Advance Physics ilivyokuwa inatugeuka ndani ya chumba cha mtihani

Acheni tu mazee katika maisha yangu ya shule sitakuja kuisahau advance ......tuliteseka kinoma hasa kwenye physics na chemistry maticha hao walikua nuksi wana sound kupita maelezo.........shule za serikali changamoto sana bila kupambana unakufa na tai shingoni......nakumbuka nililia sana kwenye necta practical ya physics mpaka wasimamizi wananiuliza dogo vipi mbona michozi mingi.......jamaa wametuwekea betri za jamaa walizokua wanatumia session 1 hazina nguvu kabisa

Adavance for me ilikua ni mate so bila chuki
 
Mechanics nili enjoy sana karibia vipati vyote isipokua projectile tu, kwa kuisoma kawaida ilikua inaenda ila maswali yake utajuta kuifahamu.

Topic nyingine ambayo sikuwahi isoma advance ilikua tism, ila nilijiwekea malengo kwamba swali lolote la atomic physics, heat, static na current electricity likija siliachi.
 
Physics sitaki hata kuikumbuka, Nakumbuka ilikuwa siku ya necta practical nimejiandaa na maswali yang ya mechanics, heat na current sababu tulijua vifaa alivyoambia mwalimu andae na maswali pia. Hapa nikiwa na uhakika wakupata sio chini ya 45 kati ya hamsini,
Ndani ya chumba cha mtihani vifaa vikawa ni vile vile lakn maswali hayaendani na vifaa mara msimamizi tunaona anafungua kibahasha anakuta instruction inabid aitwe mwl wa physics abadilishe vifaa, na Hapo muda unaenda, hiii siku ilikuwa ngumu sana katika kusoma kwangu physics nachokumbuka maswali mawili hata data nilishindwa kuchukua
 
Namkumbuka mwalimu wangu wa physics mwakanyamale alifanye nilipende sana somo hili, hakika alikuwa vzr sana
 
physics_650x400_51489484821.jpg


5aeb30138efc5bd38c3a8aacd40cc677--projectile-motion-the-motion.jpg


Wakuu japo sijapost kwenye jukwaa hili kwa miezi kadhaa sasa hivyo naomba mnipokee tena mtaalamu Deadbody ,

Wakuu najua JF kuna watu wa kila aina ya masomo humu hivyo leo naomba niwakusanye watu wote waliosoma Advanced Physics tuje tukumbushie namna tulivyokuwa tunashangaa ndani ya chumba cha mtihani .

Ngoja nianze mimi aisee kuleta ushuhuda wangu wa kwanza kabisa:

Story inaanzia pale tu kijana Deadbody niliporipoti Advance school mara ya kwanza aisee ambapo nikapokewa kwa furaha sana na watu niliosoma nao Olevel na Primary.

Walinipokea kwa mbembwe sana maana balaa langu walikuwa wanalijua vizuri kuwa Physics na Maths niliumbiwa mimi(hahaha sipo serious hapa).

Nikapokelewa na kuonyeshwa Block nitakaloishi na maisha ya boarding ndio yakaanza rasmi .

TOPIC YA KWANZA KUFUNDISHWA KWA SOMO LA PHYSICS

Kama ilivyomazoea ya shule za advance kuwa walimu hukimbilia kuanza projectile motion,measurements and error hivyo ikawa hivyo hivyo kwa mwwalimu wetu ambaye alikimbilia kuanza na PROJECTILE MOTION.

ProjectileMotion.jpg


Dah aisee nilishangaa sana kuona topic hiyo ikifundishwa ndani ya siku moja na kuisha yote huku ikiwa na formula nyepesi mno kwa mwanafunzi kilaza kama Jesca kuelewa.

Formulas zilikuwa za Range ,height ambapo kila nikigusa swali kwenye kitabu cha CHAND linaenda natia tiki ,nikaanza kujiuliza kwanini watu wanasema hii topic ngumu mbona nimesolve maswali yote aiseeee..

Dah nikahitimisha tu kwa kujiona mimi ndio mwamba ,mwamba wa mathematics na sikwami kabisa swali la PROJECTILE MOTION .Wakati najitamba hivyo kumbe washikaji wananichora tu kuwa huyu dogo kaja kwa mbwembwe tumtazame kwanza ataishia wapi.

Projectile+motion.jpg


Mwendo ukawa ndio ule ule muhuni nikigusa tu maswali ya examples ya mwalimu napasua tena kwa muda mfupi tu.Na kwa jinsi nilivyokuwa na mbwembwe ilikuwa mtu akiniletea swali la projectile naliweka kwenye calculator lote then nikipiga alama ya sawa sawa kitu imooooo.Wenzangu wakawa wananiambia dogo fanya moja moja kupunguza brackets maana zitakuchanganya,ila kwakuwa nataka kuonyesha mimi ni kichwa sichanganywi nikawabishia na kuweka lote.

Aiseee nilikuwa mpenda sifa hatari enzi hizo kushinda hata BASHITE,nikasema likizo hii watanikoma mchikichini huko ndio nitakuwa nasolvia watu kwenye mabanda ya mihogo wakati wa kusubiri pindi .

Dah maisha yanaenda kasi sana na hatimaye nikapewa habari njema na mwanangu mmoja hivi kuwa kwa mgote jumamosi ni mtihani wa PROJECTILE MOTION hivyo nenda kawaonyeshe aisee kuwa wewe ni mwamba Dar nzima.Nikajawa na sifa kama kawaida yangu na kuwaza mda wote kuwa jumamosi inachelewa aisee nikafanye maajabu mchikichini huko.

SIKU YA MTIHANI WA PROJECTILE MOTION IKAFIKA

projectile_motion_prob_2.png


Kwa kujiamini kabisa nikakaa seat ya mbele kabisa maana nilikuwa sitaki mtu anichungulie tusije tukagongana marks tukawa wote wa kwanza wakati mimi nimetumia nguvu kubwa sana na nimekamia show.

Sitasahau hii siku hasa pale nilipoufungua mtihani wa PROJECTILE MOTION na kukutana na Concepts mpya ambazo sijawahi hata kuhisi kama nazo ni projectile aisee.

Kusoma swali hata halina terminologies ngumu kuelewa ila isipokuwa sina cha kuandika baada ya kulielewa lile swali.Hahahah formulas zangu za RANGE na Maximum height zote hazitumiki na ndio nazitegemea sasa hapo.

Ule mtihani na mimi tulikuwa level tofauti kabisa ambapo ni sawa na mwanafunzi wa darasa la kwanza aliyejifunza hesabu za kujumlisha namba zenye tarakimu moja then umtolee hesabu za magazijuto.

Ule mtihani haukuwa standard yangu japo majirani zangu wanaagiza karatasi za kujibia tu baada ya kujaza za mwanzo.Muhuni natamani nisikusanye niondoke hivyo hivyo ila sasa Mgote anayesimamia mtihani ndio kakaa mbele yangu kiasi kwamba hata nikigeuza jicho tu ananiona ,hhahah noma.

Nikakutana na concepts za kitu kina kuwa projected kutoka kwenye gari linaloenda kwa speed fulani na kitu chenyewe kina speed yake aiseee.Wakati huo air unaambia inaspeed yake then natakiwa kutafuta umbali kitakapotua kutokea umbali ambao gari lilikuwepo wakati wa kurushwa.

material-YTA5u3DP.png


Kila nikiangalia naona nashindwa hata kuchora mstari wa range maana kitu kilirushwa kikiwa kwenye height fulani above the ground.

Kiukweli hilo ndio baadae nikaja kugundua lilikuwa swali rahisi kuliko mengine.Hayo mengine ilikuwa balaaa tupu maana hadi ndege wa angani waliokuwa wanatembea walipishana na hiko kitu walichokiproject tena kwa speed tofauti.

Mfano swali lingine lilikuwa linaanzia mbali kinouma kuwa ,ball imeenza kuserereka kwenye umbo lina shape ya U na kuibuka juu na kuendelea na projectile motion na mara gafla ukagongana na body nyingine huko juu hivyo nitafute velocity waliyogongana nayo halafu unapasuka then kipande kimoja kinaondoka kwa speed yake na kingine kwa speed yake (data zingine ziliwekwa)

Hapo ndio Deadbody nikanza kushtuka kuwa hata ndege na hewa zinaweza kutumika kwenye projectile motion kumbe.

curv_proj_ep2.png


Aisee nilijiona mweupe sana kichwani na hakukuwa na uwezekano wa mimi kupata 1/100 ule mtihani.

Nikasema isiwe shida,maana kukusanya pepa nyeupe ni aibu acha nijitoe ufahamu nitafute range na maximum height ambazo hazijaulizwa nitapate pa kuondokea nyumbani.

Utaratibu ulikuwa simple sana ,yani ukifanya mtihani week hii,majibu yanatoka week ijayo na sikurudi tena huko mpka dk hii napoandika mada hii sijui ule nilipata A au B na sitaki kujua.

NIKAANZA MAISHA MAPYA



Kama principle ilivyokuwa ,ukiona umeshindwa kushinda nao basi ungana nao.Nikaanza kusoma Physics upya mchikichini na nikagundua nilikuwa sijui chochote aisee maana hata circular motion ingeniumbua.
Dah ngoja niishie hapa aisee maana mzuka ukipanda nitaanza kutoa matusi humu kuhusu Newton Rings (Wave 2 ) na madude ya mule..

NAJUA WATU KAMA MIMI WAPO WENGI HUMU,NAOMBA LEO TUJARIBU KUKUMBUSHIA HUYU MNYAMA 'PHYSICS'

KARIBUNI

cart.gif
Hahaha mgote anatisha kwa maswali kila kitu anakuwekea maswali kigongo
 
Acheni tu mazee katika maisha yangu ya shule sitakuja kuisahau advance ......tuliteseka kinoma hasa kwenye physics na chemistry maticha hao walikua nuksi wana sound kupita maelezo.........shule za serikali changamoto sana bila kupambana unakufa na tai shingoni......nakumbuka nililia sana kwenye necta practical ya physics mpaka wasimamizi wananiuliza dogo vipi mbona michozi mingi.......jamaa wametuwekea betri za jamaa walizokua wanatumia session 1 hazina nguvu kabisa

Adavance for me ilikua ni mate so bila chuki
Daah mi ndo nasubiri selection
Nahitji kujua more thing kwa watu ambao munaexperience
Tsap:0715131307
Plz
 
Hahaha Daaah physics ni balaa Kuna T.O mmoja hivi alimaliza 2006 alikuja Kutufundisha sisi tukiwa form 6 tukajiona Vilaza Wote.. vitabu vya Chand...Roger. vyote tuliona Tumemaliza na Hakuna Swali Gumu.. Jamaa Halafu alikuwa ana dharau balaa na Chuo alifukuzwa Kisa Dharau kwa Maprofesa kwahiyo akabak anapiga Tuition mtaani tu na Sifa Kibao na Kuwaona Watanzania wote hawana Akili ila Yeye peke yake

Ila Nakumbuka Siku ya Mtihani wa Physics Nilipiga msuli Usiku halafu kesho yake Pepa Asubuhi Na Nikasolve Maswali Kama matatu hivi ya Chand kwenye Pepa Yamekuja Vile vile Nikasema Nashukuru Mungu Ndalichako kaniona

Ila Yote tisa nitarudi Shule Zote ila Siyo Advance
Kihombo huyo!
 
O level nilisoma engineering science, advance nikaona nisiiache physics, na chuo nikaenda kuipigia jiwe, ila heshima kwa physics bado inabaki pale pale
 
Paper ya physics nayokumbuka kuwa ilikua ngumu kwenye necta zote ilikua ya 2007,nilikua na solve paper zote za necta ila ya 2007 nilikua naiangalia tu, binafsi physics nilikua naipenda especially hyo projectile motion, maswali ya projectile motion yalikua hayakatiz kwangu ingawa kuna mengine unaweza solve week nzima ndo unapata soln,
Kusolve maswali ya projectile motion ilkua inahtaji akili ya ziada, ubunifu, pia uwe umesoma mechanics zote, ili uweze kucombine idea, ckupata A Necta ila mock na mitihani mingine ya kujipima nilikua nazipata,
 
Miaka ya 2011-2016 kuna kijana alikuwa pale Mwenge anaitwa Paul Dekka kwa Mtiga pale Mapambano alisoma Tabora Boys, watu walikuwa wanamsifia sana hadi nikashawishika kumpeleka kijana wangu pale.
Je ni kweli alikuwa vizuri na matokeo yake yalikuwaje advance hasa Physics?
 
Hahahahah shule yenyew O-level tulkuwa tunagonga Engineering Science badala ya Physics.....so ulikuwa ukichaguliwa Iyunga advance kama ulkotoka ulkuwa unabahatisha hakuna muujiza wa kutoboa.....ukigeuka kushoto unakutana na LE MUTUZ la Chemistry....Mr. SUDI.....***** mzee ana roho mbaya huyo.....kinyama.....

Umenkumbusha mbali sana kwa IYUNGA......

Hahahaha dogo umenikumbusha mbali sudy anaroho mbaya sana physics alikuwa yule jamaa ambae neno moja anarudia kwa dk 15
 
Achana na physics ya advance nyoko sitasahau pre national nlijisemea hii pepa na 86 tokeo lnatoka na 48 acha kabisa mungu mwema tu sikupata F wala E
 
Back
Top Bottom