Ahadi ya ajira milioni moja changa la macho?

Nimesoma uchumi bado nasomo haya yote hayawezi kufanya taifa na kufanikiwa na pia kama vile multiplier effect kwenye uchumi wetu na pia labda anasema hivi ili mwaka huu usiwe mgumu kwake na kuwafanya watanzania na kusema ukweli kabisa
 
It is very funny, maana hata marekani yenye uchumi mkubwa kuliko nchi zote, yenye watu zaidi ya milion 300 haijaweza kufanya hayo maajabu. Nchi zilizoendelea ajira 1000 huwa hata waziri husika anatoa tamko, kwa maana ni mafinikio yasiyo kidogo.

Turudi bongo, ni kwamba baada tu ya JK kutangaza hiyo ahadi wizara ya Kapuya ikaingia kazini, Kila mwajiri alilazimika kusubmitt no ya watu alioajiri kwa mwezi regardless ni permanent, kwamkataba au kibarua. Hawa jamaa walikuwa happy kuona tu namba inaongezeka na hivyo kumfurahisha bosi. Nakumbuka one time nikiwa bongo in one of the consulting firms tulipewa kazi kwenye one of the mines. Tukaajiri watu 6 for like 6 weeks, baadae nillitwa HR dept kwa ajili ya details za hao watu. Nilipoulizwa why nikaambiwa zinatakiwa wizara ya kazi ili kujua ni ajira ngapi zimezalishwa. I told them but this is temporary wakasema hata kama ni siku moja, data need to be submitted as per maagizo ya wizara.

ISSUES:

1. Je ni ajira ngapi zimepotea katika utaratibu huo huo unaotumiwa na wizara ya kazi in these four years?

2. Nna amini kabisa hata JK haamini hizi takwimu pamoja na kwamba ni ahadi aliyotoa yeye. I am sure akibanwa kwenye 18 atairuka kama alivyoiruka ilani ya uchaguzi ya CCM.

3. Je ni indicators zipi zinasupport kuzalishwa kwa hizo ajira? It is funny kuona kwamba NSSF ambao ndiyo mfuko mkubwa wa social security na hasa kwa private firms, idadi ya member wake ni kama 500,000 tu an increase of about 60,000 kwa miaka minne. Sasa hawa waajiriwa wapya wako mifuko ipi ukizingatia mfuko kama LAPF member hawafiki hata laki mbili.

4. Hivi Kapuya na watu wake wanafahamu milioni moja maana yake ni nini wasije wakawa wanachanganya na 1000 kama ndugu zetu wa nyumba ya Gavana. Anyways kwa ufafanuzi zaidi, watu milioni ni sawa na abiria kutosha vipanya 50,000 au nchi nzima ya Botswana, au idadi ya wananchi wote mkoa wa Rukwa au Ruvuma. Ukikusanya hao waajiriwa wapya ni wengi kuliko watu wote mkoani Lindi.

5. Akina Kapuya wanweza kumegamega hizo takwimu zao at least tukajua kila wilaya zimezalishwa ajira ngapi?

6. Kapuya mwenyewe kama waziri wa kazi and in this sense the smartest in the world amezalisha ajira ngapi jimboni kwake?

Mkuu umesema sawa kabisa.

Ukweli ni kwamba hawa wanasiasa wetu wameanza kutunga uongo wa kuombea kura. Wanajua vyema kuwa si rahisi kuunganisha dots (kwa wapiga kura wa vijijini). Wanapika data za uongo kabisa. Kwakuwa naamini si kweli kuwa kuna ajira mpya zilizopatikana. Ni kuajiri kwa masaa tu.

Unawezaje kuwa na ajira mpya zaidi ya milioni moja halafu zisionekane? Kuna Watanzania wangapi wanaohitimu vyuo ambao hawajapata kazi hadi leo? Je, hao wanaoajiriwa wanatoka wapi? Au ni waKenya wanaoongezeka nchini kila siku?

Ningeelewa zaidi kuhusu ongezeko la ajira mpya milioni moja kama wangeonyesha ni vyanzo vipi vipya vya ajira vilivyojitokeza katika kipindi cha miaka minne. Sioni uwekezaji mpya (hata JK amethibitisha), sioni hali bora ya uchumi unaoruhusu ongezeko kubwa kiasi hicho la ajira (hilo pia JK amelisema). Sasa wamewezaje kuongeza ajira?

Vinginevyo, kwa hali ya uchumi usioridhisha, na kama kweli wameweza kuongeza ajira kiasi hicho, basi ni dhahiri hali yetu ya uchumi itakuwa mbaya zaidi katika kipindi kijacho kuanzia mwaka huu. Inaonyesha matumizi mabaya ya serikali. Kwani kwa kuongeza ajira bila kuongeza ufanisi, ni dhahiri kabisa kuwa Taifa linapata hasara kwa matumizi ya nyongeza yanayosababishwa na ajira hizo.
 
Mkurugenzi Mwanakijiji:

Mimi sio msomi wa uchumi. Lakini idadi ya wanaofanyakazi inaweza kupimwa kwa kutumia payrolls za waajiri. Watu wanapolipwa mishahara rasmi ni lazima wailipe kodi serikali. Na ukihesabu waliolipa kodi kupitia mishahara yao, serikali inaweza kujua walipaji kodi kutokana na mishahara wameongezeka kiasi gani.

Kwa nchi kama Tanzania ajira ambayo mambo mengine yanaendeshwa katika sekta zisizo rasmi, njia kubwa moja ya kuongeza idadi ya wafanyakazi rasmi ni kuongeza matumizi ya serikali katika sekta za huduma ya jamii. Miongoni mwa sekta hizo ni elimu na Afya. Katika elimu, serikali iliongeza sekondari za kata, lakini sidhani kama ajira zilikuwa nyingi. Vilevile ujenzi wa mabarabara katika sehemu mbalimbali.

Na kama waliochukua mikopo ya Mabilioni ya JK, walifungua biashara zao na kujitegemea basi tunaweza kusema kuwa nafasi za kazi ziliongezwa kwa sababu huwezi kukopa na kurudisha bila kuwa-productive labda upate ucheze upatu wa DECI.

Kwa kumalizia tu, huwezi kupima ongezeko la nafasi za kazi wakati wanasiasa wanashindwa kuchukua majukumu ya kuanzisha masoko yalio rasmi.

Mabilioni ya JK ni zoezi lililoshindwa kabisa. Asilimia kubwa ya waliokopa hawakurudisha, na wengine walisema hizo zilikuwa ni shukrani za JK kuchaguliwa.

Biashara nchini zinadorora sana. Wafanya biashara wengi wanalalamika na wengine kufunga biashara zao. Serikali hailipi madeni ya wafanya biashara wanaoipa huduma. Sioni kwa kweli ongezeko la ajira linatoka wapi.
 
Kwanza samahani.

Kuelewa ongezeko la ajira hizo, inafanana kidogo na kuelewa maarifa ya kuruka na ungo.

Wakati wazungu wanatumia theories/models zao kutengeneza ndege, na tukaiona inaruka; sisi kwetu tunahitaji imani tu kwamba kuna namna ya kuruka na ungo kwenda kokote unakotaka. Ungo mmoja unatosha kubeba watu hata kumi
 
Hivi karibuni, Rais Jakaya Kikwete wakati akiwa katika ziara mjini Arusha alitangaza kuvuka lengo la ajira 1,000,000 alizoahidi katika kipindi chake cha kwanza kwa ajira 200,000.

Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Omary Yussuf Mzee alisema ajira hizo zimepatikana kutoka taasisi za serikali na sekta binafsi.

Ajira 1,185,387 zilipatikana kutoka katika sekta binafsi hasa kwenye kilimo, 965 taasisi za serikali na 85, 571 zilitoka serikalini.

Wabunge wameitaka Wizara ya Fedha na Uchumi kutoa mchanganuo wa ajira 1,271,923 ambazo zilitangazwa kupatikana katika kipindi hicho.

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Bw. Hamad Rashid Mohamed ameitaka serikali kutoa mchanganuo wa ajira 1,185,387 ambazo zilipatikana kutoka katika sekta binafsi.

"Napaenda kuipongeza taarifa hii imeandikwa vizuri lakini kuhusu ajira 1,185,387 ingekuwa vema kama serikali ingetoa mchanganuo katika ajira hizi zimepatikana vipi," alihoji Bw. Mohamed.

Alisema, hadi sasa ni vigumu kuamini kuwa kuna ajira hizo, kwani hakuna mchanganuo halisi unaoonesha kuwa kuna vijana katika idadi hiyo wamejiajiri ndani ya kipindi cha miaka minne ya awamu ya uongozi wa Rais Kikwete, hoja iliyoungwa na wabunge wengi ndani ya kikao hicho.

Unasemaje mwanaJF mimi binafsi bado najiuliza eti 93% ya ajira zote zimetokana na watu binafsi kujiajiri ndiyo kusema ahadi ya rais imejazwa na wananchi waliojiajiri tu hasa kwenye kilimo?

Katika nchi za wenzetu mahesabu ya ajira yanahusisha pia ajira zilizopotea (unemployment figure) ndipo unapata mahesabu kamili ya ajira zilizopatikana, ina maana sisi tumetengeneza ajira tu hakuna tulizopoteza?
 
we kuwa mvumilivu kidogo jibu la swali lako atalijibu yy mwenyewe jk kwenye kampeni na atakaposema kwamba amevuka kile kiwango alicho sema usishangae kwani ndo siasa za tanzania unaongea lolote watu wanapiga makofi akuna kuhoji wala nn yani ni raha tuuuuuuuu
 
Ajira mil. 1.2 za JK zazua maswali http://www.majira.co.tz/index.php?v...swali&format=pdf&option=com_content&Itemid=57 http://www.majira.co.tz/index.php?v...nt&print=1&page=&option=com_content&Itemid=57 http://www.majira.co.tz/index.php?o...hbGkmb3B0aW9uPWNvbV9jb250ZW50Jkl0ZW1pZD01Nw== Wednesday, 20 January 2010 09:49 Na Edmund Mihale
Majira

WABUNGE wameitaka Wizara ya Fedha na Uchumi kutoa mchanganuo wa ajira 1,271,923 ambazo zilitangazwa kupatikana katika kipindi cha miaka minne ya utawala wa awamu ya nne wa Rais Jakaya Kikwete.

Hoja ya kutaka mchanganuo huo ilijitokeza katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi wakati Wizara ya Fedha na Uchumi ilipokuwa ikiwasilisha mmelekeo wa utekelezaji wa awamu ya pili ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA-II).

Akiwasilisha taarifa hiyo Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Omary Yussuf Mzee alisema ajira hizo zimepatikana kutoka taasisi za serikali na sekta binafsi na taasisi za serikali.

Akitoa ufafanuzi wa mchanganuo wa ajira hizo, Bw. Mzee alisema kuwa ajira 1,185,387 zilipatikana kutoka katika sekta binafsi, 965 taasisi za serikali na 85, 571 zilitoka serikalini.

Hata hivyo pamoja na maelezo hayo, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Bw. Hamad Rashid Mohamed aliitaka serikali kutoa mchanganuo wa ajira 1,185,387 ambazo zilipatikana kutoka katika sekta binafsi.

"Napaenda kuipongeza taarifa hii imeandikwa vizuri lakini kuhusu ajira 1,185,387 ingekuwa vema kama serikali ingetoa mchanganuo katika ajira hizi zimepatikana vipi," alihoji Bw. Mohamed.

Alisema, hadi sasa ni vigumu kuamini kuwa kuna ajira hizo, kwani hakuna mchanganuo halisi unaoonesha kuwa kuna vijana katika idadi hiyo wamejiari ndani ya kipindi cha miaka minne ya awamu ya uongozi wa Rais Kikwete, hoja iliyoungwa na wabunge wengi ndani ya kikao hicho.

Wabunge waliokubaliana na hoja hiyo ni Bw. Siraju Kaboyonga (Tabora Mjini) na Bw. Athumani Janguo (Kisarawe), wote kutoka CCM.

Hivi karibuni, Rais Jakaya Kikwete wakati akiwa katika ziara mjini Arusha alitangaza kuvuka lengo la ajira 1,000,000 alizoahidi katika kipindi chake cha kwanza kwa ajira 200,000.
 
Hivi karibuni kila mkoa ulianza kwa kupewashillingi billioni moja kwa ajili ya huo mpango, sasa labda mtakumbuka huko nyuma niliuliza je mikoa inaweza kweli ku-create ajira?

kwa hiyo kwenye hilo yuko Mzee JK, yuko sambasamba nalo ila swali ni kwamba kama mikoa ina huo uwezo?
Tatizo sio JK nadhan tatizo ni watumiaji wa hizo fedha. Kabla hujakopesha unapeleka mchanganuo wako, wenye lugha yao wanaita Business plan. Ikiwakomvinsi watoa pesa unapewa pesa. Sasa kama unataka na Rais aje kukusimamia kama umenunulia ulanzi au umenunua selula tutakuwa hatumtendei haki.

ila mapungufu yapo kila sehemu, zile bilioni za kila mkoa zilizalisha inflation zaidi kuliko ajira!
 
kuzalisha ajira wakati serikali inajitoa ktk uzalishaji is great joke, serikali ina incourage watu tuwe wamachinga kwa kutubadilisha jina eti wajasiriamali, source za ajira kubwa ni ktk mashirika tu ambayo serikali imeapa haitajiusisha nayo, serikali inataka kazi yake ni kukusanya kodi tu na kuimarisha ulinzi( ili kuwalinda wawekezaji pale wananchi wataposhindwa kuvumilia unyonyaji).

jk ni msanii yeye anaangalia kwa mda uo nini ni talk of the town then anare adress na kuwaridhisha watu hana maamuzi magumu, cjui ktk kipindi chake ana investment gani kubwa iliyofanyika au kuanzishwa sasa izo ajira atazitoa wapi?
 
Jamani eeeh,kwa wale walioielewa vizuri BODMAS(MAGAZIJUTO) na hakika kabisa hawawezi tia lawama juu ya hili,kama mna kumbukumbu nzuri,Jk alisema atatoa ajira milioni hiyo,sasa kama mliielewa vizuri MAGAZIJUTO kinawatatiza nini na wakati kweli ametoa na wala hakujumlisha?kuweni wapole kidogo au rejeeni part two ya wimbo NDIO MZEE wa profesa Jay ndio mtaupata ukweli!!
 
Back
Top Bottom