AG awaonya TUCTA kujihusisha na siasa

Mkuu nasita kukuunga mkono kama anavyosita Mgaya kwasababu kwanza hatujui Chadema watayashughulikia vp matatizo ya wafanyakazi (isije umeruka mkojo ukakanyaga mabaya zaidi) Pia madai mengine ya TUCTA yanahusiana na mfumo mbovu ya marupurupu na posho zisizokuwa na maana wanazolipwa wakuu serikalini ambazo zinaipa mzigo mkubwa serikali. Pia kodi kubwa wanayokatwa na serikali wafanyakazi Tanzania. Sasa kama hakuna la kueleweka Chadema ni afadhali mie nisipe kura kabisa ili nifurahi roho yangu na familia yangu na washkaji zangu. Kwani tutasema si mmechagua nyie serikali hivyo tustahamili but sie hatukuwapigia kura as simple as that.

Point noted...........Vyama vya upinzani inabidi wajiandae kulezea watafanyaje kui-improve maisha ya wafanyakazi.................however,
Mkuu kampeni hazijaanza................kuwashurutisha vyama vya upinzani kuwa watafanyeje kwenye maslahi ya wafanyakazi ni sawa na kuwapa silaha CCM.............
 
NIMESHANGAZWA NA USIRI WA SERIKARI KTK ONGEZEKO LA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI HASWA KIPINDI HIKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU,YOTE HAYO NAJUA NI MATOKEO YA PRESHA YA UJUMBE UNAOSAMBAZWA KWA KASI WA WAFANYAKAZI KUINYIMA KURA CHAMA TAWALA KTK UCHAGUZI MKUU UJAO,KWANGU HIKI NI KIINI MACHO,RAI KWA WAFANYAKAZI NI KWAMBA TUSIDANGANGANYIKE:lying::embarrassed1:


Pokeeni pesa kama ni kweli zimengezwa, lakini kura msimpe kabisa. Yeye mwenyewe alisema hana shida nazo, sasa je amerudi kuziomba adharani kama aliyozikataa adgarani?
 
Huu ni uthibitisho kuwa huyu sio kiongozi. Kiongozi ni yule anayejua anatoka wapi na kwenda wapi. Inakuwaje anatekeleza maamuzi kinyumenyume?????????????????????????? Hiyo inaitwa kifafa cha uongozi. Mkulu utavuna ulichopanda!!!!!!!!!!!!!. HAKUNA KURARA.
 
Point noted...........Vyama vya upinzani inabidi wajiandae kulezea watafanyaje kui-improve maisha ya wafanyakazi.................however,
Mkuu kampeni hazijaanza................kuwashurutisha vyama vya upinzani kuwa watafanyeje kwenye maslahi ya wafanyakazi ni sawa na kuwapa silaha CCM.............

Ndio maana nikasema nasita kumsupport yule jamaa wala mkuu wa kaya kwani tunasubiri kampeni zianze ili tufahamu watafanya nini. Tunachokiomba ni kwa vyama vya siasa viwe wawazi na wakweli pasina kuleta kampeni chafu za kuwashambulia wagombea wengine hilo litaharibu swala zima la demokrasia na kusababisha kukosekana kwa mtu makini wa kushughulikia madai ya wafanyakazi
 
Wasiwaonee TUCTA. wakitaka kuandaa bajeti utasikia tasisi mbali mbali kama TCCIA zinaongelea bajeti, zinakosoa ,zinawakosoa mpaka mawaziri. TCCIA na tasisi nyingine haziwezi kukatazwa kuongolea bajeti sababu na wao ni wadau japo si taasisi za kisiasa. Je AG amewai kuwakemea TCCIA kuzungumzia bajeti?

Nadhani AG anajitafutia kesi Ngumu kama ameshindwa kudeal na kesi rahisi za EPA na RICHMOND na RADA.
 
Nani asiyejua nguvu za vyama vya wafanyakazi katika kuchangia mienendo ya kisiasa duniani? Hiyo haijaanza leo? Ilitoke Poland wakati wa kuupinga ukomunist, imetokea Afrika ya Kusini etc. Hivi Tanzania tunawadharau wafanyakazi kwa sisi ni kina nani? Do we think we have got an immune from their political influence? We probably could be making a political suicide if not mistake.
 
Hivi hawa watu wanaolaumu TUCTA wanafahamu objectives za vyama vya wafanyakazi ? Kama kuna sheria inayokataza vyama vya wafanyakazi kujishirikisha katika siasa hiyo sheria ndiyo iliyo ya kikandamizi.

CCM na serikali yao wanajua kuna uwezekano wa kupata upinzani mkubwa kutoka vyama vya wafanyakazi kuliko vyama vya siasa, ndiyo maana wanaleta hizi objections za kikandamizi.

Moja ya central roles za vyama vya wafanyakazi ni kupata "collective bargaining power", unapata "collective bargaining power" kwa ku lobby na ku capitalize on your trade union members, you capitalize on this by clearly endorsing certain parties or candidates.If some of your members don't see this as the Union, they are not forced to vote with the union's choice.In fact if the difference is significant, they should be able to remove themselves from one trade union and join another.

Kuwakataza watu wa vyama vya wafanyakazi ku endorse vyama vya siasa na wagombea ni kuwanyima "collective bargainin power" yao. Kimsingi ni kuwaondoloea uhuru wa kuwa vyama vya wafanyakazi. Vitakuwa toothless stooeges tu.
 
