Adhabu ya viboko mashuleni ifutwe; walimu wameshindwa kufuata Sheria ya utoaji wa adhabu

Fimbo ni kwaajili ya watoto wa kimaskini tu. Wanasiasa wanaoshadadia fimbo watoto wao wako English Medium hata hawapigwi bakora. Wakifokewa tu na mwalimu ni kesi kubwa. Hao tu wamejaa vyuoni na ndiyo hufaulu vizuri.
Fimbo zinajenga nidhamu ya uoga na inamfanya mtu kuogopa mamlaka, ijulikane kuwa jinsi mtu anavyoshirikiana na mamlaka inaimpact kubwa sana kwenye mafanikio yake maishani. Mbaya zaidi fimbo hazisaidii chochote zaidi ya kusababisha watu kuacha shule na kuongeza utoro.
Kwa hiyo mkuu una maanisha prof wote ni watu ambao hawakuwahi kuguswa na kiboko?

Unasema adhabu inayosababisha uoga (kama fimbo) inafanya mtu awe muoga kwa mamlaka na hatoshirikiana nayo. Vipi tufute adhabu zitolewazo na mahakama ikiwemo jela then wahalifu wawe wanapewa ushauri nasaha tu?
 
Mzazi nae pia ni mwalimu kwa mwanae.hivyo Mfunze mwanao adabu vyema ipasavyo nyumbani kwako ili aendako huko shule asipatwe na hayo majanga.Japo c jambo jema kuchapana mpk kufa au kuvunjika kiungo hivyo tusitizame upande mmoja badala yake kila mmoja ajihoji nakulifanyia kazi serikali,walimu,pamoja na wazazi kwamba kwa nn walimu wanafikia hatua hiyo?
kwa nn! mwanangu tuu kila siku?
Kwa nn! mtt wa fulani kila siku yeye tu?

sababu zinaweza zikawa

Moja,hampendi huyo mtoto

mbili,mtoto labda ana ulemavu wa akili

tatu,mwalimu hajui jinsi ya kudeal na huyo mtoto anayeonyesha challenging behaviour
 
mkuu umenikumbusha hata mimi kuna scul nilisoma meneja alikuja nakupokea malalamiko kutoka kwa wanafunzi kuwa tunachapwa sana na kiukweli tulikuwa tunachezea viboko, ss jamaa akawafokea sana walimu kwa hilo jambo,hatimaye wakaacha kuchapa week inayofuata meneja mwenyewe ndio alitandika watu makofi nakuwaomba walimu waendeleze utamaduni wao.
Yani watoto walikua hawafanyi usafi, makelele darasani, ukimtuma haendi, na mbaya zaidi wakamgomea aliyefuta adhabu siku moja. Ikabidi avirudishe tu, saivi mambo swafi shule imekua shule, mwendo wa viboko tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sababu zinaweza zikawa

Moja,hampendi huyo mtoto

mbili,mtoto labda ana ulemavu wa akili

tatu,mwalimu hajui jinsi ya kudeal na huyo mtoto anayeonyesha challenging behaviour
Sawa nimekuelewa vipi kuhusu mazingira ya huyu mwalimu hayawezi kuchangia kivyovyote vile?
 
Sawa nimekuelewa vipi kuhusu mazingira ya huyu mwalimu hayawezi kuchangia kivyovyote vile?

Ualimu ni kazi ngumu duniani,sio kwa Tanzania tu ila nadhani kuboresha maslahi ya walimu kutapunguza 'frastresheni' lol
 
Unaweza kuwa na hoja lakini hapa na wewe umevuka mipaka.
Je yalikuwa maamuzi ya walimu kuweka division five?
Point ya waalimu kuzuiliwa kuchapa itazalisha magenge
ya wahuni kuliko ilivyo sasa,nadhani ni muhimu wakuu wa
mashule waliopewa dhamana ya kutoa adhabu nao wawajibishwe
pindi inapogundulika wamesimisha madaraka yao kwa waalimu
wasiojielewa.Hiyo itaongeza nidhamu katika usimamizi.
Hata wewe huoni kwamba umevuka mipaka,


Mwalimu ukideal na magenge ya wahuni na polisi jamii ifanye kazi gani?

Hizi hoja zingine ni kuhalalisha uchapwaji na uvunjaji wa haki ya mtoto, unawaambia walimu wachape viboko kwa mujibu wa sheria, swali ni je nani atakae wachunga huko mashuleni kama wanazingatia sheria?

Haya mambo ya viboko yanahalalishwa na walimu wakuu wenyewe, embu jaribu kumuangalia huyo ticha mkuu wa Sperius anaongea bila hata hofu ya Mungu au ya yeye kuwa mzazi, inauma asee


#R.I.P Sperius

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwalimu kutoadhibu ni jambo linalowezekana kwa 100%
Fuatilia mwongozo huu: Mwalimu hakikisha umefika shule muda husika, simamia usafi na kama wanafunzi hawaonyeshi kushiriki kufanya usafi, tafadhali usishike kiboko. Mwalimu kumbuka muda wa vipindi ukifika hata kama mazingira ya shule ni machafu, wanafunzi waingie darasani tayari kwa masomo. Mwalimu fundisha kipindi chako kama mwongozo unavyoonesha, tafadhali usiwafuatilie wanafunzi wasioandika, kwani inaweza kuhamasisha hisia za kutoa adhabu ili kumjenga mwanafunzi husika. Mwalimu, daftari zikikusanywa kwa ajili ya kusahihisha, tafadhali usifuatilie kubaini wanafunzi wasiokusanya daftari kwani kubaini kwako kunaweza kupelekea kuwepo na mazingira yenye kuchochea adhabu.
Mwalimu wakati utakapoita majina, zingatia kuwa wale waliopo darasani kwa wakati huo ndiyo wanaokuhusu, hitaji lako la kutaka kujua mwanafunzi X ana tatizo gani la kutokuja shuleni linaweza kupelekea mazingira yatakayo chochea adhabu, kwani wanafunzi wenzie wakati mwingine watakupa jibu kuwa mwanafunzi X yupo maeneo ya chooni anacheza tu, hivyo jibu ili linaweza kupelekea mazingira ya adhabu. Mwalimu wangu, mara upatapo kesi za mwanafunzi X kuwa amepigana darasani au kutoa lugha chafu, tafadhali tumia neno moja tu kuwa "LUGHA ZA MATUSI SI NZURI " kisha mruhusu kurudi darasani ili kuepusha mazingira ya adhabu. Mwalimu wangu mzazi akikuletea kesi ya mtoto wake kuhusu tabia za nyumbani na hata mwenendo mbovu wa maendeleo yake darasani, tafadhali mueleze mzazi kuwa amalizane na mwanaye kwa namna inayofaa. Mwalimu wangu ukifuata muongozo huu, shutuma na jazba za wana wa nchi hii utaziepuka pia itakusaidia japo kurudisha mwili wako uliopukutika kwa kufuatilia watoto wasiokuhusu, nakutakia kazi njema mwalimu wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom