Ahadi ya ajira milioni moja changa la macho?

Eric Ongara

Senior Member
Sep 19, 2006
165
8
Wakati wa Kampeni Jakaya,ili kuteka vijana,ambao ndio wapiga kura wengi alitoa ahadi chongo juu ya ajira.Akaahidi ajira milioni moja!

Kwanza ahadi yenyewe haieleweki! Ukifuatilia kwa mujibu wa takimu,kila mwaka kwa wastani vijana kati ya 650,000 mpaka 750,000 wamaingia katika soko la ajira.Sasa tukichanganua ahadi ya Jakaya,kila mwaka ndani ya miaka mitano atatengeneza ajira kwa wastani wa 250,000 kila mwaka.Maana yake ni kwamba,kila mwaka vijana laki tano watakuwa hawana ajira!

Halafu anasema ajira anazo tengeneza zitatokana na mpango wa manedeleo ya shule za sekondari na ule wa shule ya msingi pamoja na sekta ya afya,huu mtazamo si sawa kwani sasa serekali ni mtengeneza mazingira na si muajiri mkuu,mikakati ilipaswa kuegemea zaidi kwenye sekta binafsi!

Bajeti ya mwaka huu,wameshindwa kusema watatengeneza ajira kwa kiasi gani na kwa njia zipi! Bora angeahidi kutaja asilimia la ongezeko la ajira na sio kutaja takwimu ambazo hazina mantiki yoyote! Anachemka!

Nasema,sioni muelekeo wala uelewa wa Jakaya na Baraza lake la mawaziri katika kutekeleza azma hii!
 
Ndugu yangu Eric, hata wakenya wantudharau,

Kenya: Kikwete Criticised for Poking His Nose Into Kenyan Politics

The East African Standard (Nairobi)

September 24, 2006

Posted to the web September 25, 2006
Ernest Mpinganjira
Nairobi
Tanzania's President Jakaya Kikwete's reported talks with US President George Bush over "political instability" in Kenya have generated debate at home.
Opposition leaders say the President had no business poking his nose in Kenyan politics when Zanzibar is on the brink of chaos and Tanzania staring economic crunch.
The comments came days before the expiry of the ultimatum the Civic United Front (CUF) had given President Kikwete to address the differences between Zanzibar and the mainland, over political autonomy. Failing to act, CUF leaders warned, there would be an uprising in Zanzibar "similar to the recent Hezbollah war with Israel."
At the end of CUF national congress on Thursday evening party chairman, Prof Ibrahim Lipumba, was forthright in his indictment of the President.
"He is a globe-trotter who is out of touch with reality. We appeal to President Kikwete to reduce his foreign trips and concentrate on solving domestic problems," Lipumba said.
There should be no debate over the demand for the formation of a government of national unity to appease the opposition over electoral fraud, he said.
The warning was a pointer to the increasingly volatile atmosphere in Zanzibar, where the President and the ruling Chama Cha Mapinduzi are accused of rigging polls.
CUF leaders in Zanzibar, led by Seif Shariff Hamad, have refused to recognise the CCM Government. The stance has created political instability, which Kikwete is accused of being reluctant to solve.
The stand off in Zanzibar is threatening to explode into full-scale civil strife and has been a cause of concern to Britain and United States. Both fear the situation could land Zanzibar into the hands of Middle East Islamic jihadists and al Qaeda terrorists. Intelligence reports show the groups have a foothold there.
Lipumba says the nation is on the verge of economic crunch because of one crisis after another. Due to power shortages there has been a slump in the manufacturing sector, leading to massive lay offs. As a result the country is preparing for the lowest gross domestic growth in 10 years.
"It isn't ironical that President Kikwete is abroad marketing a country without electricity? Which investor would want to put his money in a country with poor infrastructure?" he says.
The remarks by Lipumba, a former economics lecturer and World Bank and International Monetary Fund (IMF) adviser, reflect the growing pessimism.
The impact of the economic crisis is perceived through indicators such as the foreign bank reserves, which the Central Bank of Tanzania (CBT) announced had dropped from $2.8 billion in January to $2.1 billion. CBT governor David Balali says the amount is just enough for imports for five months.
With hydropower production having dropped to less than 80 megawatts, Tanzania is expected to import more fuel and foodstuff in the next six months.
The subdued economy has disillusioned majority, including, President Kikwete's ardent supporters. They criticised the President for attending a Real Madrid Football Club training session at Barnabeau Stadium in Madrid, Spain, the same day the country sank deeper into the crisis.
There is no time since his election that support for the President been so low. The biting power cuts have sent a message that the Government is extravagant and insensitive to the citizens.
The public are accusing the President and his Prime Minister Edward Lowassa of extravagance, citing more than 15 trips the President has made abroad since his election. Lowassa has done about half that.
President Kibaki and President Museveni have since the power rationing intensified received praise from opposition parties and the public for making less than 10 trips abroad in the past four years compared with Kikwete's 16 in eight months in more than 20 countries. Their entourages are equally lean, compared to that of the Tanzanian leaders, who sometimes at times are accompanied by their families. Lowassa, for instance, travelled with his teenage son to Thailand on official duty -where he allegedly asked the ousted Thai Government to send rainmakers to Tanzania to solve the power crisis.
The perception of extravagance was fuelled further when Minister for Infrastructure Development Basil Mramba told journalists recently that the Government had drawn a budget for three presidential jets, each costing $26 million.
The current reconditioned jet breaks down frequently. It cost the Government $45 million, although Canadian aircraft manufacturer, Lombardi, had offered to sell the Government a new jet at $18 million. There have been calls for the Government to sell the jet and invest the proceeds in power generation.
A Kiswahili daily, Tanzania Daima, reported last week that the jet has been given to First Lady, Salma Kikwete, for her private trips outside the country.
The First Lady travels in police and military helicopters within the country.
On Wednesday, Lipumba summed up the current Government as "headed by wasanii (con artists)." He also indicted Kikwete and Lowassa for abandoning Zanzibar.
 
Muda si mrefu waliokuwa wakimwita JK kuwa ni chagua la Mungu wataficha nyuso zao.Hivi kwanini yule anayejiita Tafiti Then Jadili huwa hachangii mada kama hizi?
 
Mlalahoi,
Wameshaanza kuficha nyuso zao. Wamemshutukia kwa swala la Mufti.
 
JK alipokea nchi ambayo uchumi wake ulikuwa unaongezeka kwa kasi ya 7% kwa mwaka. Mwaka mmoja tu baadaye hiyo kasi ya kukua kwa uchumi imedorora na kufika chini ya 5%.

JK alipokea uchumi wenye mfumuko mdogo wa bei wa 4.5% kwa mwaka. Mwaka mmoja tu baadaye, kasi ya kukua kwa mfumuko wa bei inakaribia 10%. Na kwa staili ya JK, hiyo kasi itafika 20 - 30% kabla hajamaliza miaka 5 ya Urais.

JK alipokea uchumi uliokuwa na fedha za kigeni za kutosha kuagiza bidhaa toka nje za kutosha miezi 9. Mwaka mmoja tu baadaye ametumia hizo fedha kwa kasi kiasi kwamba sasa uwezo wetu ni wa kulipia bidhaa za kutosha miezi 5 tu. Kwa hali hii, ni wazi kwamba kabla JK hajamaliza miaka 5 ya Urais, tutakuwa kama tulivyokuwa 1985. Wakati huo, ilibidi taifa likopeshwe $8 mil ili kuweza kukomboa bidhaa ya mafuta iliyokwa bandarini.

JK amekuta serikali iliyokuwa na surplus kwenye bajeti zake. Atatufikisha kwenye deficits kubwa baada ya mwaka mmoja tu wa utawala wake. Hizo deficits zitakuwepo kipindi chake chote.

Taifa sasa lina shida kubwa ya maji na umeme. Baraza la mawaziri ni la marafiki wa Rais, sio la watu wenye uwezo wa kuongoza vizuri. Ukubwa wa serikali unatisha, na umetokana tu na njama za JK za kuwapa kazi kubwa kubwa marafiki zake.

Kwa kiasi fulani, Watanzania wanastahili hiki walichopata. Walikuwa rahisi mno kudanganywa na kurubuniwa na JK.

Augustine Moshi
 
Mwalimu,

Wadanganyika walio wengi ni wavivu wa kufikiri na mbilikimo wa mawazo.
JK anatumia advantage hiyo. Walioenda shule wengi wameshashtuka kuwa nchi inatawaliwa kimaskani. Muulize rafiki yako yeyeote nyumbani utaambiwa kuwa TULIKOSEA. Nchi ina marais wawili, mmoja anakaa nchini mmoja anatumbua maisha nje ya nchi. makala niliyoleta hapo juu inajieleza.
Wajanja tumeshashtuka!

FD

FD
 
Fikira duni, sasa ni dhahiri tunajiandaa na machungu makubwa. Mpaka sasa JK ameshindwa kufafanua vipaumbele vyake.Tuna kiongozi ambae hana muelekeo.Anafanya siasa za show game,kutembelea magereza,hospitali na kadhalika. Lakini masuala ya msingi hayatatui.

Vyombo vya habari navyo viko taabani kazi yao ni kusifia tu.Jambo moja linalonishangaza,raisi akikosea wanasema kashauriwa vibaya! Huwa sielewi dhana hii,kwani wakati wanamshauri walimshikia bunduki akubali ushauri huo? mbona kwenye kusifiwa huwa hawawakumbuki washauri kwamba walimshauri raisi vizuri?.
 
Ngoja nikwambie ndugu yangu. Watu wengi wanaolelewa hawapigi kura, wapiga kura ndio wale wale wanaonunua magazeti ya kasheshe.

Kwa TZ tutaendelea kudorora mpaka tuwape watu elimu ya kuweza kutambua mambo. Kitu kama hicho viongozi hawataki, wanatenga asilimia 8 kwa ajili ya elimu.!!! Nani awape 28% au 26% kama nchi za jirani? tukisha waelimisha si ndio tutaondoka madarakani?

Ndio maana nasema mimi nalia na Elimu, wananchi hawana elimu. Uzalendo ni inborn haiitaji elimu hata ya chekechea!

FD
 
Hivi karibuni kila mkoa ulianza kwa kupewashillingi billioni moja kwa ajili ya huo mpango, sasa labda mtakumbuka huko nyuma niliuliza je mikoa inaweza kweli ku-create ajira?

kwa hiyo kwenye hilo yuko Mzee JK, yuko sambasamba nalo ila swali ni kwamba kama mikoa ina huo uwezo?
 
Mzee es,hapa ndipo tunasema serekali hii ni populists.Hivi kabla ya kutoa hizo bilioni moja walipatia ripoti za halmashauri na kujua matatizo yanayozungukia mikopo? kwa nini walikurupuka?

Si unafahamu tangu 2003 serekali ilianza utaratibu wa kutoa mikopo kwa vijana na wanawake kupitia halmashauri? ukweli ni kwamba mikopo ilikuwa inatolewa ni midogo na ilidhihirika pia shemu kubwa ya mikopo ilikuwa hairudishwi na halimashauri nyingi zilishindwa kutoa hiyo mikopo(rejea economic survey report ya 2005).

Lakini pia zipo stadi nyingi kupitia mashirika yanayo toa mikopo. Kuna tatizo la riba,kuna suala la uwezo,mafunzo,fursa zi biashara na menejimenti ya mikopo yenyewe. Ilipendekezwa kuwa na menejimenti ya kusimamia hii mikopo ihusike na mafunzo na tafiti pia kuwawezesha watanzania kutengeneza miradi ya biashara na kutambua fursa za kibiashara.

Je mikopo hii ilipotolewa mambo haya yamezingatiwa? Ni kiasi gani kimetengwa kwa ajili ya menejimenti ya kusimamia hii mikopo pamoja na kutoa ushauri? kuna mafunzo yoyote yatatolewa? je maeneo ya vipaumbele kwa ajili ya hii mikopo yamebainishwa? Hili zoezi litakuwa la kudumu? kama ndio, bila kuwa na menejimenti ya wataalamu ya mambo ya mikopo ya biashara?

Ndio hapo nahisi fedha hizi,ingawaje ni chache sana,bado zina mtazamo wa kutafuta sifa kuliko kuzalisha ajira yenyewe! Waseme basi projections zao wanategemea kutengeneza ajira ngapi kutokana na hizo mikopo!

Ipo hofu kuu,kutokana na uelewa mdogo wa wananchi kuna uwezekano wakizitumia vibaya hizi fedha,yani fedha hizi zitawaongeza umaskini zaidi,kwani watabaki na umaskini ule ule wa awali na madeni juu! Au kuna uwezekano hizo fedha zitaliwa na wajanja wachache au pengine ni njia ya kuwaambia asante watu wa "chama".

Mzee es,ukichanganua kwa umakini suala hili utajua kwamba hakuana umakini wowote wala nia ya dhati ya kuzalisha ajira hapa. Ole wake Tanzania.
 
Mzee es,hapa ndipo tunasema serekali hii ni populists.Hivi kabla ya kutoa hizo bilioni moja walipatia ripoti za halmashauri na kujua matatizo yanayozungukia mikopo? kwa nini walikurupuka?

Si unafahamu tangu 2003 serekali ilianza utaratibu wa kutoa mikopo kwa vijana na wanawake kupitia halmashauri? ukweli ni kwamba mikopo ilikuwa inatolewa ni midogo na ilidhihirika pia shemu kubwa ya mikopo ilikuwa hairudishwi na halimashauri nyingi zilishindwa kutoa hiyo mikopo(rejea economic survey report ya 2005).

Lakini pia zipo stadi nyingi kupitia mashirika yanayo toa mikopo. Kuna tatizo la riba,kuna suala la uwezo,mafunzo,fursa zi biashara na menejimenti ya mikopo yenyewe. Ilipendekezwa kuwa na menejimenti ya kusimamia hii mikopo ihusike na mafunzo na tafiti pia kuwawezesha watanzania kutengeneza miradi ya biashara na kutambua fursa za kibiashara.

Je mikopo hii ilipotolewa mambo haya yamezingatiwa? Ni kiasi gani kimetengwa kwa ajili ya menejimenti ya kusimamia hii mikopo pamoja na kutoa ushauri? kuna mafunzo yoyote yatatolewa? je maeneo ya vipaumbele kwa ajili ya hii mikopo yamebainishwa? Hili zoezi litakuwa la kudumu? kama ndio, bila kuwa na menejimenti ya wataalamu ya mambo ya mikopo ya biashara?

Ndio hapo nahisi fedha hizi,ingawaje ni chache sana,bado zina mtazamo wa kutafuta sifa kuliko kuzalisha ajira yenyewe! Waseme basi projections zao wanategemea kutengeneza ajira ngapi kutokana na hizo mikopo!

Ipo hofu kuu,kutokana na uelewa mdogo wa wananchi kuna uwezekano wakizitumia vibaya hizi fedha,yani fedha hizi zitawaongeza umaskini zaidi,kwani watabaki na umaskini ule ule wa awali na madeni juu! Au kuna uwezekano hizo fedha zitaliwa na wajanja wachache au pengine ni njia ya kuwaambia asante watu wa "chama".

Mzee es,ukichanganua kwa umakini suala hili utajua kwamba hakuana umakini wowote wala nia ya dhati ya kuzalisha ajira hapa. Ole wake Tanzania.
 
Mzee Eric,

Ni kweli you have a strong point, lakini ninataka uwe rest assured kuwa waliozipokea hela hizo watamueleza JK, wamezifanyia nini?

kwa hiyo kuna hatari zikaishia kukaa benki bila kuguswa, maana sio siri kuwa hakutakuwa na creativity za ajira,

kula hizo pesa haiwezekani kabisaaaa!, baada ya kuiangalia kwa makini srikali mpya for the last nine months, sasa ninaamini kama kuna kiongozi anayekula mpaka leo, basi kuna wachache ambao wameruhusiwa kwa ajili ya sababu maalum, ama sivyo hali mtu, yaani mabay hata kuna wanaojuta kupewa uwaziri!
 
Ujinga ni adui yetu mkubwa kuliko wote. Njia ya kumpiga vita ni kuipa Elimu kipaumbele. Nasikia kuna watoto wamerudi nyumbani kutokana na kukosa fedha za mikopo ya Elimu, na wengine kukosa ada. Sasa mtoto kama huyo ndiye anatarajiwa akakope toka kwenye fedha zilizopelekwa mikoani!

A well educated population would be our most important resource. JK hatambui hivyo, ndio maana ameipunja sana Elimu fedha. Kama tungetumia 25% ya bajeti yetu kwenye Elimu (achilia mbali 27% ya Kenya) basi mwaka huu wa fedha tungetenga shilingi 1,212,647,000,000 (trilioni 1, bilioni 212, na milioni 647) kwa ajili ya wizara zetu mbili za Elimu. Hii ni mara tatu ya fedha ambazo tumetenga. Kwa hali ya fedha kama hizi (ambazo ndiyo haki ya Elimu), kila shule, chuo na idara za wizara husika ingeweza kupata fedha mara 3 ya itakavyopata sasa. Wanafunzi wote wangepata mikopo ya kutosha, tungekuwa na uwezo wa kuajiri watendaji zaidi mashuleni, na shule zingekuwa na vyoo na vifaa kama vitabu vya kuridhisha.

Ukitaka uwe na wananchi wenye uwezo wa kupokea na kutumia vizuri mikopo na kuirudisha, basi kazania Elimu. Usiruke Elimu ukawatupia wananchi fedha. Hazitazaa.

Kijana anaachishwa chuo kwa kukosa mkopo wa Elimu, na badala yake apewe mkopo mkoani wa kujiajiri?

Augustine Moshi
 
Mzee Moshi,
Umeuliza swali la msingi sana hapo juu: "Kijana anaachishwa chuo kwa kukosa mkopo wa Elimu, na badala yake apewe mkopo mkoani wa kujiajiri?"
Natamani kusikia "wenyewe" wangetoa jibu gani!

Yote kwa yote, nadhani tuna tatizo la kukosa dira, ubunifu na kutoona mbali. Ni kutojua namna gani mipango ya taifa inapaswa kuwa inasaidiana au inaungana (backward and forward linkages). Watunga sera na mipango wetu hawafikirii kwa upana na marefu, matokeo yake kila kitu kinakuwa kama kuzima moto. Mifano kuthibitisha hili ni tele: kuanzia Mpango wa Elimu ya Msingi (MEM), Mpango wa Elimu ya Sekondari (MES) na hiyo elimu ya juu na bodi yake ya mikopo. Matatizo ya umeme nayo kwa kiasi kikubwa ni kutoona mbali; sasa leo wanapambana na wakulima, kisa wanamaliza maji ya kuzalisha umeme! Ni serikali hiyo hiyo iliyobuni miradi ya kilimo cha umwagiliaji katika maeneo mbalimbali bila kuzingatia kuwa hatimaye kiasi cha maji kiingiacho kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme kitaathirika. Ama kweli tuna kazi!
 
Nakubaliana nanyi,Moshi na Mwanagenzi, Serekali yetu haina vipaumbele

Naona Mzee Es una uhakika sana na uaminifu wa viongozi wetu,kama itakuwa hivyo ni jambo jema,tusubiri tuone mambo yatakavyokwenda. Lakini kwenye kukurupuka nahisi ndio style ya serekali yetu,maana si kwenye mikopo pekee yake,si umesikia habari kwamba JK alizungumza na Barrick(wale wenye migodi) juu ya ulipaji wa kodi,wakakubaliana walipe bilioni tisa kwa kila mwaka(ni kidogo sana hizi) bila kujua wanazalisha kiasi gani kwa mwaka!

Suali la kujiuliza kwanini JK asingesubiri kamati iliyoundwa ya kufanya mapitio ya mikataba ya madini ndio azungumze nao?

Kwa hiyo kuna kukurupa sana hapa ndugu! Maana badala ya kuweka hizi fedha zikakaa tu benki,kwa kuwa hatuna miundo inayoelewaka kwa sasa kwa nini fedha hizi zisingepelekwa kwenye bodi ya mikopo ya wanafunzi,hawa mahitaji yao ni dhahiri na ya haraka na muundo upo,tayari ulishwawekwa? Maana ilionekana kama kuna haraka vile ya hata kwenda kinyume na bunge! Bunge liliidhinisha milioni miatano JK akatangaza bilioni moja!! Tuna kazi hasa!
 
Ndugu zangu hapa kuna kiiini macho na kuhusu suala la mikataba ya madini na alichokifanya JK,

ukweli ambao wananchi hawajaambiwa ni kwamba, serikali inaposaini mikataba ya madini na mingineyo mingi, huwa inasainiwa kwa muda maalumu, yaani kwa mfano huu mkatba wa madini ulikuwa ni wa miaka mitano, na serikali inai-review mikataba hiyo kila baada ya miaaka mitano, au inakuwa ime-expire,

kwa hiyo JK alichofanya na ambacho wananchi hawajaambiwa ni kwamba wakati wa mikataba hiyo ku-expire ulikuwa umefika, sasa badala ya kuwaachia wataalamu wa madini na serikali kui-review mikataba hiyo kitaalamu, yeye JK akaamua kuingilia kati, na kuweka mikataba ambayo ni great kwenye gazeti, lakini ukweli ni ule ule kuwa bado tunaliwa,

kwa hiyo ndugu zangu kuweni waangalifu na any great news ya hii awamu ya nne, maan siku zote huwa ni mkenge, kama huu wa madini, halafu magazeti ya payroll yakasema hatimaye JK afanya kweli, NONESENSE and IDIOTIC!
 
