Freesociety
JF-Expert Member
- Jul 19, 2017
- 943
- 888
Mauritius wanatulisha ndege kubwa hivyo sisi tunashindwa? Kha! Kazi mapangaboy tu.A380 imetua JNIA kwa dharura kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya huko Mauritus ilikokuwa ikielekea.
---------
Ndege kubwa aina ya Airbus A380 mali ya Shirika la Ndege la Emirates imetua kwa dharura katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) uliopo jijini Dar es Salaam, baada ya kushindwa kutua Mauritius kutokana na hali mbaya ya hewa.