Ahadi ya ajira milioni moja changa la macho?

Mwanakijiji huyu kasema hajasoma uchumi kwa hiyo nadhani anyamaze kimya wana uchumi waseme.
Huna hoja huna haki ya kuzungumza!
Asilete hapa upuuzi wa sisi m kutudanganya hata great thinkers!
 
According to the recent figures in UK mfano unemployment ni about 7.9% between Aug-Dec 2009. US unemployment rate stands at 10%.

Inawezekana zikawepo ajira milioni 4 despite hali mbaya ya uchumi (katika ndoto lakini). Tanzania impact ya recession haipo katika banking sectors, or other financial sectors we are facing a real economic recession. Kwasababu ukitazama uchumi wa Tanzania 40 of budget depends on donor funding. Sasa kama wazungu wanasafa utakuta watapledge but pesa inaweza isifike kwasababu wao wenyewe hawana hiyo pesa.

Tuje katika impact ya recession Tanzania. Kiufupi kuna sekta zitakazoumia mfano Tourism ambapo tunategemea zaidi overseas travellers. sasa hapa utakuta sekta ya utalii inasafa kwa kiasi kikubwa sana. Tunaona sasa hivi zanzibar inavyoumia kwasababu inategemea kwa kiasi kikubwa katika utalii.

Tuje viwandani. Tanzania tunategemea tuvutie FDI (Foreign direct investment). Now these multinational firms expansion programmes depends largely with their overall performance. At the moment most companies are undergoing cost reduction (kupunguza gharama), hivyo basi utakuta na sitoshangaa nikaona FDI kwa Tanzania zikapungua 2009-2008. Hivyo basi kama tunategemea ajira katika makampuni ya kimataifa tujiuliza mara mbili zitakuwapo kweli au ndio tunapeana moyo (hope).

Tukija katika mining ndio mkombozi wetu, price of gold wakati tunaelekea kumaliza mwaka iligonga $1108 per ounce saa mbili ya asubuhi 31/12/2009. sasa tungelikuwa na misingi mizuri ya kusimamia madini hapa ndipo ajira milioni 4 zingeliweza kutokea kwani tukiuza madini na mapato yakapatikana kinadharia tungeliweza kuongeza pato la nchi tukajenga mabarabara, hospitali, majengo hivyo basi kutoa kazi kwa vijana. bei ya silver nayo iko juu pia na madini mengineyo but!!! Tatizo la tanzania mikataba mibovu, ufisadi , njia mbovu za kukusanya mapato zinachangia kuona athari zozote katika uchumi.

Pengine kimtazamo wangu inawezekana serikali imetoa ajira milioni 4 kwa kupanua ufanisi wa serikali (which is usanii maana inaliongezea mzigo taifa) kufungua ofisi vijijini ukawapa ajira vijana. But hili ni mbaya kwasababu inaliongezea mzigo taifa kwa kuongeza government expenditure sasa inawezekana ajira ndio zimetokea huko.

venginevyo ninavyoangaza sioni mahali ajira milioni 4 zimetoka labda wengine wachangie.

I stand to be corrected!!!!
 
mwanakijiji huyu kasema hajasoma uchumi kwa hiyo nadhani anyamaze kimya wana uchumi waseme.
huna hoja huna haki ya kuzungumza!
asilete hapa upuuzi wa sisi m kutudanganya hata great thinkers!


wewe huna uwezo kuita nilichoongea nupuuzi....
Wewe ndo mpuuzi kwa sababu unajiita great thinker
while hata a b c d ya nilichozungumza hujaelewa...

Swali ni hili,,,,wewe umesoma ripoti ya mkurabita???????

Kama hujasoma ripoti ya mkurabita na hujui mkurabita ni nini
basi bora unyamaze.............

Huwezi zungumza uchumi bila statistic sahihi,period.
 
Huwezi zungumza uchumi bila statistic sahihi,period.
vile you can never claim to increase job opportunities in private sector during a recession period.

Hivyo kuna uongo somewhere unless kama mdondoaji alivyosema serikali imetengeneza hizo nafasi zenyewe kama stimulus package ya obama. Something which makes us raise the eyebrows tungeona ushahidi fulani.
 
vile you can never claim to increase job opportunities in private sector during a recession period.

Hivyo kuna uongo somewhere unless kama mdondoaji alivyosema serikali imetengeneza hizo nafasi zenyewe kama stimulus package ya obama. Something which makes us raise the eyebrows tungeona ushahidi fulani.

kabisa kabisa..
Ndo maana nimesema one million new jobs si big
deal....umenipata????

Kama uchumi unge endeshwa vizuri sana
wangeweza kutengeneza hata five milion new jobs...

But kwa kuwa wmeshindwa na statistic sahihi
hakuna,,,,,,hata wakisema wametengeneza
ajira milioni moja tusione ajabu....

Sio miujiza kabisa.
 
Katika hotuba yake ya kuuaga mwaka 2009 na kuukaribisha 2010 Rais Kikwete alisema hivi:



Wakati huo huu tumeambiwa kuwa serikali ya JK imefanikiwa kuvuka lengo lake la ajira milioni moja na kuwa wametengeneza ajira mpya zaidi ya milioni moja ndani ya miaka minne.

Naomba wachumi mnisaidie ni katika mazingira gani nchi inayokabiliwa na athari za recession inatengeneza ajira zaidi ya asilimia 100 ya makadirio yake na wakati huo huo kudai kuwa ina hali mbaya ya kiuchumi?

It is very funny, maana hata marekani yenye uchumi mkubwa kuliko nchi zote, yenye watu zaidi ya milion 300 haijaweza kufanya hayo maajabu. Nchi zilizoendelea ajira 1000 huwa hata waziri husika anatoa tamko, kwa maana ni mafinikio yasiyo kidogo.

Turudi bongo, ni kwamba baada tu ya JK kutangaza hiyo ahadi wizara ya Kapuya ikaingia kazini, Kila mwajiri alilazimika kusubmitt no ya watu alioajiri kwa mwezi regardless ni permanent, kwamkataba au kibarua. Hawa jamaa walikuwa happy kuona tu namba inaongezeka na hivyo kumfurahisha bosi. Nakumbuka one time nikiwa bongo in one of the consulting firms tulipewa kazi kwenye one of the mines. Tukaajiri watu 6 for like 6 weeks, baadae nillitwa HR dept kwa ajili ya details za hao watu. Nilipoulizwa why nikaambiwa zinatakiwa wizara ya kazi ili kujua ni ajira ngapi zimezalishwa. I told them but this is temporary wakasema hata kama ni siku moja, data need to be submitted as per maagizo ya wizara.

ISSUES:

1. Je ni ajira ngapi zimepotea katika utaratibu huo huo unaotumiwa na wizara ya kazi in these four years?

2. Nna amini kabisa hata JK haamini hizi takwimu pamoja na kwamba ni ahadi aliyotoa yeye. I am sure akibanwa kwenye 18 atairuka kama alivyoiruka ilani ya uchaguzi ya CCM.

3. Je ni indicators zipi zinasupport kuzalishwa kwa hizo ajira? It is funny kuona kwamba NSSF ambao ndiyo mfuko mkubwa wa social security na hasa kwa private firms, idadi ya member wake ni kama 500,000 tu an increase of about 60,000 kwa miaka minne. Sasa hawa waajiriwa wapya wako mifuko ipi ukizingatia mfuko kama LAPF member hawafiki hata laki mbili.

4. Hivi Kapuya na watu wake wanafahamu milioni moja maana yake ni nini wasije wakawa wanachanganya na 1000 kama ndugu zetu wa nyumba ya Gavana. Anyways kwa ufafanuzi zaidi, watu milioni ni sawa na abiria kutosha vipanya 50,000 au nchi nzima ya Botswana, au idadi ya wananchi wote mkoa wa Rukwa au Ruvuma. Ukikusanya hao waajiriwa wapya ni wengi kuliko watu wote mkoani Lindi.

5. Akina Kapuya wanweza kumegamega hizo takwimu zao at least tukajua kila wilaya zimezalishwa ajira ngapi?

6. Kapuya mwenyewe kama waziri wa kazi and in this sense the smartest in the world amezalisha ajira ngapi jimboni kwake?
 
kabisa kabisa..
Ndo maana nimesema one million new jobs si big
deal....umenipata????

Kama uchumi unge endeshwa vizuri sana
wangeweza kutengeneza hata five milion new jobs...

But kwa kuwa wmeshindwa na statistic sahihi
hakuna,,,,,,hata wakisema wametengeneza
ajira milioni moja tusione ajabu....

Sio miujiza kabisa.
kwa hawa wanavyopenda sifa wangesema kama wametengeneza hizo ajira na ni sehemu zipi.

Mbona amesema sehemu zote zilizo hasirika hili ionekane the fall was beyond their control bali due to international crisis.

Na kazungumzia humuhimu wa kuwasaidia wakulima wa pamba na stimulus package na tunaelewa asilimia kubwa ya wakulima wa pamba ni design ya akina rostam wanao zifilisi benki day in day out walioja kule bunda kama umenipata.

Huyu kweli angeacha kutafuta sifa za kusema hizo ajira kazitengeneza wapi na zime cost kiasi gani. Hapa hatuitaji takwimu kujua muongo zikija ni zita dhihirisha uongo wake.
 
Mkurugenzi Mwanakijiji:

Mimi sio msomi wa uchumi. Lakini idadi ya wanaofanyakazi inaweza kupimwa kwa kutumia payrolls za waajiri. Watu wanapolipwa mishahara rasmi ni lazima wailipe kodi serikali. Na ukihesabu waliolipa kodi kupitia mishahara yao, serikali inaweza kujua walipaji kodi kutokana na mishahara wameongezeka kiasi gani.

Kwa nchi kama Tanzania ajira ambayo mambo mengine yanaendeshwa katika sekta zisizo rasmi, njia kubwa moja ya kuongeza idadi ya wafanyakazi rasmi ni kuongeza matumizi ya serikali katika sekta za huduma ya jamii. Miongoni mwa sekta hizo ni elimu na Afya. Katika elimu, serikali iliongeza sekondari za kata, lakini sidhani kama ajira zilikuwa nyingi. Vilevile ujenzi wa mabarabara katika sehemu mbalimbali.

Na kama waliochukua mikopo ya Mabilioni ya JK, walifungua biashara zao na kujitegemea basi tunaweza kusema kuwa nafasi za kazi ziliongezwa kwa sababu huwezi kukopa na kurudisha bila kuwa-productive labda upate ucheze upatu wa DECI.

Kwa kumalizia tu, huwezi kupima ongezeko la nafasi za kazi wakati wanasiasa wanashindwa kuchukua majukumu ya kuanzisha masoko yalio rasmi.
 
Agenda iliyombele yetu ni uhusiano wa ongezeko la ajira zilizotajwa na Mhe. Rais kwenye hotuba yake ya juzi na hali mbaya ya uchumi (economic recession) ya nchi yetu na dunia kwa ujumla.

Kwanza kabisa nianze na kuelezea aina mbalimbali za ajira ambazo nchi inaweza kuona zinapatikana nchini kwa kipindi fulani kilichohusishwa katika utafiti au mjadala:
1. Ajira binafsi: Ajira hizi hutokea pale ambapo serikali hutengeneza mazingira mazuri ndani ya nchi kwa watu wake hasa wajasliamali (Entrepreneurs) hujiajiri wenyewe. Hili linawezekana pale ambapo kwa mfano mitaji na masoko ya bidhaa fulani itakuwa rahisi kupatikana kama matunda ya kazi ya Serikali husika kuweka miundombinu mizuri kwa uchumi wake kufanya kazi kwa ufanisi na kujitoshereza (kuwepo kwa taasisi za kifedha na miundombinu mingine muhimu kwa watu binafsi kuwekeza. Lingine katika hilo, ni kuwawezesha wananchi walio wengi kuwa na kipato cha juu kiasi cha kuwa na uwezo wa kununua bidhaa ndani ya nchi yao zizalishwazo na wajasiliamali (entrepreneurs).
2. Ajira za Sekta binafsi: Hapa ni pale mashirika ya kitaifa na kimataifa ndani na nje ya nchi yanapoweza kutoa ajira wa jamii yetu (Tanzania). Mfano ni pale ambapo mashirika kama TIGO, VodaCom, TBL, n.k kupitia ama FDI (Foreign Direct Investment) au mitaji wa wananchi wetu, huweza kuwekeza kwenye viwanda na mashirika ya kutoa huduma. Haya mashirika huweza kuajiri watanzania kwa asilimia kubwa (kwa mjibu wa Sera ya Ajira ya nchi yetu). Lakini kutokana na hali ya uchumi wa dunia kuwa mbaya, tuliona mashirika ya kimataifa kama mdau hapo juu alivyosema hujaribu kujiendesha kwa kupunguza gharama. Ikiwezekana kupunguza hata waajiriwa wake (employees lay-off). Hivyo kuna uwezekano mkubwa tu kwamba ajira zilipungua kwa kigezo hicho kwenye makampuni yenye mitaji ya FDI;