Nina mashaka na hiyo habari ya kupandishwa mshahara, sio ajabu sasa baada ya CCM kuona kwamba mambo yanamwendea kombo mkuu wa kaya wanaanza mbinu ya kununua magazeti na hasa front pages kama walivyofanya leo kwenye gazeti la mwananchi. Wafanyakazi kamwe tusirudi nyuma!!
 
Chama legelege huzaa serikali legelege. Vivyo hivyo Chama kinachoendeshwa kihuni huzaa serikali inayoendesha mambo yake kihunihuni na chama cha kifisadi huzaa serikali ya kifisadi. Ukiona wasemaji wa Chama wanatoa majibu mepesi mepesi kwa maswali muhimu ya kitaifa, ujue na wasemaji wa serikali nao watakurupuka hivyo hivyo hivyo. Dawa hapa ni moja tu, wananchi kuwanyima kura.
 
Bajeti ilikuwa imesema mishahara ingefikia 125,000 sasa kama imebdilisha ghafla na kuwa 250,000 nje ya bajeti.

  • Basi Kikwete alipowaponda TUCTA alikuwa mwongo, ni kweli serikali ina uwezo wa kuwalipa ila alikuwa anatia kiburi tu. Sasa amegundua utamu wa kura za wafanyakazi, ndiyo anatoa hela hizo.
  • Kwa kuwaongopea wazee wa Dar es Salaam, alionyesha kutowaheshimu, hivyo ni bora ajiandae kukataa kura za wazee wa dar es Salaam
  • Kama Yote hapo juu si sahihi, basi hapa kuna EPA nyingine itakayorindima baada ya uchaguzi. yaani serikali ijayo itajikuta inahangaika na kashafa badala ya kutekeleza mambo ya maana. Kama kawaida fedha haramu huwa zinaharabu sana uchumi, tujiandae kwa msukosuko mkubwa sana wa uchumi miaka ijayo, infalation itafikia 15% na zaidi, wakati thamani ya shilingi taporomoka kwa zaidi ya 50%.
 
mbona huyo AG anakuwa anashutumu upande moja tu, je nini kuhusu yale magazeti ya al/el shabab na ya ra yanayo chochea mfarakano wa kidini? kweli chama twawala kimeshikwa kubaya, ndio maaana wanatafuta kila njia ya kutoka, lakini wapi, sasa hivi naona wanatafutavijisababu ili kuwasimamisha vyama vya upinzani/shindani kushiriki uchaguzi.
 
HIVI KWANINI TUSIWAFUNDISHE ADABU VIONGOZI KWA KAULI ZAO. hIVI WAFANYAKAZI TUSHASAHAU TULIVYOTUKANWA NA KUTUKANIWA VIONGOZI WETU. NAFIKIRI IFIKE MAHALI WATU TUKATAE DHARAU ILIYOONYESHWA NA JK KWA KUTOMPA KURA ILI IWE FUNDISHO KWA WENGINE
 
Naibu katibu mkuu wizara ya kazi amesema tamko la katibu mkuu wa Shirikisho la vyama vya ushirika TUCTA kusema kwamba shirikisho hilo litatoa tamko lake kuhusu mgombea urais anayewafaa wafanyakazi, kuwa ni kinyume na seria na kanuni za serikali ya Tanzania, amedai kazi ya shirikisho hilo ni kutetea maslahi ya wafanyakazi na si kuingilia uhuru wao wa kuchagua viongozi wanaowataka.

Na vilevile amedai wafanyakazi wameongezewa mishahara yao na kodi kwenye misharaha yao imepunguzwa.


My Take:
Kama wewe ni mbayuwayu, changanya na ya kwako.
 
Hatudanganyiki kamwe wafanyakazi, waache watoe matamko yao mpaka yaishe, wembe ni ule ule hakuna kura kwa JK. Wapuuzi sana wanaofungwa kengele ili kuilaani TUCTA.
 
Hawa Tucta nao (hasa Mgaya) ni wababaisahaji na wanafki wakubwa, gazeti moja la kiswahili leo linamnukuu katibu mkuu wa Tucta akisema hivi " Matatizo yetu na serikali yamepungua...kiasi kilichoongezwa kinapunguza makali ya maisha kwa watumishi wa umma. Tunafikiria kumpa pilau yetu kiongozi anayesikiliza matatizo ya watu wake"

Huu ni unafiki wa hali ya juu.
 
Inasikitisha na kuhusunisha kwa mfa maji kila kitu anashika anazani kinaweza kumuokoa! haya shika na nyaya za umeme tuone kama zitakuokoa.
 
Hawa Tucta nao (hasa Mgaya) ni wababaisahaji na wanafki wakubwa, gazeti moja la kiswahili leo linamnukuu katibu mkuu wa Tucta akisema hivi " Matatizo yetu na serikali yamepungua...kiasi kilichoongezwa kinapunguza makali ya maisha kwa watumishi wa umma. Tunafikiria kumpa pilau yetu kiongozi anayesikiliza matatizo ya watu wake"

Huu ni unafiki wa hali ya juu.

...Ungetaja jina la gazeti hilo ingekuwa vyema zaidi maana hata magazeti nayo sasa yana vyema yanavyopendelea na yapo tayari kumuwekea mtu maneno mdomoni ili kukidhi haya yao..
 
Back
Top Bottom