AG awaonya TUCTA kujihusisha na siasa

Huo mshahara wa kinyemela wa wapi huo? Au ni allowance za muda, au ni rushwa ?

Nakubaliana na wewe Mfamaji, kama ni kweli wameongeza basi hawa CCM na viongozi wake wanatoa rushwa kwa wafanyakazi. TAKUKURU mko wapi, mnaangalia watu wanatoa rushwa wazi wazi, tafadhali Dr. Hosea na timu yako tunawaomba mchunguze hili kwani hii ni rushwa kwa sababu mkuu wa kaya alishakataa ongezeko hilo.Iweje sasa????:frusty:
 
Siasa ni mchezo wa rafu. Kama rafu si hobby yako usijaribu kujiingiza katika siasa.
 
Kama wameongeza kinyemela bila maandishi, pia wanaweza kupunguza kinyemela bila maandishi.

WAJINGA NDIYO WALIWAO.
 
tatizo TUCTA wanalilia hela za kunywea bia na kuhonga sio maisha magumu!Mgaya kila siku tupo nae kwenye kilaji,amchague Rais atakaye mjaza manoti.kwa ninavyojua mtu yoyote hata umpe hela kiasi gani haridhiki.au nani aseme anaridhika na kiasi gani cha fedha???hakuna!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kwani hamjuwi sifa zenu Siku zote hilo lakuengezewa mshahara si lina afadhali mara nyingi mpo hivyo mkishwa teremshiwa nyama choma na beer inakuwa ndio msharidhikana na kulainika kinachofuata mnafanya wanachokitaka wajaja wachache ,na zaidi hii mika ya karibuni mmekuwa mkiletewa waimbaji toka USA, katika mawazo yenu mamastasta wanakupendeni mkitoka hapo wengi mnaishia familia moja chumba kimoja viatu jiko ukumbi nK ni humo humo (aliye lala usimuamshe ukimuamsha utalala wewe)
 
Rais Kikwete ni msanii, pia inonekana ni mtu asiye makini na washauri wanaomzunguka wanaonekana kutokuwa makini siku zote, Kikwete anaonekana muda wote kutoyapitia yale yota ambayo amekuwa akiandaliwa tayari kuyatoa au kuuambia umma juu ya jambo fulani, aliweza kusainishwa mswada wa gharama za uchaguzi na hatimaye kuwa sheria kumbe ndani yake kachomekewa vipengele, leo hii anataka kula matapishi yake mwenyewe kwa kutaka kura za wafanyakazi? alisema kama ni kukosa azikose hayuko tayari kuongeza mshahara kwa shinikizo la Viongozi wa TUCTA, huku akirudia kutaja jina la mgaya kila baada ya dakika, leo anaongeza mshahara! sasa kama serikali haina hela hizo zimetoka wapi? Kikwete ninamjuwa ni mtu wa visasi, jaziba, hana maamuzi, na mtu wa kurukia mambo pasi kuchunguza, amekuwa akipotoshwa kila wakati na hii yote ni kutokana na tabia yake ya kutaka kila kitu aandaliwe na yeye kutokuwa na muda wa kuyapitia, mimi ni mwajiriwa wa serikali toka mwaka 2002 ktk Hospitali moja kubwa ya Taifa hapa nchini, mara ngapi tumekuwa tukipigwa danadana juu ya kuongezwa mshahra, leo anasema ataongeza mshahara? aache usanii huo,
 
Mimi nakubaliana na yule aliyesema kamaTUCTA ingetamka kuisapoti CCM, huyo AG angekuwa kimya -- angeufyata! Yote haya yanatokana na hofu kubwa iliyotanda ndani ya viongozi wa chama hicho kutokana na wimbi la kukubalika kwa Chadema. Kumbe hawa watu wanaweza ku-panic namna hii?

Na hilo unaweza kulithibitisha kwa namna Msekwa alivyobariki utoaji rushwa kwenye kura za maoni wakati kabla ya hapo walikuwa kifua mbele wakiahidi serikali yao kupambana na rushwa.
 
Mlioko serikalini tunaomba mthibitishe kama kweli salary slip zenu zina mabadiliko
 
Mie nimeiona hii habari nikawa na mshangao mkubwa kwanza naomba niulize ongezeko hilo limefanyika lini? Pili katika slip yangu nakatwa kodi kubwa ajabu utafikiri wanaugomvi na mie je ile kodi watapunguza? Tatu wanapoongeza mshahara hizo pesa wamezitoa wapi kwani mkuu wa nchi si amesema hana pesa? Kwasababu unapoongeza mshahara watu pasina na kuwa mpangilio wa maana unaweza kuta mshahara huo hauna significant effect katika maisha ya kila siku kwasababu mfumuko wa bei na gharama za maisha zitaongezeka. Lazima tukubaliane kwamba lazima kuweko na mfumo wa kuweza kuregulate mfumuko wa bei na gharama za maisha. Vilevile kuongeza mshahara pasina kupunguza posho kwa wakubwa ni hatari kwa serikali kwani inaongeza mzigo wa gharama kwa serikali na serikali yenyewe sijui itazitoa wapi pesa za kuendesha gharama hizo. Hivyo ni vema watuambie kwanza wamepunguza kodi ili wafanyakazi wawe na unafuu, wamekata posho wanazojilipa zisizokuwa na maana zaidi ya kulipa pesa. Ni pia watueleze ni kwa vp wanatuhakikishia hawatakuja kuongeza kodi baadae kama wakishinda uchaguzi. Mie bado nashaka na hizi taarifa mpaka nipate hayo majibu.
 