Kipengele kingine ambacho kinaweza kuwa ni kikwazo kwa ajira nchini Tanzania hasa hizi za FDI ni kipato kidogo kwa wananchi wetu, maana soko sasa linakuwa funyu kuweza kununua bidhaa zizalishwazo na makampuni hayo yaliyowekeza kwa mfumo wa FDI (market seeking FDI). Tanzania tunategemea zaidi FDI zinazokuja kutafuta maeneo na mali ghafi kama vile kwenye madini, vinginevyo hatujajenga mazingira ya kuwavutia wawekezaji kutoka nje waje kuwekeza nchini kwetu kwa kutegemea kuuza ndani ya nchi. Hivyo, Serikali ifanye bidii kuongeza kipato cha watu wake ndipo ajira nyingi zitapatikanaj;

3. Ajira za Sekta za Kiserikali: Hapa ni ajira ambazo Serikali yenyewe huajiri watanzania kulingana na hitaji, ili kuweza kutekeleza kwa urahisi majukumu yake ya kukuza uchumi. Hapa naomba niandike zaidi maana ndipo hapo tulipo na matatizo makubwa yanayotufanya tubaki nyuma siku hadi siku katika kukuza uchumi wetu. Serikali ya Tanzania, huajiri watumishi wapya bila kufanya uchambuzi wowote wa kisayansi kwamba tunahitaji waajiriwa wangapi na fani gani ili kuongeza tija (productivity) ya sekta mbalimbali nchini? Kwa sababu Rais aliahidi ajira kwa kipindi cha miaka minne watu wameajiriwa tu kwa agizo la Ikulu kwamba kila Halmashauri lazima iajiri watu kadhaa, Wizara lazima iajiri watu kadhaa ili hesabu ya idadi ya ajira milioni moja ifikiwe kabla ya uchaguzi wa 2010. Hii ni kweli na nina ushahidi juu ya hili. Ilitokea watumishi fulani ndani ya Serikali waliajiriwa 2009, walipowasili kuanza kazi Wakurugenzi wa Idara waliwakataa maana kwanza hawakuwa na taarifa za ajira hizo, Pili hawakuwa na hitaji la watu hao kuingia kwenye idara zao. Kwa sababu ni agizo la wakubwa, waajiriwa hao waliweza kupokelewa na kuwa waajiriwa wa kudumu wa Serikali.

Madhara ya hatua hiyo ni kuongeza matumizi kupita kiasi cha kawaida na ndiyo maana tunaona sasa mfumko wa bei ulipanda kwa kasi sana tangu JK alipoingia madarakani. Mfumko wa bei ulitoka namba 1 ya asilimia hadi kufikia namba 2 za asilimia kama (18%, 2009), sikumbuki vizuri.

Kiwango cha ukosefu wa ajira (unemployment) katika nchi yeyote ile hauwezi kuondolewa kwa 100%, bali hulinganishwa na kiwango cha mfumko wa bei nchini (nchi yeyote) kwamba kuna kiwango tu kinachoruhusiwa kupunguza ukosefu wa ajira (unemployment), katika kiwango fulani cha mfumko wa bei (inflation). Kama kiwango fulani kati ya viashiria hivyo vya uchumi itakiukwa kupita kiasi, basi hali ya uchumi nchini huharibika hata kama Serikali itafanya marekebisha kwa muda mrefu (Phillip Curve) inaeleza uhusiano huo kuwa huwa wa kutengana (inverse relationship between inflation and unemployment). Tanzania imeajiri kupita kiwango kinachotakiwa kiwe kwa kawaida hivyo kuurudisha nyuma mfumko wa bei (inflation) itakuwa kazi ya kutoa jasho. Tunatumia kingi zaidi kuzalisha kidogo ambacho haturudishi hata gharama za uzalishaji (mishahara). Tanzania hatuzalishi kwa kuongeza tija (there is no productivity among employees). Kila mwajiriwa anafanya kazi na kuzalisha chini ya hitaji ndani ya masaa aliyojihusisha kufanya kazi hiyo (kazi ndogo na yenye matokeo madogo inafanywa na watu wengi kuliko kawaida). Hivyo hatuwatumii wataalamu wetu ipasavyo, ndiyo maana utakuta mtumishi wa Serikali siku hizi anaweza kuwa na muda wa ziada kufanya mambo yake hata kama ni wakati wa masaa ya kazi ya mwajiri wake.

Hivyo, uchumi umeshuka maana uzalishaji umeshuka ukilinganisha na gharama za uzalishaji husika. Hivyo kipato cha Taifa kitaendelea kudumaa kwa sababu ya Sera mbovu zilizotawaliwa na msukumo wa Kisiasa zaidi kuliko kitaalamu.

Haya ni machache tu ambayo naweza kuelezea kuhusiana na thread ya M. M. Mwanakijiji.
 
Mkurugenzi Mwanakijiji:

Mimi sio msomi wa uchumi. Lakini idadi ya wanaofanyakazi inaweza kupimwa kwa kutumia payrolls za waajiri. Watu wanapolipwa mishahara rasmi ni lazima wailipe kodi serikali. Na ukihesabu waliolipa kodi kupitia mishahara yao, serikali inaweza kujua walipaji kodi kutokana na mishahara wameongezeka kiasi gani.

hapa ina maana tunazungumzia ajira rasmi; ina maana kuna ajira rasmi milioni moja na nusu na wote wanalipa kodi. je ni sekta gani rasmi imeingiza ajira hizi?



Na kama waliochukua mikopo ya Mabilioni ya JK, walifungua biashara zao na kujitegemea basi tunaweza kusema kuwa nafasi za kazi ziliongezwa kwa sababu huwezi kukopa na kurudisha bila kuwa-productive labda upate ucheze upatu wa DECI.

Hili ni mojawapo ya maswali ninayobaki nayo tunapoingia mwaka huu mpya; zile fedha za Kikwete zimepimwaje mafanikio yake, maana mara ya mwisho alipozizungumzia alielezea jinsi zilivyotolewa na vyombo gani vimetoa na kiasi gani; hakutuambia kiasi gani kimerudishwa (kama mkopo) na kiasi gani kimezalisha kama mtaji.

Kwa maneno mengine, kama mabilioni ya JK hayajarudisha mtaji ule wa bilioni 21 basi tumepata hasara. Ni kiasi gani cha asilimia ya fedha ile kikipatikana pamoja na mtaji tutasema tumepata faida? Yaani kama biliioni 21 zote zinarudisha faida ya shilingi milioni 100 tunaweza kusema zimefanikiwa sana, kidogo, au kwa kiasi?
 
i am not
an economist,
but i know it is possible.

mm mwanakijiji......uchumi wa tanzania
tatizo kubwa sana ni kukosekana kwa takwimu sahihi....

rejea mkurabita.....
kwa hiyo uchumi huu una uwezo wa kutengeneza
hata ajira milioni 5 kwa miaka minne.

kwa hiyo kwa jk kusema ametengeneza ajira milioni moja.
its not a big deal kabisa.

ni mara chache sana naafikiana na boss, lakini hapa nakubali.

kutokana na tatizo la takwimu, nawezekana hata hizo ajira zilizopatikaa sio realistic, na kuna uwezo wa kutengeneza ajira zaidi ya hizo 1m, mfano kama tutaanza usindika mazao na madini ghafi, pamoja na kutoa vipaumbele kwa wazawa katika ajira za sekta mbalimbali kama utalii nk. halafu kadiria ajira za mojakwamoja (direct) na zile zisizo za mojakwa moja (indirect).

jibu ni wazi kuwa ahadi ya ajira 1m ingeweza kutelkelezwa kikamilifu ndani ya miezi michache sana

pia kumbukeni kuwa uchumi unaodaiwa kudorora ni uchum wenye uhusiano wa moja kwa moja na sekta ya fedha za nje, ule wa sekta nyinginezo japo hautegemewi kubakia na kasi yake ya kawaida lakinni aghalab utachukua muda kushuka kwa hizo asilimia 2.5 kama mikakati madhubuti itafanyika, ikiwemo kruzuku sekta ya kilimo kwa leno la kuimarisha upatikanaji wa chakula ambacho ni moja ya vigezo vikubwa vinavyomua kiwango mfumuko wa bei
 
Hizi ajira milioni moja na nusu ziko katika sekta gani?

a. Haiwezekani kuwa ziko katika kilimo kwani kilimo kwa mujibu wa rais ndiyo kimeathirika zaidi na hali ya uchumi;

b. haziwezi kuwa katika viwanda, kwani hatuna viwanda ambavyo tunaweza kusema kuwa vimefaidika na kukua kwa haraka kiasi cha kuajiri watu milioni moja ndani ya miaka minne.
 
Mzee Mwanankijiji wala usihangaishe akili sana kujiuliza ni vipi nchi inayokabiriwa na economic recession iweze kutengeneza ajira zaidi ya 100%.

Kwa CCM hata kuongezeka kwa wasukuma mikokoteni ni ajira, achilia mbali mamalishe na wauza vocha za simu.

Tatizo la CCM ni kushindwa kujua tafsiri sahihi ya ajira ni nini?
 
Mzee Mwanankijiji wala usihangaishe akili sana kujiuliza ni vipi nchi inayokabiriwa na economic recession iweze kutengeneza ajira zaidi ya 100%.

Kwa CCM hata kuongezeka kwa wasukuma mikokoteni ni ajira, achilia mbali mamalishe na wauza vocha za simu.

Tatizo la CCM ni kushindwa kujua tafsiri sahihi ya ajira ni nini?

tupe wewe tafsiri sahihi ya ajira. itatusaidia sana
 
Hizi ajira milioni moja na nusu ziko katika sekta gani?

a. Haiwezekani kuwa ziko katika kilimo kwani kilimo kwa mujibu wa rais ndiyo kimeathirika zaidi na hali ya uchumi;

b. haziwezi kuwa katika viwanda, kwani hatuna viwanda ambavyo tunaweza kusema kuwa vimefaidika na kukua kwa haraka kiasi cha kuajiri watu milioni moja ndani ya miaka minne.

ziko katika sekta zote mkuu.

tatizo ni takwimu tu. usisahau kuna sekta isiyo rasmi. mathalani kama bilioni moja kila mkoa = bilioni 21 kwa tanzania bara. halafu jiulize kila kijana asiye na ajira akikopa 200,000 akajiajiri na halafu weka economic multiplier effect (ceteris puribus) utapata ajira ngapi?
 
Wakuu binafsi nimeamini...kuwa; misingi ya uchumi inavyopimwa na kutumiwa Tanzania ni tofauti kabisa na nchi zingine. Ukisiliza viongozi wetu utagundua kuwa Tanzania ina "new types of Economic theories" ambazo bado wanazuoni wa economics sehemu nyingine duniani bado hawajangamua..lol

Hapa hotuba ya JK inajadiliwa kwa misingi ya uchumi inayojulikana na kutumika sehemu zingine dunia. Tanzania ni tofauti; hebu angalie out of the box wenyewe mtaona.
 
Unapotoa data............ni muhimu ukazi-back up data zako............sasa hawa viongozi wanapokuja kutuelezea/kutupa terms in numbers....waweke hizo back-ups zao tuzione...........

Nyambala........yaani ulivyoeleza ulinifanya nicheke sana.....kwani hata mimi hilo jambo liliwahi kunikuta..........na kuna baadhi ya nephews wangu hivi sasa wana temporary ajira serikalini........nikawa nakumbuka yale yale ya HR........
 
Labda swali jingine ambalo tunaweza kuhoji (maana hoja yangu hapa naona haikuzama vizuri) ni hili:

Nchi inayokabiliwa na hali mbaya ya uchumi, yaani hali mbaya hadi kutenga shilingi trilioni moja na nusu hivi "kuunusuru" uchumi huo yaweza kuwa katika hali mbaya pasipo kupoteza ajira ya watu wengi .. Can a nation facing economic recession do so without causing unemployment?

a. Ukisema ndiyo, ina maana hali yetu ya kiuchumi siyo mbaya sana kama inavyodaiwa

b. Ukisema siyo, ina maana ajira za watu milioni moja na nusu wakati wa recession haiwezekani unless.. hali ya uchumi siyo mbaya sana!

c. If a and b are both true as some have implied then Tanzania (as Yebo Yebo put it) has found some new economic theories that need to be studied by the most developed countries so they could imitate us in what we are doing right..
 
Ajira milioni moja bongo....are you kidding me? Marekani kwenyewe sijawahi kusikia wakiongeza ajira milioni moja ndani ya miaka minne. Labda unambie ajira za kuuza nyanya magengeni na kubeba matenga.
 
Back
Top Bottom