UZUSHI Afrika Mashariki yazindua noti yake iitwayo SHEAFRA

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Habari wakuu,

Nimeona taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki imetambulisha noti yake itakayotumika katika nchi wanachama, iliyopewa jina la SHEAFRA (SHF). Wengi wameinukuu akaunti kutoka mtandao wa X (zamani Twitter) inayojulikana Government of East Africa

Moja ya chombo kikubwa kilichoinukuu akaunti hiyo ni pamoja na ITV , binafsi bado nina mashaka na hii taarifa kutokana na kwamba akaunti maalum ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ninayoifahamu siyo hii.

Ukweli ni upi?


IMG_20240304_082413_660.jpg
 
Tunachokijua
Jumuiya ya Afrika Mashariki au Mtangamano wa Afrika Mashariki ni muundo wa kisiasa unaounganisha nchi saba za kanda ya Maziwa Makuu ya Afrika Mashariki: Tanzania, Burundi, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Sudan Kusini na Uganda.

Kwa sasa eneo la Mtangamano ni km2 4,810,363, likiwa na wakazi wamaokadiriwa kufikia 281,050,447(kadirio la mwaka 2022), iwapo ingekuwa nchi moja ingekuwa ya nne duniani.

Jumuiya yenye jina hilo imepatikana mara mbili katika historia: jumuia ya nchi tatu kati ya hizo ilianzishwa mwaka 1967, lakini ilisambaratika mwaka 1977.

Baada ya kuvunjika, kwenye miaka ya 1990 majaribio ya kujenga upya umoja yalionekana tena. Marais Daniel arap Moi wa Kenya, Ali Hassan Mwinyi wa Tanzania, na Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda walipatana katika Mkataba wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki huko Arusha, tarehe 30 Novemba 1993, na kuanzisha Tume ya Ushirikiano ya nchi hizi tatu. Shughuli ya kuzileta pamoja nchi hizi kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni, utafiti na teknolojia, ulinzi, usalama, masuala ya kisheria na kimahakama ilianza.

Mkataba wa kufufua jumuiya ulitiwa sahihi tarehe 30 Novemba 1999 ukaanza kuwa rasmi tarehe 7 Julai 2000. Vyombo vya Jumuiya mpya ya Afrika ya Mashariki vilianza kufanya kazi mnamo Januari 2001 penye makao makuu ya jumuiya hii huko Arusha. Mkataba wa 2004 uliweka msingi wa Umoja wa Forodha ulioanzishwa 2005.

Mwaka 2010, Mtangamano ulitangaza soko la pamoja kwa bidhaa, kazi na mitaji kati ya nchi hizo, kwa lengo la kuanzisha Pesa ya pamoja na hatimaye Shirikisho kamili.

Kuna majadiliano ya kuanzisha shilingi mpya ya pamoja kwa nchi za Jumuia ya Afrika ya Mashariki. Kwanza ilitarajiwa kuanzishwa mwaka 2012, ikasogezwa mwaka 2015, kisha mwaka 2024. Mwaka 2013 ulisainiwa mkataba wa kuamua kuanzisha pesa ya pamoja ndani ya miaka 10.

Katika mitandao ya kijamii umesambaa uvumi ambao ulioonesha picha inayodaiwa kuwa ni noti iliyotangazwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa ndiyo pesa yao ya pamoja na itajulikana kwa jina la SHEAFRA ( SH: Shilling, EA: East Africa FRA: Franc)

Uvumi huo ulichapishwa kwa mara ya kwanza na akaunti yenye jina Government of East Africa katika mtandao wa X ambayo ilifunguliwa Oktoba 2023 ikiwa na alama ya tiki kuonesha ni akaunti halali.
screenshot-2024-03-04-at-03-12-24-government-of-east-africa-on-x-the-east-african-sheafra-of-png.2923656

Baada ya kusambaa kwa uvumi huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, January Makamba kupitia akaunti yake ya X aliandika kanusho la kutolewa kwa pesa hiyo na Jumuiya ya Afrika Mashariki huku akifafanua kuwa taarifa siyo za kweli makubaliano bado hayajakamilika na mapendekezo ya kufikia hatua hiyo ni mpaka 2031, huku akiitaja akaunti rasmi ya Jumuiya hiyo.

screenshot_20240303_225357_x-jpg.2923606
Pia, kupitia akaunti iliyotajwa na Waziri Januari Makamba kuwa ndiyo akaunti rasmi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Iliyoanzishwa mwaka 2009 katika mtandao wa X imechapisha kanusho linalosema kuwa taarifa ya uwepo wa pesa hiyo si la kweli na pesa hiyo ni feki.

The EAC Secretariat wishes to inform all our stakeholders that the Partner States' journey to a single currency is still a work in progress. Kindly ignore any rumours circulating in social media on the unveiling of new banknotes for the region.
1709512341729-png.2923659

JamiiCheck, imeifuatilia akaunti inayojiita Government of East Afrika na kubaini ilifunguliwa rasmi Oktoba 2023, imekuwa ikichapisha vitu vingi vinavyohusiana na mambo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na visivyohusiana na Jumuiya ikiwemo utani.
1709513301269-png.2923663
Pia mara ya kwanza kuchapisha vitu kwenye akaunti hiyo ilikuwa ni Januari 20, 2024, Hiyo inathibitisha shaka kuwa akaunti hii ni akaunti bandia na Si akaunti halisi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, inatuonesha kuwa akaunti hii bandia ililipia kupata uthibitisho wa tiki kwa kuwa kwenye mtandao wa X kwa sasa kupata uthibitisho ni kwa njia ya kulipia tu.
1709513525043-png.2923667

Picha ya kwanza kuchapishwa na akaunti ya Government of East Afrika
Jamiicheck pasi na shaka imejiridhisha kuwa akaunti ya X yenye jina Government of East Africa si ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwamba taarifa za kutolewa kwa fedha ya pamoja yenye jina la SHEAFRA ni za kutungwa na uzushi.

Attachments

  • 1709514024933.jpeg
    1709514024933.jpeg
    81.2 KB · Views: 10
Hii taarifa imeleta taharuki kwenye macho ya wananchi. Nimeisambaza taarifa hiyo ya Kuwepo kwa Sarafu ya Sheafra zaidi ya ma group Sita ya Whatsup, kumbe sio ya kweli.

Ombi langu kwenu ni kuwataka wananchi radhi; Ili jambo hili liwe sawa katika jamii, Hata kama na Nyie mlitoa kwenye Media Nyingine. 🙏🏾🙏🏾🙏🏾
 
Hii taarifa imeleta taharuki kwenye macho ya wananchi. Nimeisambaza taarifa hiyo ya Kuwepo kwa Sarafu ya Sheafra zaidi ya ma group Sita ya Whatsup, kumbe sio ya kweli.

Ombi langu kwenu ni kuwataka wananchi radhi; Ili jambo hili liwesawa katika jamii, Hata kama na Nyie mlitoa kwenye Media Nyingine. 🙏🏾🙏🏾🙏🏾
 
Siamini kama jamii forum walifany jambo wasilolijua, labda wakati haujafika, nipo radhi kuamini jamii forum zaidi ya mkanushaji.

Kama jamii forum kwa 100% wamekurupuka kwenye hili, then watakuwa ni watu wa hovyo sana kuliko maelezo.
 
Hii taarifa imeleta taharuki kwenye macho ya wananchi. Nimeisambaza taarifa hiyo ya Kuwepo kwa Sarafu ya Sheafra zaidi ya ma group Sita ya Whatsup, kumbe sio ya kweli.

Ombi langu kwenu ni kuwataka wananchi radhi; Ili jambo hili liwe sawa katika jamii, Hata kama na Nyie mlitoa kwenye Media Nyingine.
Ulitaka uwe wa kwanza kupost uonekane upo up to date. Tusiwe wepesi wa kushare taarifa za mitandaoni mpaka pale tunapokuwa na uhakika kwa 100%
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom