Afrika inakufundisha kuwa mvumilivu

Pantosha

JF-Expert Member
Sep 22, 2022
349
464
Kwa miezi hii kadhaa niliyokaa nchini baada ya kuishi miaka ya ujana wangu takribani yote nje ya bara la Afrika, nimegundua kuwa waafrika ni watu wavumilivu sana. Hali hii sikuiona mahali pengine tofauti na huku kwetu.

Mfano: Muendesha pikipiki anaweza kuamua kupiga kelele na pikipiki yake, hakuna anayejali hata kama watu wanachukizwa na kitendo hicho.

Mwenye bar anaweza kufungulia mziki kwa sauti kubwa, hakuna anayejali.

Kanisani/Msikitini wanaweza kuhubiri kwa kutumia vipaza sauti, hakuna anayejali.

Usafi kwenye stend za mabasi, sokoni siyo wa kuridhisha, ila hakuna anayejali.

Huduma zinaweza kutolewa chini ya kiwango, hakuna anayejali.

Muhudumu anaweza akaamua kukucheleweshea order yako au chenji, hakuna anayejali.

Barabara za mitaa zinaweza kuharibika, hakuna anayejali.

Kwakweli ninawapongeza wote kuwa watu wa aina yake wenye maadili ya Kiafrika.
 
Kwa miezi hii kadhaa niliyokaa nchini baada ya kuishi miaka ya ujana wangu takribani yote nje ya bara la Afrika, nimegundua kuwa waafrika ni watu wavumilivu sana. Hali hii sikuiona mahali pengine tofauti na huku kwetu.

Mfano: Muendesha pikipiki anaweza kuamua kupiga kelele na pikipiki yake, hakuna anayejali hata kama watu wanachukizwa na kitendo hicho.

Mwenye bar anaweza kufungulia mziki kwa sauti kubwa, hakuna anayejali,

Kanisani/Msikitini wanaweza kuhubiri kwa kutumia vipaza sauti, hakuna anayejali,

Usafi kwenye stend za mabasi, sokoni siyo wa kuridhisha, ila hakuna anayejali.

Huduma zinaweza kutolewa chini ya kiwango, hakuna anayejali,

Muhudumu anaweza akaamua kukucheleweshea order yako au chenji, hakuna anayejali,

Barabara za mitaa zinaweza kuharibika, hakuna anayejali,

Kwa kweli ninawapongeza wote kuwa watu wa aina yake wenye maadili ya kiafrika
 
Uko sahihi kabisa, When i came back in Tanzania from States nilipata changamoto sana, unaenda public bus station kubwa kama Mawasiliano, unakunywa maji, ukimaliza hauoni public waste bins za ku dispose ile chupa na ma afisa mazingira wapo tu ofisini. Nilijitahidi kuwa nazibeba naenda kuzitupia nyumbani hadi siku nilipochoka ndo nikaanza na mimi kuchafua mazingira kama vile i am an uneducated swindler. Africa ni kugumu jamani.
 
Watu wananjali, kama unavyoona wewe nasi tuliisha yaona yote hayo. Lakini Waliopewa dhamana, hawaoni kama hayo ni vipaumbele vyao.
Hata ukipewa dhamana, bado utashindwa ku implement kama ulaya, utafanyiwa figisu mpaka ushangae.

Ni kuwa, Serikalini kuna watu wengi wenye mawazo chanya, lakini wanakosa nafasi ya kuonesha uwezo wao.

Utapigwa zengwe mara, anataka cheo, anajifanya anajua kazi, anataka kum outshine boss wake, yani mambo meengi ya kukatisha tamaa.

Tatizo la Africa specifically TZ ni Watanzania wenyewe ikichagizwa na Ujinga,
 
Kwa miezi hii kadhaa niliyokaa nchini baada ya kuishi miaka ya ujana wangu takribani yote nje ya bara la Afrika, nimegundua kuwa waafrika ni watu wavumilivu sana. Hali hii sikuiona mahali pengine tofauti na huku kwetu.

Mfano: Muendesha pikipiki anaweza kuamua kupiga kelele na pikipiki yake, hakuna anayejali hata kama watu wanachukizwa na kitendo hicho.

Mwenye bar anaweza kufungulia mziki kwa sauti kubwa, hakuna anayejali,

Kanisani/Msikitini wanaweza kuhubiri kwa kutumia vipaza sauti, hakuna anayejali,

usafi kwenye stend za mabasi, sokoni siyo wa kuridhisha, ila hakuna anayejali.

Huduma zinaweza kutolewa chini ya kiwango, hakuna anayejali,

Muhudumu anaweza akaamua kukucheleweshea order yako au chenji, hakuna anayejali,

Barabara za mitaa zinaweza kuharibika, hakuna anayejali,

Kwa kweli ninawapongeza wote kuwa watu wa aina yake wenye maadili ya kiafrika
Mambo madogo sana haya ......tunalilia kwanza umeme na maji, mfumuko wa bei na chakula ni shida tuje kugombana na boda boda?
 
Sahihi mkuu.

Majungu ni mengi na wachache wanataka changes
 
Huu mbona siyo uvumilivu? Ni ujinga!
 
Wakati mwingine ni ujinga na upumbavu unatusumbua. Mtu anaingia ndani ya bus zuri la kumsafirisha aendako lakini jambo la ajabu anaamua tu kung'oa vile vijitaa vilivyowekwa kwa juu pale katika staff carrier hadi unabaki unashangaa.

Vimejengwa vyoo vizuri sana pale stand ya mabasi msamvu Morogoro, mtu anaenda kutia jiwe ndani ya sinki la choo!!!! Sijui ni akilli ya namna gani!!!?

Unakuta mtu kapakaza kinyesi ukutani eti anaweka chata yake...aaaarrrrgggggh! Ni shida kubwa
 
Mambo madogo sana haya ......tunalilia kwanza umeme na maji, mfumuko wa bei na chakula ni shida tuje kugombana na boda boda?
Kufumbia macho haya madogo ndiyo yanayosababisha hata hayo makubwa watu wasijali.
Mfano: Watu wanakata maji mwezi mzima, hakuna anayejali.
Umeme kukatika mara kwa mara, hakuna hata anayeshtuka,
Hata hospitali zikikosa dawa, hakuna anayeona ni shida,
Miundombinu ya barabara mibovu, sisi tunapeta tu.
 
Kwa miezi hii kadhaa niliyokaa nchini baada ya kuishi miaka ya ujana wangu takribani yote nje ya bara la Afrika, nimegundua kuwa waafrika ni watu wavumilivu sana. Hali hii sikuiona mahali pengine tofauti na huku kwetu.

Mfano: Muendesha pikipiki anaweza kuamua kupiga kelele na pikipiki yake, hakuna anayejali hata kama watu wanachukizwa na kitendo hicho.

Mwenye bar anaweza kufungulia mziki kwa sauti kubwa, hakuna anayejali,

Kanisani/Msikitini wanaweza kuhubiri kwa kutumia vipaza sauti, hakuna anayejali,

usafi kwenye stend za mabasi, sokoni siyo wa kuridhisha, ila hakuna anayejali.

Huduma zinaweza kutolewa chini ya kiwango, hakuna anayejali,

Muhudumu anaweza akaamua kukucheleweshea order yako au chenji, hakuna anayejali,

Barabara za mitaa zinaweza kuharibika, hakuna anayejali,

Kwa kweli ninawapongeza wote kuwa watu wa aina yake wenye maadili ya kiafrika
Tatizo kubwa la Afrika na Mwafrika ni kukosekana kwa ustawi wa ustaarabu wa jamii nzima wenye kuendana na matakwa ya wakati sambamba na mazingira ya sasa ya dunia.
Ustaarabu wenye kuakisi mambo mazuri upo kwa mtu mmoja mmoja badala ya jamii pana.

Licha ya muingiliano mkubwa wa ustaarabu wa kigeni, bado Afrika haitaki kubadilika. Afrika imejikuta ikiiga baadhi ya mambo mazuri nusu nusu, huku yenyewe ikizidi kukumbatia mambo mengi mabaya na yenye machukizo. Viongozi hawajali, hali kadhalika raia wa kawaida, kibaya zaidi kuna suala la kukatishana tamaa.

Ni lazima tuelewe kuwa ustaarabu wa kiafrika ni mtindo mzima wa maisha ya watu ambao hujumuisha utamaduni, taratibu za kijamii, imani za kidini, maadili, desturi, falsafa, imani, siasa, na sanaa ambavyo asili yake ni Afrika. Ni lazima tukiri kuwa biashara ya utumwa na ukoloni vilikuwa na athari hasi katika ustawi wa ustaarabu wa Mwafrika, na hata kujikuta ni muhanga mkubwa wa tamaduni mbaya za kigeni.

Utakubaliana na mimi kuwa nchi nyingi ziliwahi kuwa makoloni, mathalani za Latin America, Asia na kwingineko, lakini zilijitahidi kurithi mambo mazuri tu yaliyokuwepo katika ustaarabu wa kigeni, na kuendelea pia na mambo mazuri yaliyokuwapo katika ustaarabu wao wa asili. Lakini mambo mengi yaliyokuwa ni machukizo jamii pana ya watu waliachana nayo.

Kwa "mindset" ya Mwafrika wa kawaida, dhamira huweza kumchoma kwa vitu vinavyoonekana, yaani endapo kosa linaonekana kutendeka kwa maneno na vitendo tu, lakini kamwe dhamira haimchomi endapo mtu atakosea kwa mawazo ama kutokutimiza wajibu wake. Hii ndiyo sababu wenzetu hutudhihaki kwa maneno, "Kila kitu kinawezekana Afrika"
 
Kiwango cha ustaarabu na kujali kipo chini sana kwa ukweli katika bara letu, labda bado tunaendelea na evolution au umasikini uliopitiliza unatuathiri sana kiakili na kisaikolojia kiasi kwamba baadhi ya mambo ya hovyo tunayachukulia ya kawaida tu.
 
Kwa miezi hii kadhaa niliyokaa nchini baada ya kuishi miaka ya ujana wangu takribani yote nje ya bara la Afrika, nimegundua kuwa waafrika ni watu wavumilivu sana. Hali hii sikuiona mahali pengine tofauti na huku kwetu.

Mfano: Muendesha pikipiki anaweza kuamua kupiga kelele na pikipiki yake, hakuna anayejali hata kama watu wanachukizwa na kitendo hicho.

Mwenye bar anaweza kufungulia mziki kwa sauti kubwa, hakuna anayejali,

Kanisani/Msikitini wanaweza kuhubiri kwa kutumia vipaza sauti, hakuna anayejali,

Usafi kwenye stend za mabasi, sokoni siyo wa kuridhisha, ila hakuna anayejali.

Huduma zinaweza kutolewa chini ya kiwango, hakuna anayejali,

Muhudumu anaweza akaamua kukucheleweshea order yako au chenji, hakuna anayejali,

Barabara za mitaa zinaweza kuharibika, hakuna anayejali,

Kwa kweli ninawapongeza wote kuwa watu wa aina yake wenye maadili ya kiafrika
Karibu nyumbani na wewe uwe mvumilivu
 
Back
Top Bottom