu juu ya serikali na chama chao ambacho wanaona kinafanya maajabu ambayop hakuna binadamu au chama kiingine kinaweza kufikia.INAUMIZA SANA
 
Last edited by a moderator:
Mkuu MM..haya mambo sio kwamba hayajulikani...yako wazi,kwamba kuna interest za 'wakubwa' of which zinaweza kumeza 'good will' ya 'mdogo' aliyerushia kitumbua mchanga...yatosha kumwappreciate 'whoever' aliyeenda so called 'under cover' kufichua ufedhuli wa aina hii...long live private dick!
 
lakini pia tz hatuna waandishi wa habari za uchunguzi bali wote wamekuwa ma-reporter ndo maana hata ktk vipengele vya zawadi za baraza la hbr hakuna hicho kipengele cha hbr za uchunguzi
asante al-jazeera
 
Chanzo cha watu kuamini ushirikina ni nini? Huyu Bwana Mtangazaji anasema kisa watu are "uneducated". Hivi Tanzania wale waliosoma hawaamini ushirikina? Manake nimekumbuka kisa cha Chenge na ungaunga Bungeni
...Hakuna ushahidi unaoonyesha bungeni kuna watu "educated", hata wa kimazingira. Badala yake, kuna watu waliohudhuria shule.

...Wengi tumehudhuria shule tu. Hatukujifunza, ndio maana haya na mengine mengi yanafanyika, na baadhi wanashangaa inakuwaje.
 
Back
Top Bottom