Afande wa bungeni!!!

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,168
8,142
Waungwana salaam!!
Kuna mahali nilikuta ubishi ambao kabla wala sikuwahi kufikiria endapo watu wangekuwa interested kufahamu hilo jambo!!! Ingawaje nami nilitamani kuchangia, lakini kiukweli sikuwa na hata ABC ya jambo lenyewe! Hivyo nimeamua kuja kuwauliza waungwana humu ndani manake hata nami nimejisikia kutaka kufahamu!! Hapa namzungumzia yule afande anayeonekana bungeni akipiga kwata na rungu lake kumsindikiza Speaker wa Bunge. MIongoni wa waliokuwa wanabishana, wapo waliokuwa wanasema kwamba yule afande ni afande wa polisi na pale yupo kama polisi tu.....yaani ni kama polisi anavyopelekwa kuwa kwenye msafara wa kiongozi wa nchi na yule wa bungeni anapelekwa pale kuhudumia bunge! Hata hivyo, kuna waliodai kuwa yule bwana ana-apply kibarua lakini sifa yake ni kwamba awe anatoka kwenye jeshi lolote hapa nchini. Na kama akipata, anaacha magwanda yake ya awali na kuwa mwajiriwa wa Bunge na sio tena mambo ya ndani! Natamani kujuwa ukweli ni upi kati ya hayo!! KUna mtu ambae anaweza kuwa na maelezo zaidi kuhusu mheshimiwa yule?! Manake kama vp na mimi nianze kuandaa CV yangu nikaidondoshe pale ili niwe mbeba rungu!!!
 
Yule mama ni askari Polisi tena b4 alikuwa trafk, bado ni muajiriwa wa Jeshi la Polisi kwan kpnd bunge hakuna utamkuta akiwa kazin kama kawa ila eneo lake la kazi ni bunge. The same applied kwa wale askali wa kiume nao ni askari wa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma
 
Mimi kuna siku moja nilimsikia yule mkuu wa kitengo cha ulinzi na usalama bungeni, simkumbuki jina, akihojiwa clouds alisema wale ni waajiriwa wa bunge na sifa mojawapo ni kwamba lazima awe amepitia mafunzo ya ulinzi na usalama, na huyo jamaa alisema yeye alikuwa ni polisi alivyoona tangazo akaapply na akapata nafasi hiyo, hivyo wale watu watu sio waajiriwa wa jeshi la polisi bali ni waajiriwa wa bunge.
 
imefika javini

YAANI bado nipo pale pale manake majibu yametoka kwa wadau wawili ambao majibu yao yametofautiana kwa 100% !! But very interesting, sehemu ambako nilikuta mada hiyo ikijadiliwa nako kulikuwa na majibu mawili sawa na haya ya wadau wa humu ndani!!!!!
 
YAANI bado nipo pale pale manake majibu yametoka kwa wadau wawili ambao majibu yao yametofautiana kwa 100% !! But very interesting, sehemu ambako nilikuta mada hiyo ikijadiliwa nako kulikuwa na majibu mawili sawa na haya ya wadau wa humu ndani!!!!!


Wale ni Askari Polisi,ni waajiriwa wa Jeshi la Polisi,kazi hiyo inafanywa na Polisi Pekee hii ni kutokana na nature ya majukumu yao.Bungeni wanakwenda kwa shughuli hiyo tu, kwa hiyo Bunge likiisha wanarejea kwenye kazi zao za Polisi kama kawaida. Ninachoona hapa mimi tatizo ni neno ajira,ukweli ni kuwa akiwa Bungeni Askari huyo analipwa Posho na Bunge.
 
Back
Top Bottom