Aibu kubwa kwa polisi - hadi sasa wachoma makanisa Zenj na waliomteka Ulimboka hawajakamatwa!

una maana gani unaposema shinikizo toka juu kwa manufaa ya walio juu

Wale majambazi waliowavamia watalii na kufanikiwa kuiba/kuua walishakamatwa siku nyingi vipi kuhusu hawa waliomdhuru Dkt Ulimboka mbona hakuna hata mmoja aliekamatwa walau hata kwa kuhojiwa tu?,wewe inakuingia akilini kweli au unanichungulia!!!!Bunge linazuiwa kujadili mgomo Wa Madaktari(tunaoathirika ni sisi walalahoi)upande wa pili Serikali nayo inawatimua kazi madokta/inawafutia leseni vipi wewe hujiuluzi wewe mwenyewe kwa nini Serikali inajitahidi/inatumia nguvu
sana kulificha suala hili la mgomo Wa madaktari?
 
Kazi kubwa ya polisi ni kukamata wapiga filimbi (whistleblowers) katika vita dhidi ya ufisadi. Katika watu walionilet down ni sadi Mwema, nilifikiri angemtolea nje yule Omar Mahita kwa utendaji wake kazi.

Kumbe naye ni mfata amri za wakubwa tu, professionalism yake ameisalimisha kwa watu vigogho wa CCM!
 
Tumechoka na POLICCM wanaoendeshwa kwa pua na matajiri (aka vigogo) wa chama cha mabwepande!
 
Usiku huu Channel 10 imetangaza kwamba watu kadha wamekamatwa mkoani tabora kwa kosa la kuuwa watu wawili. Polisi wamawekamata hao siku moja tu baada ya tukio!
 
Policcm kweli! Watesaji watu na wachoma majengo (hawa nao ni wauwaji tu) hawakamatwi, lakini anayetoa taarifa kutaka kudhuriwa ndiyo wanakamatwa! shame upon you CCM govt!
 
Leo hii ni karibu miezi miwili na nusu tangu makanisa yachomwe huko Zanzibar na 'watu wasiojulikana'. Na vile vile ni karibu wiki tatu tangu Dr Ulimboka akamatwe na 'watu wasiojulkana na kupigwa vibaya.

Matukio yote mawili jeshi letu la polisi lilidai kuwa lingefanya uchunguzi wa kina na kuwakamata wahusika na kuwapeleka katika vyombo vya sheria, lakini hata mtu mmoja hajakamatwa.

Hii jamani siyo aibu kubwa kwa jeshi letu la polisi ambalo juzi tu waziri wao, Dr Nchimbi alijidai ni jeshi makini na kwamba yoyote asiyeliamini ana matatizo?

Zanzibar ni sehemu ndogo sana na watu wachache ambao wengi wanajijua. Inakuwaje hadi sasa polisi imeshindwa kuwakamata wahusika wa uchomaji wa makanisa?

Au sasa tuanze kuamini yanayozungumzwa sana, tena sana mitaani kwamba kuna mkono wa serikali katika matukio yote mawili, na polisi kazi yake ni kuilinda tu serikali kwa maovu hayo?

hawa polisi wetu ni marobot wa CCM.
 
Ndio maana anakuwa mhalifu sugu. Angekuwa jela huo uhalifu angeufanya saa ngapi? umesahau, kuna mmoja kakataa hata dhamana ili akawatembelee wenzake jela?

sasa naanza kuamini jeshi la polisi dhaifu kwani wasingekuwa dhaifu hao waalifu sugu wasingekuwepo.
 
Hakuna iliye juu ya sheria ni mashaka yako tu.

TISS imeundwa kisheria hivyo kinyume chake ni kukiuka sheria..... polisi hawawezi kushindwa kuwakamata.

Tumeshuhudia wanajeshi (JWTZ) na TISS wamekamatwa na kufikishwa mahakamani.

post yako inataka kuonyesha kuwa TISS wanaweza kufanya lolote na wasiguswe na sheria si kweli.

Pole ndugu!! labda unaishi mwezini!! huko unaiona TZ yenye utawala wa kisheria!! Niambie wauaji wa General Kombe wako wapi? kwa ufahamisho wako waliachiwa kwa msamaha wa "rais". Zombe yuko anapeta!! Hebu nifanunulie kisa cha mchezo wa Kova na kichaa kutoka kenya Muhindi" eti sasa tusiseme suala liko mahakamani! crazy!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom