Aibu nyingine ya serikali: Haina pesa kuendesha mitihani ya Taifa kidato cha pili mwaka huu

jibu hapo ni kufuta NECTA na kuruhusu kila shule ijitungie mitihani yake kama vyuo vikuu..........................tangia tuwe na mitihani ya kitaifa sijaona maendeleo yoyote.......................kenya wanajadili kufuta mitihani ya kitaifa..................na kuacha kila shule ijipime yenyewe.................huo utakuwa mwisho wa wizi wa mitihani......waajiri itabidi watafute utaratibu wa kupima uwezo wa wahitimu ingawaje tunafahamu ya kuwa bado kuna upendeleo mkubwa huko..........
 
Kwa uelewa wangu huu mtihani ulifutwa miaka michache iliyopita,unarudishwa tena mwaka huu sababu kubwa ni matokeo mabovu ya kidato cha nne mwaka jana ambako takribani nusu ya watahiniwa walipata division 0. Sababu kubwa ilidaiwa ni kuondolewa kwa huo mtihani.

mkuu huu mtihani haukufutwa watoto walikuwa wanaserereka mpaka kidato cha 3. Sema mwaka hu ndo wamesema wanaanza mchujo. Mchujo haukwepo awali. Ila yatakuwa yaleyale mwalimu mmoja anafaulisha darasa zima kwangu mi maajabu au we kwako imetulia.!?
 
Sasa wanzengu mtamulaumu nani?Nchi yenu haina serikali wala rais teh mnaishi kwenye kufikirika bora sisi wazenjibari.
 
Hata ikivuja haisaidii kwani siku hizi akuna anayeshindwa kuendelea form 3 kwa kufeli form 2. nchi hiiiiiiiiiiiiii, tutafika tu
 
Taarifa kutoka kwa walimu wakuu wa shule za sekondari na wasimamizi wa mitihani wa Kanda ya Mashariki iliyofanyika jana katika shule ya sekondari ya Kilakala, wameelezwa kuwa TAMISEMI wametoa pesa kidogo sana ambazo hazitoshelezi uendeshaji wa mitihani hiyo. Hata wanasema hao walikaa kwenye semina hiyo hata bila ya kupata maji ya 200 ya kunywa, chai wala chakula.

Wakuu wa shule za Manispaa wameelezwa kuifata mitihani hiyo kwa usafiri wa kujitafutia wenyewe walielezwa na Afisa Elimu Manispaa hiyo kuwa hana pesa ya mafuta kusambaza mitihani hiyo. Hakutakuwa na pesa za kulipa wasimamizi wasaidizi na wakuu wa shule kutoka serikalini.

Dalili zinaonesha kuwa usiri wa mitihani huenda ukawa mdogo sana.

Huenda ikavuja sana.
Jamani hili swala watu wanaweza kulichukulia kimzaamzaa, inasemekana serikali ipo taabani sana kifedha. TRA wanakusanya pesa kidogo sana(Uchumi umedorora), kuna nyepesi nyepesi kwamba katika bajeti ya mwaka huu ni fungu moja tuu ndiyo linapata pesa za OC kama walivyoomba na fungu hilo ni Fungu namba 20, wanaofanya serikalini wanafahamu Fungu namba20 ni Ikulu. Wengine woote wana Haha namna ya kuziendesha ofisi zao. Juzi nimepita maeneo ya TFDA nikamsikia mkaka mmoja anataka kuacha kazi anasema hawajapata OC toka mwezi wa nane, anadai ufanyaji wa kazi umekuwa mgumu sana. Nilipita maeneo ya Wizara ya nishati nikamsikia mtu analalamikia kutokuwa na Vitendea kazi kama Stationaries sababu kubwa ikiwa ni kutokupata OC. Kuna jamaa naye yupo serikalini nimesikia anahaha kwamba almanusura mwezi huu wasipate mshahara anadai amepata mshahara wake wa October jana tarehe3 November Sijui watakuwa wamekopa tena Exim?????

Note: OC=Other charges
 
jk akipunguza safari zake za nje mbili tu mitihani inaweza chapishwa,hii nchi cjui Mungu atatusaidiaje tuondokane na umasikini huuView attachment 40556

ni shule ya wapi hii? hakika nimesikitika mno.Nape kaiona? maana yuko mstari wa mbele kueleza mafanikio yao binafsi ya miaka 50 ya uhuru. nawapa pole hawa watoto na kuwatia moyo kwa hali hiyohiyo wasome kwa bidii na mwalimu wao ataingia mbinguni
 
Mkuu nlipokuwa nasoma masikitiko yako na huruma juu ya yiyo shule, mwishoni nimejikuta navunjika mbavu baada ya kusoma ''NA MWL WAO ATAINGIA MBINGUNI" du!
 
Kwanza mitihani yenyewe siku hizi wastani umeshushwa hadi ziro. Ukiandika tu jina umefaulu.!
 
Ndo tanzania hiyo kikwete yuko bze kwenda kubembea'pinda hana sauti'membe na ghadaf na ushoga'mkullo hajui kwanin thaman ya sh inaporomoka'sitta yuko bize na visasi'shukuru kawamba kasema serikal haina hata ela za mikopo kwa watz'spika wa bunge yuko bize na cdm'nadhona yuko bize na lema'
hakuna hata kiongoz mmoja wenye interest na taifa

ukweli mtupu
 
Taarifa kutoka kwa walimu wakuu wa shule za sekondari na wasimamizi wa mitihani wa Kanda ya Mashariki iliyofanyika jana katika shule ya sekondari ya Kilakala, wameelezwa kuwa TAMISEMI wametoa pesa kidogo sana ambazo hazitoshelezi uendeshaji wa mitihani hiyo. Hata wanasema hao walikaa kwenye semina hiyo hata bila ya kupata maji ya 200 ya kunywa, chai wala chakula.

Wakuu wa shule za Manispaa wameelezwa kuifata mitihani hiyo kwa usafiri wa kujitafutia wenyewe walielezwa na Afisa Elimu Manispaa hiyo kuwa hana pesa ya mafuta kusambaza mitihani hiyo. Hakutakuwa na pesa za kulipa wasimamizi wasaidizi na wakuu wa shule kutoka serikalini.

Dalili zinaonesha kuwa usiri wa mitihani huenda ukawa mdogo sana.

Huenda ikavuja sana.

Haya ndiyo matokeo ya serikali isiyokuwa na vipau mbele. Ningeshauri utoe takwimu za fedha kiasi gani kinachohitajika kwa ajili ya kugawanya hiyo mitihani ili uone madhara ya nchi kukosa mwelekeo.
 
walishainyongelea mbali zamani sana. Kuirudisha ni kuwalazimisha tu. Na kinachofanyika sasa ni kuijengea tena mazingira ya kuirudisha ahera
 
Ingekuwa vyema kwa UK kukata hii misaada ili serikali iwe responsible zaidi kukusanya mapato (KODI). Michezo michafu inafanywa na serikali ikijua kuwa kuna hela ya misaada from wahisani.
 
Tumethubutu,tumeweza ,tunasonga mbele na ujinga wetu,misaada itakatwa tu labda tusign mou na mashoga wa cameroon
 
Jamani uchumi wa dunia umeyumba. Haya yanayotokea Tanzania pia yanatokea kwenye nchi za wenzetu. Hakuna sababu ya kuitupia serikali lawama kwa kila kitu. Tupevuke akili na tuangalie mambo kwa mapana zaidi. Imekuwa ni hulka ya JF kuishutuma serikali na viongozi wake wa juu kwa kuwatupia lawama na kejeli. Hivi ina maana hakuna jambo jema hata moja ambalo serikali tawala imetenda kwa wananchi wake?. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Mkuu, ili nchi iendelee pamoja na mambo mengine (uongozi bora, matumizi bora ya mali asili) inahitaji WATU ambao ni productive baada ya kuwekeza kwenye elimu iliyo bora. Kwa ufupi Elimu Kwanza.
 
Ndo tanzania hiyo kikwete yuko bze kwenda kubembea'pinda hana sauti'membe na ghadaf na ushoga'mkullo hajui kwanin thaman ya sh inaporomoka'sitta yuko bize na visasi'shukuru kawamba kasema serikal haina hata ela za mikopo kwa watz'spika wa bunge yuko bize na cdm'nadhona yuko bize na lema'
hakuna hata kiongoz mmoja wenye interest na taifa

Hiv kwan waTZ tunasoma kwa faida gan? Muulize Kawambwa swal hli kama hatasema ume2mwa na CDM na kituo cha HAKIELIMU.
 
Back
Top Bottom