Kumbe JK ni bogus kweli kweli! Ameaambia wafanya kazi kuwa yuko tayari kuzikosa kura zao lkn hawezi kuongeza mishahara. Sasa, kama ni kweli kuwa mshahara umefikia 260k, hii ni rushwa inayokuja kwa sura fulani. TUCTA inatakiwa kum-endorse Dr Slaa na itangaze hivyo, CCM (Chama Cha Mafisadi) ijue hivyo na wannch na wafanyakazi kwa ujumla wajue hivyo. Tunahitaji aggresive mass media campaign kufikisha ujumbe huu kwa wananchi. Hebu niambieni CHADEMA inachangiwaje. CCM lazima kitoke. Sisi Wafanyakazi tunasema kwa JK: Ukitupa rushwa tutaila (hata TAKUKURU hatutawaambia) na kura hutapata.

CHADEMA Hoyeee!
 
NIMESHANGAZWA NA USIRI WA SERIKARI KTK ONGEZEKO LA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI HASWA KIPINDI HIKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU,YOTE HAYO NAJUA NI MATOKEO YA PRESHA YA UJUMBE UNAOSAMBAZWA KWA KASI WA WAFANYAKAZI KUINYIMA KURA CHAMA TAWALA KTK UCHAGUZI MKUU UJAO,KWANGU HIKI NI KIINI MACHO,RAI KWA WAFANYAKAZI NI KWAMBA TUSIDANGANGANYIKE:lying::embarrassed1:

lakini upandishaji wa mishahara haikuwa siri, kilichokuwa kinaleta shida ni kupandisha kufikia kiwango walichopanga TUCTA cha Tshs 315,000.
mbona waziri wa utumishi alisema mishahara itapanda ila hakutaja viwango kwa kusema vitaleta mfumuko wa bei? na hata hivyo Mh Raisi alitaja kuwa kima cha chini kimepanda kutoka 105,000 mpaka 135,000?
 
Tena nasikia kuwa walio ongezewa mishahara ni ma-askari tu! ndo serikali ina waogopa. Wengine mlie tu! Kwakuwa umeongezwa kisiri, baada ya uchaguzi mtegemee kurudi kwenye mshahara wa zamani. Hii ndiyo Serikali yenu ya tangu Uhuru ni usanii kwa kwenda mbele. Uongozi umewashinda lakini hamsalimu amri.
Aibu itawapata wengi kama hawaamini wasubiri 31/10/2010. 'MABADILIKO NI LAZIMA'

sio kweli kuna wengine si askari na wameongezewa, cheki na watu wa wizarani nk
 
Kama serikali wanaogopa kutangaza mishahara waliyoiongeza basi ni wapumbafu.
 
Unajua wangetangaza, wangetoa mwanya kwa wafanyakazi kujadili ongezeko walilolipata na hivyo kuweza kuendeleza msimamo wao. Maana hilo ongezeko halijafikia kiasi kile ambacho TUCTA walikiomba kutoka serikalini. Kwa hiyo hapa ni aina ya rushwa ili wafanyakazi waone kuna ongezeko na washawishike kuipigia kura CCM. Kazi ipo, hapati kura mtu hapa.
 
Kumbe JK ni bogus kweli kweli! Ameaambia wafanya kazi kuwa yuko tayari kuzikosa kura zao lkn hawezi kuongeza mishahara. Sasa, kama ni kweli kuwa mshahara umefikia 260k, hii ni rushwa inayokuja kwa sura fulani. TUCTA inatakiwa kum-endorse Dr Slaa na itangaze hivyo, CCM (Chama Cha Mafisadi) ijue hivyo na wannch na wafanyakazi kwa ujumla wajue hivyo. Tunahitaji aggresive mass media campaign kufikisha ujumbe huu kwa wananchi. Hebu niambieni CHADEMA inachangiwaje. CCM lazima kitoke. Sisi Wafanyakazi tunasema kwa JK: Ukitupa rushwa tutaila (hata TAKUKURU hatutawaambia) na kura hutapata.

CHADEMA Hoyeee!

Mkuu nasita kukuunga mkono kama anavyosita Mgaya kwasababu kwanza hatujui Chadema watayashughulikia vp matatizo ya wafanyakazi (isije umeruka mkojo ukakanyaga mabaya zaidi) Pia madai mengine ya TUCTA yanahusiana na mfumo mbovu ya marupurupu na posho zisizokuwa na maana wanazolipwa wakuu serikalini ambazo zinaipa mzigo mkubwa serikali. Pia kodi kubwa wanayokatwa na serikali wafanyakazi Tanzania. Sasa kama hakuna la kueleweka Chadema ni afadhali mie nisipe kura kabisa ili nifurahi roho yangu na familia yangu na washkaji zangu. Kwani tutasema si mmechagua nyie serikali hivyo tustahamili but sie hatukuwapigia kura as simple as that.
 
nashangaa watu mnataka kuangalia salary slip ili kuthibitisha ongezeko..............hivi mkiona ndio iweje.............yaani mnataka kumuangalia NYANI USONI?................aaarrgggghhhh................

wakuu hakuna kurudi nyuma.............msimamo JK alishaweka............."thats fundamental".............kw ahiyo na wafanyakazi tujue kuwa sisi sio mabwege............kudanganywa na pipi..........
 
ongezeko lililosemwa na Rais ni la kufikia 135,000 kima cha chini kutoka 105,000, hii inayoongelewa hapa Tshs 260,000 sijui wameitoa wapi? huenda ni udaku tu wa kupamba gazeti.
si vizuri kuchangia kwa kulaumu na kukejeli ikiwa hatuna hakika na kinachoongelewa
 
Back
Top Bottom