Aibu nyingine ya serikali: Haina pesa kuendesha mitihani ya Taifa kidato cha pili mwaka huu

natamani nirudi utotoni ili nipate masomo yote As na gpa ya 5 chuo kikuu, lol mbona kizazi cha sasa kinafaidi hivi!
 
pesa za posho za vikao na safari pia za kuadhimisha 5
yrs of indemonie zipo! Lakini ya mitihani hamna!
 
Hii sasa ni balaa, mbona pesa za kusherehekea miaka 50 ya uhuru zipo?

Unashangaa hizo na zile wanazonunulia majumba USA je?pesa zipo nyingi tu ila kwa CCM tu wengine haziwahusu kabisa.
 
huu mtihani una umuhimu gani si ungefutwa tu. Kuna shule moja ya kata huko mkuranga mwaka jana ilikuwa na mwalimu mmoja tu tena wa kujitolea ilifaulisha wanafunzi wote kwenda kidato cha tatu. Huyu mwalimu inavyoonekana ana kipaji cha kufundisha, darasa zima linafaulu du.!!!
 
zilitumika kwenye uchaguzi mdogo wa igunga pamoja na safari za mkuu wa kaya
 
Mtihani wa FORM TWO una faida gani? mbona vilaza wote huenda hadi FORM FOUR. Bora wakose hiyo fedha maana hauna faida wala sijui wanapima nini na halafu iweje.
 
Jamani uchumi wa dunia umeyumba. Haya yanayotokea Tanzania pia yanatokea kwenye nchi za wenzetu. Hakuna sababu ya kuitupia serikali lawama kwa kila kitu. Tupevuke akili na tuangalie mambo kwa mapana zaidi. Imekuwa ni hulka ya JF kuishutuma serikali na viongozi wake wa juu kwa kuwatupia lawama na kejeli. Hivi ina maana hakuna jambo jema hata moja ambalo serikali tawala imetenda kwa wananchi wake?. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Ndo tanzania hiyo kikwete yuko bze kwenda kubembea'pinda hana sauti'membe na ghadaf na ushoga'mkullo hajui kwanin thaman ya sh inaporomoka'sitta yuko bize na visasi'shukuru kawamba kasema serikal haina hata ela za mikopo kwa watz'spika wa bunge yuko bize na cdm'nadhona yuko bize na lema'
hakuna hata kiongoz mmoja wenye interest na taifa

nimeipenda sana.
 
Pesa za kuwasomesha watu watatu wa TCRA zipo
Pia Bil 1.4 ya kufanyia matengenezo nyumba ya mkuu wa mkoa wa mtwara ipo
Ila za shule na mitihani zimeisha wakuu tufunge mikanda
 
Mtihani wa FORM TWO una faida gani? mbona vilaza wote huenda hadi FORM FOUR. Bora wakose hiyo fedha maana hauna faida wala sijui wanapima nini na halafu iweje.

Ni kweli mtihani wa kidato cha pili hauna maana? Kama umesoma basi haukuelimika.
 
huu mtihani una umuhimu gani si ungefutwa tu. Kuna shule moja ya kata huko mkuranga mwaka jana ilikuwa na mwalimu mmoja tu tena wa kujitolea ilifaulisha wanafunzi wote kwenda kidato cha tatu. Huyu mwalimu inavyoonekana ana kipaji cha kufundisha, darasa zima linafaulu du.!!!

Kwa uelewa wangu huu mtihani ulifutwa miaka michache iliyopita,unarudishwa tena mwaka huu sababu kubwa ni matokeo mabovu ya kidato cha nne mwaka jana ambako takribani nusu ya watahiniwa walipata division 0. Sababu kubwa ilidaiwa ni kuondolewa kwa huo mtihani.
 
dah hv? Hawa jamaa ni matahira pesa wamepupa kwny maonesho ya wizara eti maadhimisho ya uhuru.miaka 50 ya ukoloni mamboleo
 
Ila nchi hii kipindi hiki dah, as if inaongozwa na watoto na si watu wazima. Kwani si walishaandaa na kupitisha bajeti zote-za wizara husika na serikali kwa ujumla, hawakujua kama kuna mitihani itapaswa kufanyika??! Na si ni hao waliopanga hiyo mitihani iwepo??! Wamelazimisha kila Wizara ifanye maadhimisho ya sherehe za miaka 50 wakaacha mambo ya msingi yanayomgusa mwananchi moja kwa moja kama haya!

Kuna haja gani ya kuwa na Viongozi sasa, si bora tujiendeshe tu
 
Taarifa kutoka kwa walimu wakuu wa shule za sekondari na wasimamizi wa mitihani wa Kanda ya Mashariki iliyofanyika jana katika shule ya sekondari ya Kilakala, wameelezwa kuwa TAMISEMI wametoa pesa kidogo sana ambazo hazitoshelezi uendeshaji wa mitihani hiyo. Hata wanasema hao walikaa kwenye semina hiyo hata bila ya kupata maji ya 200 ya kunywa, chai wala chakula.

Wakuu wa shule za Manispaa wameelezwa kuifata mitihani hiyo kwa usafiri wa kujitafutia wenyewe walielezwa na Afisa Elimu Manispaa hiyo kuwa hana pesa ya mafuta kusambaza mitihani hiyo. Hakutakuwa na pesa za kulipa wasimamizi wasaidizi na wakuu wa shule kutoka serikalini.

Dalili zinaonesha kuwa usiri wa mitihani huenda ukawa mdogo sana.

Huenda ikavuja sana.

Tumethubutu, tumeweza na tunazidi kusonga mbele!
 
Uk wasitishe hiyo misaada tuone kama tuna uwezo wa kufikiria nje ya misaada

Mwanakijiji, inatakiwa misaada yote isitishwe ili tujipime kujitegemea. Nimefurahi sana Membe alivyotumia hii nafasi ya kujipigia kampeni kukataa ushawishi wa kuwa mashoga. Ingekuwa vyema kama tungeweza kumshawishi Cameron atie ngumu na kukata msaada wote tukwame jumla. Mabadiliko hapa hayaji bila kila kitu kukwama jumla.
 
Back
Top Bottom