Afukuzwa Chuo Kikuu Baada ya Kuvaa Kimini Kilichosababisha Mtafaruku

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,149
November 10, 2009

Chuo kikuu kimoja nchini Brazili kimemfukuza chuo kikuu mwanafunzi wake wa kike aliyejaribu kuingia darasani akiwa amevaa sketi fupi sana na kusababisha mtafaruku mkubwa sana chuoni hapo.

Chuo kikuu binafsi cha Bandeirante University cha mjini Sao Bernardo do Campo, nje kidogo ya jiji la Sao Paulo, kimemsimamisha masomo mwanafunzi wake wa kike Geisy Arruda mwenye umri wa miaka 20 ambaye alisababisha mtafaruku mkubwa sana chuoni hapo mwezi uliopita baada ya kujaribu kuingia darasani akiwa amevaa kimini kifupi sana cha rangi ya pinki.

Taarifa iliyotolewa na chuo hicho ilisema kwamba Arruda alifanya kitendo ambacho kipo nje ya maadili ya jamii na misingi ya taaluma.

Arruda alikuwa gumzo kwenye vyombo vya habari mwezi uliopita baada ya kuokolewa na polisi kutokana na kipigo na mashambulio ya kijinsia aliyokuwa akifanyiwa baada ya kuingia darasani akiwa amevaa kimini kilichokaa kimitego mitego.

Ilimbidi Arruda ajisitiri kwa kutumia koti la profesa wake huku akisindikizwa na polisi kutoka nje ya chuo hicho kufuatia matusi na mashambulio ya kijinsia aliyokuwa akifanyiwa na wanafunzi wenzake wenye hasira.

Baada ya tukio hilo la oktoba 22, Arruda amekuwa akitokea kwenye televisheni mbali mbali za Brazili akisema kuwa anapata tabu sana kurudia maisha yake ya kawaida baada ya kudhalilishwa.

Uongozi wa chuo kikuu hicho ulibandika tangazo la kumsimamisha masomo Arruda siku ya jumapili.

Tangazo hilo lilisema kuwa Arruda amesimamishwa masomo kwa kuingia darasani akiwa amevaa vazi lisilofaa na lisiloendana na mazingira ya chuo kikuu.

Akielezea kusimamishwa kwake masomo kwasababu ya kimini alichovaa, Arruda alisema kuwa ameonewa.

"Mimi ndiye niliyedhalilishwa, imekuwaje nifukuzwe chuo?", alisema Arruda.

Arruda alisema kuwa amezisoma habari za kufukuzwa kwake chuo kwenye magazeti lakini hadi sasa bado hajapokea barua ya kusimamishwa masomo.

Arruda amesema kuwa uongozi wa chuo kikuu hicho ulimwambia kuwa utamruhusu aendelee na masomo yake chuoni hapo lakini aambatane na mlinzi wake wakati wote.
 
mungu wangu hii sheria ikifika UDSM si nusu ya wanawake tutawasimamisha shule...ooooh no waiangalie upya
 
r2438637289.jpg

Brazilian student Geysi Villa Nova Arruda attends a media conference in Sao Bernardo do Campo, November
 
Mh, huyu kwa kumwangalia tu anaonekana ana kiburi kwanza kutokana na facial expression yake. Pia anaonekana ni "exhibitionist", anapenda kuonesha sehemu za mwili wake.

Duh, eti anashangaa kufukuzwa wakati yeye ndio amedhalilishwa!! Jamani!
 
Kibs,unayo ile aliyokuwa amevaa hicho kimini?

Siku nyingine tafuta mwenyewe kwenye GOOGLE na si uulize.

Acha uvivu na ujitume....

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=z9AqaIA9akk[/ame]
 
Siku nyingine tafuta mwenyewe kwenye GOOGLE na si uulize.

Acha uvivu na ujitume....


Je, habari zinazowekwa hapa nazo ziwe ni kwa muhtasari tu?
Tuanze kuweka vichwa vya habari pekee ili watu wakitaka kujua zaidi waende ku-google?


attachment.php

Geysi Villa Nova Arruda
 

Attachments

  • Geysi Villa Nova Arruda.JPG
    Geysi Villa Nova Arruda.JPG
    24.5 KB · Views: 207
Je, habari zinazowekwa hapa nazo ziwe ni kwa muhtasari tu?
Tuanze kuweka vichwa vya habari pekee ili watu wakitaka kujua zaidi waende ku-google?


Mkuu,

Ukiona habari imeandikwa nusunusu na unataka kusoma zaidi si U-Google mwenyewe uitafute? Sasa unataka Kibs akutafutie hadi picha? Mbona wewe umeenda kupekua ingawa umetuletea picha ya kimini ila si cha huyu binti. Binti ni amejaa kwelikweli na siyo huto tuMIWA utafikiri miguu ya mkimbiaji mbio ndefu....... KIP-Tanuru.
 
Mbona vimini ni poa tu cha msingi vivaliwe na wanawake wenye umri zaidi ya 14
 
Mkuu,

Ukiona habari imeandikwa nusunusu na unataka kusoma zaidi si U-Google mwenyewe uitafute? Sasa unataka Kibs akutafutie hadi picha? Mbona wewe umeenda kupekua ingawa umetuletea picha ya kimini ila si cha huyu binti. Binti ni amejaa kwelikweli na siyo huto tuMIWA utafikiri miguu ya mkimbiaji mbio ndefu....... KIP-Tanuru.



Umeanza kuona tatizo la kila mmoja wetu akienda ku-google?
 
Kwakuwa umejivika u-kibs, haya haraka nitafsirie hiyo lugha wanayoongea.

By the way, nilihitaji picha tu.Umejituma ku-google 'bila uvivu' umerudi na unachotaka wewe sio nilichoomba.

Wee vipi?

Umeomba PICHA, nikakutumia. Kama ni Video, ulitakiwa uzime sauti na uangalie picha tu. Wewe kwa URAFI na UROHO papo, ukaona uongezee na ufaidi zaidi hadi SAUTI.

Na mimi nilifahamu mapema utataka kuangalia na kusikiliza. Nikakuwekea KIRENO. Umesikiliza hukuambua kitu. Kama wataka kuelewa kinachosemwa, basi unaweza ku-google translation.

Ila Mkuu, umenivunja mbavu hayo maneno kwenye BOLD... hahaaaa U made my day.......Thanks.
 
Umeanza kuona tatizo la kila mmoja wetu akienda ku-google?

Yaani unasema TATIZO? Macho yamefaidi sana sana. Umenikumbusha Summer ikifika nchi za wenzetu hasa ukienda baharini. Miaka hizo never miss. Maana utakuta vimini, bikini na hadi G-string.

Hata ukiona nyingine, tena anaweza kuwa hata Mchina, wewe weka..... Nani kakuambia Sikonge tunapolia hatuli? Tunapomjadili Mbrazil, twaweza kuwaangalia Wahindi, Waarabu ........ Hata kama ipo ya Mama kubwa yuko kwenye kimini, wewe weka..... :)

Mwisho wameandika alikuwa kavaa mini-skirt ya PINK. Sasa wee hiyo umeweka ndiyo PINK? Walau ungeliweka hii hapa chini:

vs+skirt2.jpg
 
Source ya hiyo picha hii hapa by the way.
Inawezekana demu ni huyo huyo ila hili ni tukio tofauti?

http://www.peru.com/noticias/portad...-con-minifaldas-a-sus-companeros-en-Brasil---



A university in the Brazilian state of Sao Paulo announced the expulsion of a student to attend classes with very short skirts and "provocative attitude" had to accept the girl again after the local government intervened.

The expulsion of the student travel Geysi Villa Nova Arruda was due to a "flagrant disregard for ethical principles, the academic dignity and morality," according to an announcement released today by the University Bandeirantes in some newspapers of St. Paul.

The incident that led to the expulsion occurred a few days ago, when the student was verbally abused by dozens of classmates because of the attitude "provocative", and go to class with a short pink dress. Now, police in Sao Paulo state would investigate the facts and the girl's attackers (a few hundred students who called her "*****").
In addition, the National Union of Students (UNE) of Brazil asked the University to publicly retract the expulsion of Arruba and that the perpetrators are duly prosecuted and convicted, something that is on the line taken by the authorities of the university, which already suspended ten students for the episode.
The dimensions of the events were such that the university authorities were forced to call the police to escort to Villa Nova Arruda and could leave the classroom without being assaulted by their colleagues in the study.

Pictures of the incident were recorded by some students and hanging on the porch of videos on Youtube, after which had impact on some TV channels.

According to the announcement published by the university, "it was found that the student attended the premises of the campus with inadequate clothing, a position incompatible with the college environment and, despite having been alerted, did not change their behavior."

The legal adviser from the university, Lecioni Decio Machado, said the portal G1 that the cause of the expulsion was not the dress, but certain gestures and attitudes "of the student, who were rejected even by his own comrades.
 
Lazydog,

Niamini mie hapa Mkuu. Huyo dada wameweka picha tu. Ukiangalia picha zake nyingi, yeye havai hivyo. Pia hiyo miguu siyo yake. Na kama ni yake basi walipiga miaka kadha ya nyuma. Huo ukurasa kwanza ni wa PERU na habari imetokea Brazil. Nafikiri wamefanya tu kuweka picha ili afahamu MINI ni nini na haswa baada ya kutokuwa na picha ya kimini cha Pink....
 
Back
Top Bottom