Mzee ES,

Kwa maoni yangu, una uchungu na nchi yako, na sio mtu wa kusifu tu au kutukana bila sababu. Naomba nikupongeze kwa msimamo thabiti. Hiyo mikataba umeitia machoni? Sidhani kama mtu atakubali kweli mkataba wa madini unaokwisha baada ya miaka mitano. Hata hii ya kwetu ya kuyachukua madini bure (3% ni bure) bado inahitaji iwe ya angalau miaka 10-20.

Kiasi cha fedha kinachotokana na mauzo ya madini yetu ni kikubwa sana. Hapa chni nimeweka dondoo kuonyesha kiasi kilichopatikana mwaka jana. Kama haya madini yangekuwa yetu, basi tungekuwa tunapata angalau 50% ya fedha zinazopatikana.

Nielewavyo ni kwamba tuna URANIUM vile vile. Hilo nadhani halizungumzwi sana kwani ni la hatari. Iran inabidi ipate mahali itakapouziwa Uranium, siku za karibuni. Woga wa Bush na wengine ni kwamba huenda Tanzania ikawa ndio mahali penyewe.

Kuna wakati Simba wa Vita (Mzee Kawawa) alisema "Watanzania mnao uchumi lakini mmeukalia". Sijui kwanni alijitoa, asiseme "tunao" badala ya "mnao". Hata hivyo, huu uchumi hatuukalii tena, tumeutoa bure. Tutakalia nini sasa?

Augustine Moshi
=========================================


Exports of gold have generated around 93 percent of Tanzania's foreign currency earnings from the mineral sector last year, according to the latest statistics of the central bank.

The Bank of Tanzania figures showed that last year's exports of gold had fetched the country 641.7 million U.S. dollars while exports of gemstones of tanzanite, rubies, sapphires and emeralds got the country 31.4 million dollars. Exports of diamonds netted Tanzania 19.7 million dollars.

"During 2005, non-traditional exports went up by 13.3 percent to 1,176.3 million dollars," said the bank's monthly economic review for January.
"Gold led the list by accounting for over 50 percent of the total non-traditional exports due to improved prices in the world market and increase in production," the review added.

All told, exports of minerals accounted for 58.89 percent of last year's Tanzanian foreign currency earnings. The remainder came from exports of manufactured goods, fish and fish products, horticultural products, vegetables, oil seeds, cereals, cocoa, raw hides and skins, and woods.
Exports of gold earned Tanzania 629.4 million dollars in foreign exchange in 2004.
 
Mzee Moshi,

Heshima yako mzee, unajua majuzi nilikuwa na "Kigogo" mmoja wa CCM, alikuwa na print-out nyingi za hii forum, yaani michango yako juu ya Elimu ilimuuua kweli, na halafu kuna mchango wako mmoja unaongelea inflation kwa namba, yaani I wish ungemuona huyo Mzee alivyotakasika roho, na kusema kuwa ".......hawa vijana ni hatari hawa, umeiona hii......"

Hii mikataba asikudanganye mtu hiyo ni nyeti kubwa sana kwa serikali, miaka mitano nimeweka kama figurative figure, lakini ninajua as a Fact kwamba kilichotokea majuzi kayi ya JK na mikataba ya madini, ilikuwa kama nilivyosema kuwa wakati wa ku-review ulikuwa umefika, na sio kama media uchwara zilivyosema kuwa JK kaingilia kati si ukweli!
 
Mzee Es asante kwa kutupa habari mara kwa mara juu ya impact ya michango yetu.Sasa umesema kigogo unajua Serikali ina vigogo wengi hata Katibu kata .Tueleze nani hasa alikuwa ili tujue kwamba ujumbe wetu umefika.Je alikuwa ana print kwa uelewa wako na maongezi yenu akafanyie nini hizo info? Ulivyo msoma umesema alikuwa kakasirika .Je alikasirika kwamba ana print zile info ama nyeti za alizo kuwa ana print zilikuwa kinyume na alivyo tegemea kwamb watu wanajua ?

Je baada ya kusoma kwamba sasa Mzee Es kasema kwamba JK katulaghai juu ya mikataba na hasa mkataba wa majuzi alikuwa na comments gani ? Tueleze tujue namna ya kuweka habari hapa maana nia ni kuokoa Nchi ni ngumu lakini tutawapa ujumbe wakatae kwa kiburi chao tu .
 
Mzee Es,Fafanua hapo imekaa vizuri hiyo kama mijadala hii inawafikia viongozi ili ipate kutimia:
"Tuliamba hamkucheza tulilia na hamkuomboleza kwa maana mioyo yenu imefanywa kuwa migumu".
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom