Ajali mbaya Handeni, basi la Burudani limeua 12

Otatenaneeee. Burdan nkwai? Nkwai? Hili basi linapendwa sana na ndugu zangu wa pale Korogwe. Sijui sababu ni nini? Ngoja niwatafute ndugu zangu maana moyo unanienda kwa kasi mno

Eka du maya,zumbe na atiambize du.
 
Marehemu wote mpumzike kwa amani na majeruhi mwenyezi Mungu awaponye haraka.

Nimesafiri mara kadhaa na hili basi la burudani na nilichogundua kama huna roho ngumu huwezi ulipanda.Imagine tulikuwa tukitoka Dar saa 9 mchana na saa 2 usiku tupo Lushoto.

Huko njiani inakuwa balaa tupu na usiombe mfike milima ya Usambara yaani utatamani ushukie njiani usiku huo.
 
Dah..sina ndugu kweli hapo..basi la nyumbani hili..majeruhi wapone haraka..na waliopoteza uhai Mungu awaweke panapostahili.
 
Msiba ni wangu kabisa huu,mji mzima Leo utakuwa majonzi tupu,poleni sana wana Korogwe
 
Nimepokea taarifa basi burdani likitokea korogwe asubuhi ya leo limepata ajali maeneo ya kabuku na inasemekana zaidi ya abiria 22 wamefariki hapo hapo

Uwe unasikilza taarifa ya habari vizuri na sio unarukia rukia tuu. 22 hao wakwako, ni 22 mzee.
 
Tarehe 9.10.2013 lilipata ajali eneo hilo hilo.

Picha ya basi la kampuni ya Burdan linalofanya safari za Lushoto-Korogwe (Tanga) na Dar es Salaam limepata ajali katika eneo la Kabuku, Handeni wakati likielekea Dar es Salaam. Taarifa za watu wa maeneo hayo zinasema mtu mmoja ameripotiwa kufa huku wengine wakiachwa na majeraha. Kandili Yetu Leo: PICHA: AJALI MBAYA YA BUS LA BURDAN, HANDENI MKOANI TANGA

NA leo tena. RIP

Mkuu nakwambia haya majanga si madogo.
Na leo tena nasikia kuna ajali nyingine njia hiyo hiyo. Siku si nyingi utasikia watu wanashuhudia katika majukwaa ya kwamba tulitumwa kufanya ajali kisa wanataka damu kule kuzimu. Nasema na WASHINDWE kwa jina lake Bwana aliye hai na hata sasa!

Wote wale waliopata na mauti Mwenyenzi MUNGU na awape pumziko la milele katika shamba lake Bwana wetu! Na majeruhi wapone mapema!
 
Marehemu wote mpumzike kwa amani na majeruhi mwenyezi Mungu awaponye haraka.

Nimesafiri mara kadhaa na hili basi la burudani na nilichogundua kama huna roho ngumu huwezi ulipanda.Imagine tulikuwa tukitoka Dar saa 9 mchana na saa 2 usiku tupo Lushoto.

Huko njiani inakuwa balaa tupu na usiombe mfike milima ya Usambara yaani utatamani ushukie njiani usiku huo.

ingawa wanasema ajari haina kinga, lakn magari haya yamezidi mwendo. ugua pole majeruh na waliokufa wasamehewe
 
Mkuu nakwambia haya majanga si madogo.
Na leo tena nasikia kuna ajali nyingine njia hiyo hiyo. Siku si nyingi utasikia watu wanashuhudia katika majukwaa ya kwamba tulitumwa kufanya ajali kisa wanataka damu kule kuzimu. Nasema na WASHINDWE kwa jina lake Bwana aliye hai na hata sasa!

Wote wale waliopata na mauti Mwenyenzi MUNGU na awape pumziko la milele katika shamba lake Bwana wetu! Na majeruhi wapone mapema!

Poleni wafiwa na majeruhi
 
He kafara mwisho wa mwaka?
kweli yonyesha ni kafara, jana usiku niko mahala tanga pale naongea mshikaji derva tax anasema jamaa kweli kafanya kafara,kaleta gari mbili mpya kabisa na next zaweza anza kazi....
 
Back
Top Bottom