Ajali mbaya Handeni, basi la Burudani limeua 12

nimewahi kuripoti hapa juu ya mwendo kasi na ukosefu wa mikanda ya usalama. nikapuuzwa, sasa matokeo yake yake ndio hayo. ivi gari linaenda na kurudi dar to lushoto sumatra mpo wapi? servece inafanyika wakati gani?
 
Kuna maeneo yana mkono wa wenyewe ndugu yangu...si kila jambo hutokea kwa sababu za kimaumbile bali zipo zile zitokeazo kwa namna isiyoonekana kwa macho...

ila KABUKU NA MBWEWE ni maeneo ya ajali sana kwa hii njia ya kwenda kaskazini,
kinachonishangaza siku ya uhuru basi la kampuni hii hii lilipata ajali maeneo hayo hayo sasa je kuna nini hapo??
je madereva wake ni wagen kiasi kwamba hawajui hilo eneo??
ama je wanadharau alama za barabaran zilizoko hapo maeneo?? ama hakuna alama za kutosha kuongoza magari eneo hilo??
 
Dah! Siku ya ajali hii nilipita hapo,nilikuta basi hili likiwa katika hali hiyo na tuliambiwa mtu mmoja amefariki! Ilikuwa mbele kidogo tu ya kituo cha polisi Kabuku. Na leo tena!
Tarehe 9.10.2013 lilipata ajali eneo hilo hilo.

Picha ya basi la kampuni ya Burdan linalofanya safari za Lushoto-Korogwe (Tanga) na Dar es Salaam limepata ajali katika eneo la Kabuku, Handeni wakati likielekea Dar es Salaam. Taarifa za watu wa maeneo hayo zinasema mtu mmoja ameripotiwa kufa huku wengine wakiachwa na majeraha. Kandili Yetu Leo: PICHA: AJALI MBAYA YA BUS LA BURDAN, HANDENI MKOANI TANGA

NA leo tena. RIP
 
Wanabodi,

Kumetokea ajali mbaya ya basi huko Korogwe!.
Watu 11 wafariki papo kwa papo!.

Source: Radio One Breaking News!.
Pasco
 
Sad news! I have long drive on 20th Dec, will be driving more than 2600Km. Dah mapka naogopa!!!!
 
Sad news! I have long drive on 20th Dec, will be driving more than 2600Km. Dah mapka naogopa!!!!

Kaka unatoka wapi kwenda nchi gani, maana hakuna umbali huo kutokea mkoa wowote kwenda mkoa wowote nchi hii..

Inasemekana sehemu ambayo ni mbali sana kutokea Dar es salaam ni kigoma na ni Km 1500 tu, dar musoma km 1400, dar-bukoba km almost 1500 sasa wewe hizo km 2600 unatoka mkoa gani na unakwenda mkoa gani?

Na kiusalama na kiafya sidhani kama ni sahihi kwa dereva mmoja kuendesha umbali wote huo peke yako
 
Mh! Na huu mwisho wa mwaka! Natamani tu nijifungie ndani! Aisee so sad jamani! Poleni wafiwa wote! Hapo lazima kutakuwa na watoto/vijana ambao ndio taifa la leo na kesho dah!
 
Kwa nini ajali huwa nyingi sana kipindi hiki cha mwisho wa mwaka?
R.I.P marehemu.
 
R.I.P na haihai kwa majeruhi wote pamoja wana Korogwe kwa ujumla maana huo ni mcba wetu sote
 
Back
Top Bottom