Afghanistan: Zaidi ya watu 600 wamefanikiwa kupanda ndege ya Jeshi la Marekani

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
416
Baada ya kushuhudia Waafghanistan wakijaribu kudandia ndege ya Jeshi la Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khamid Karzai mjini Kabul jana, Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetoa picha inayoonesha watu 640 wakiwa ndani ya ndege yake ya kijeshi.

Idadi hiyo ya watu inatajwa kuwa zaidi ya mara tano ya uwezo wa ndege hiyo kubeba abiria na moja ya idadi kubwa zaidi kuwahi kubebwa katika ndege hiyo aina ya Boeing C-17 Globemaster III. Waliofanikiwa kuingia ndani ya ndege hiyo walitumia mlango ambao haukufungwa vizuri wakati ndege hiyo ikiwa katika uwanja wa ndege mjini Kabul.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imeripoti kuwa haikuwa na mpango wa kuwabeba watu hao, lakini ililazimika kutokana na vurugu zilizotokea katika uwanja wa ndege jana. Inaripotiwa kuwa watu wawili wamefariki baada ya kuanguka kutoka kwenye ndege hiyo.

Kujaa kwa watu katika Uwanja huo wa Ndege kulitokana na taarifa za uzushi kusambaa awali Mjini Kabul kuwa Jeshi la Marekani linatoa usafiri wa bure kuwapeleka wananchi wa Afghanistan kwenda Marekani na Kanada, ndipo mamia ya watu walipovamia uwanja huo wakijaribu kupata usafiri huo wa bure na kuyaokoa maisha yao kutoka kwa Wataliban.

Waliofanikiwa kupanda ndege hiyo - wakiwamo wanawake na watoto wachanga - wamefanikiwa kutua salama nchini Qatar.

Wapiganaji wa Taliban wamefanikiwa kuchukua udhibiti wa Mji Mkuu na mipaka ya nchi. Uwanja huo wa ndege ndio sehemu pekee iliyo chini ya udhibiti wa Jeshi la Marekani.

Chanzo: Guardian US

guardian_us_237084384_4411980808844955_5805196802886511564_n.jpg
 
Back
Top Bottom