WA-UKENYENGE
JF-Expert Member
- Oct 1, 2011
- 2,918
- 1,233
Kwenye Red, mkuu hayo ndiyo mnalishwa na kumeza propaganda za serikali bila kuangalia au kufikiria. Kuna madai zaidi ya kumi mkuu, mafao ni mojawapo, basi kama serikali haiwezi kuwalipa mafao yanayowapa moyo iboreshe mazingira ya kazi, iongeze dawa, inunue vifaa vya kufanyia kazi! Haiingii akili wewe hapo ukiwa kama Daktari mgonjwa unayemtibu anapoteza maisha kwa kukosa pamba za kusafishia, sindano au vifaa ambavyo gharama yake inaweza isifike hata elfu kumi lakini unashangaa mtu anapoteza maisha mbele yako. Kisaikolojia daktari mwenyewe anaweza kuathirika kwani uwezo wa kumtibu anao, lakini vitendea kazi hakuna huku akiangalia serikali inamatumizi ya kianasa.Serikali hasa katika awamu hii ya nne imewafanyia mengi mazuri madari, hata hivyo inaonekana hawaoni chochote kizuri walichofanyiwa. Mtaka yote kwa pupa hukosa ...... Nawaomba watumie busara. Kwanini kuwaacha watanzania wagojwa kufa kwa maradhi, kisa mafao ya ziada. Kumbukeni mmesoma kwa kodi za watanzania wanyonge na wao walikuwa na mategemeo makubwa kwenu. Haya! Nawashauri madaktari muache mgomo mara moja na muonyeshe uzalendo wa hali ya juu. Kama kuna kazi baadhi yenu wameona zinalipa zaidi .. Vilevile wajiepushe kujichukulia sheria mkoni kama kuwapiga askari.
Uzalendo huanzia kwa viongozi wenyewe, mimi nawewe ni walipa kodi tena pengine kwa kulazimishwa lakini ingekuwa tunapewa fedha zote za basic salary harafu ndiyo tukalipe kodi, huenda serikali ingekuwa imeshauza hadi barabara maana ningekuwa radhi kujitolea kuipeleka hiyo fedha kwenye moja ya hospitali kusaidia walau kero moja.
Mkuu ningefurahi zaidi kama ungepitia ile orodha ya madai ya madaktari nauhakika hata kama unatibiwa private hospitals, inakugusa moja kwa moja kwani una ndugu, jamaa, rafiki na majirani wanaoumia pengine wanapoteza maisha kwa kukosa vitu tajwa hapo juu.