Afrika Kusini na Congo DRC zasaini mkataba wa ujenzi wa bwawa la Umeme la Megawati elfu 70 mto Congo

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,909
Nchi za Afrika Kusini na Congo DRC zimetiliana saini ya mkataba wa uendelezaji wa ujenzi wa bwawa la umeme la Megawati elfu 70 ama GW 70 katika maporomoko ya mto Congo.

Mradi huo unaoitwa Grand Inga Dam Project uko mto Congo na unakadiriwa kugharimu Dola Bilioni 80 hadi kukamilika kwake na utazalisha megawati elfu 70. Iwapo litakamilika litakua ndio bwawa kubwa kuliko yote Duniani

Kumbuka Tanzania tunaenedeleza bwawa la mwalimu Nyerere la Megawati 2115 sawa na Gigawatt 2.

Pia kumbuka Afrika Kusini inazalisha umeme ama ina uwezo wa kuzalisha umeme Megawati elfu 60, ama Gigawatt 60, hii ni sawa na 50% ya umeme wote unaozalishwa Afrika nzima lakini bado haitoshelezi mahitaji yake kwani kumekua na mgao mkubwa sana wa umeme.

Ukanda huu wa kusini mwa jangwa la sahara(Southern African Power Pool) una upungufu mkubwa sana wa umeme.

Wale wazee wa umeme wa maji umepitwa na wakati mpo?


China pia anatarajia kujenga Bwawa la umeme la kuzalisha megawati elfu 60 ili kukabiliana na mazingira na hali ya hewa.
 
Hapo labda ni joint ya HEP zaidi ya moja...

Kwa moja ni ngumu sanaa,
GW 70 hio sio kawaida,

Mchina mwenyewe na Three Gorges Dam kagonga kwenye 22.5GW na wanasema ni risk sana, mana pressure ni kubwa mno wanaogopa kingo kupasuka.
 
Sadec wangekuwa na ajili walitakiwa kychabgua share hata wakajenga Kwa awamu 7 kila awamu megawat elf 10,, harafu tunagawana umeme equally Kwa state members
 
Zitto na vibaraka wake wako wapi kupinga maana ni uharibifu wa mazingira
 
Hapo labda ni joint ya HEP zaidi ya moja...

Kwa moja ni ngumu sanaa,
GW 70 hio sio kawaida,

Mchina mwenyewe na Three Gorges Dam kagonga kwenye 22.5GW na wanasema ni risk sana, mana pressure ni kubwa mno wanaogopa kingo kupasuka.
Nadhani unazijenga tofauti tofauti..Sielewi Africa kwanini kama Sadec na East Africa tulishindwa kuchabgua tukazlisha umeme tukagawa elf 5000
 
Zilikuwa siasa dhidi ya Magufuli. Umeme wa maji ni wa uhakika na nafuu sana.
Madalali kina Zito, Mhongo et al waliokua wanasema umeme wa maji umepitwa na wakati.

Walikua wanapigia debe waume zao kina Siemens,, General Electric na Mitsubishi wenye mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi.

Ajabu, wakati wanapiga kelele, waume zao wa huko Ulaya wanajenga mabwana makubwa sana ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji, soma hapa Canada wanajenga bwawa la umeme la Megawati 1100, ama wao hawajui maji yamepitwa na wakati?

Wakati waume zao wanawadanganya kwamba maji yamepitwa na wakati, huko kwao wana miradi ya green energy projects na zero carbon emissions ana ESG policy kutaka nchi ziachane na kuzalisha umeme kwa kutumia fossil fuels na kwenda kwenye renewable energy.

Kweli ukipigwa miti anaekupiga miti anakupangia hata cha kusema.
 
Hawajatiliana Saini, Bali wamekubaliana kwenda mbele na mchakato wa hiyo Project (kimazungumzo)..

ACHA kupotosha watu..
 
Hapo labda ni joint ya HEP zaidi ya moja...

Kwa moja ni ngumu sanaa,
GW 70 hio sio kawaida,

Mchina mwenyewe na Three Gorges Dam kagonga kwenye 22.5GW na wanasema ni risk sana, mana pressure ni kubwa mno wanaogopa kingo kupasuka.
Wamepanga kujenga "a series of 7 hydro power stations along the Congo River". Hivyo nadhani yatakuwa mabwawa 7 ambayo kila moja litakuwa na uwezo wa 10 Gigawatts.
 
Back
Top Bottom