Akamatwa kwa wizi wa magari

MR LINKO

JF-Expert Member
Aug 20, 2016
3,034
3,481
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia mkazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam, Venance Ramadhani (36) kwa tuhuma za wizi wa gari aina ya Nissan Xtrail.

57550740.295.jpg
Kukamatwa kwa gari hilo kulitokana na askari wa usalama barabarani walipokuwa wakifuatilia madeni ya faini za tozo la makosa ya usalaama barabarani ambapo mtuhumiwa alidai kuwa sio mmliki wa gari hilo na kukaidi kulipa faini ya deni.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Fortunatus Musilimu amesema gari hilo likiwa kituo cha polisi alijitokeza, Melkizedeck Gahutu (50) mkazi wa Tabata Dar es Salaam akieleza kuwa iliibiwa toka Juni 22 mwaka huu baada ya kukodishwa kutokomea nalo kusikojulikana.

Kamanda Musilimu amesema Melkizedeck ni msimamizi wa kampuni inajishughulisha na kazi ya kukodisha magari kwa watu binafsi ambapo mahojiano ya kina yalifanyika kwa dereva aliyekutwa na gari hilo na kukikiri kuhusika na wizi wa gari hilo pamoja na magari mengine mawili ambayo yamefichwa.

“Tulifuatilia maelezo ya dereva yule na kupatikana kwa gari la Toyota Alphad likiwa nyumbani kwa mtu mwingine, Shabani Amani (33) mkazi wa Mafisa Morogoro.”amesema Kamanda Musilimu.

Kamanda Musilimu amesema Shabani katika mahojiano yao na jeshi hilo alionyesha gari nyingine Toyota Alphad eneo hilo la Mafiga ambapo upelelezi zaidi ulifanyika na kugundua kuwa gari aina ya Nissan X-Trail ilikuwa katika mchakato wa kugushi hati za umiliki.

Kamanda Musilimu amesema mahojiano na upelelezi unaendelea dhidi ya watuhumiwa wote wawili ili kubaini mtandao mzima unaojihusisha na uhalifu wa aina hiyo na taratibu zinaendelea kuwafikisha watuhumiwa na vielelezo katika mikoa waliyofanyia uhalifu kwa hatua zaidi za kisheria.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom