Bongo Pix Blog
JF-Expert Member
- Sep 13, 2011
- 213
- 33
Taarifa nilizozipata toka eneo la ajari Lusaunga ni kuwa basi la Taqwa toka Dar es Salaam limengongana na roli la mizigo na watu zaidi ya 30 wanahofiwa kuwa wamekufa, shuhuda wa ajari ambaye amenipigia simu muda si mrefu, amesema ameona maiti wengi sana, wamelazimika kusitisha safari yao ya kikazi na kubeba majeruhi kuwaleta hospitali ya Biharamulo, Ninaelekea hospitali nitawajuza zaidi kilie kinachoendelea.
Updates:
Nimetoka Hospitali Teule Biharamulo, nimeshuhudia miili ipatayo 10 ikishushwa toka katika fuso, pia niliongea na afande mmoja akanambia kuwa walishaleta miili 2, hivyo inafanya idadi kuwa 12, majeruhi ni zaidi ya ishirini, hata hivyo idadi kamili na majina itapatikana baada ya kuongea na mamlaka husika RPC na Mganga Mkuu wa Hospitali, hali ni mbaya sana, yamegongana uso kwa uso, hivyo idadi ya vifo yaweza kuwa maradufu. Tembelea HAPA kwa picha na taarifa zaidi