Adhabu ya viboko mashuleni ifutwe; walimu wameshindwa kufuata Sheria ya utoaji wa adhabu

Regnatus Cletus

JF-Expert Member
May 26, 2018
1,114
958
Pameshuhudiwa matumizi ya nguvu iliyozidi, adhabu za kutweza, na uchapaji wa viboko dhidi ya wanafunzi kwa namna ya kikatili, ya kuogofya, na isiyozingatia sheria.

Jana, tarehe 28/8/2018 Paliripotiwa mauaji ya Sperius Eradius yaliyofanywa na mwalimu kwa tuhuma batili za wizi wa mkoba.

Utoaji wa adhabu mashuleni unasimamiwa na SHERIA YA ELIMU, SURA YA 353, MAREJEO YA 2002, KIFUNGU NAMBARI 61 (1) (V) ; PAMOJA NA EDUCATION (CORPORAL PUNISHMENT) REGULATIONS G. N. 294 , 2002. (1) (2) (5).

MWANAFUNZI ATACHAPWA VIBOKO VISIVYOZIDI VINNE, NA MWENYE MAMLAKA YA KUCHAPA MWANAFUNZI NI MWALIMU MKUU TU, AU MWALIMU ATAKAYEPEWA MAMLAKA NA MWALIMU MKUU KUTOA ADHABU YA VIBOKO NA SI VINGINEVYO.

ADHABU ITATOLEWA ENDAPO TU PANA UTOVU MKUBWA SANA WA NIDHAMU, NA ADHABU HIYO ITAZINGATIA UMRI, JINSIA, NA HALI YA KIAFYA YA WANAFUNZI KISHA KUREKODI KATIKA KITABU IDADI YA VIBOKO, PAMOJA NA JINA LA MWANAFUNZI HUSIKA.

Kwasababu, inaonekana walimu wengi ni watu wasiojitambua, mamlaka yao ya kuchapa wanafunzi yafutwe kabisa.

Na kwasababu waalimu wakuu wamekuwa wazembe katika kusimamia utaratibu huu, nao wafutiwe mamlaka hayo.

Mwalimu mkuu asiwe na mamlaka ya kuchapa wala kukaimisha mamlaka ya kuchapa kwa mwalimu chini yake.

Mwalimu anaporarua wanafunzi kwa viboko awajibishwe kama muhalifu yoyote anayefanya SHAMBULIO LA MWILI DHIDI YA MWANAFUNZI (BATTERY).

WAALIMU WAMESHINDWA KUJIONGOZA NA KUGEUKA GENGE LA MIGAMBO WANAOTOA VIPIGO VYA KINYAMA PINDI WANAPOTAKA TU.

Ni walimu wachache sana waadilifu wanaozingatia uchapaji wa idadi ya viboko, na wengi wao wanatoa adhabu pasipo ruhusa ya waalimu wakuu.

Matokeo yake ni uchapaji wa kinyama, kutoa vilema, na kupoteza uhai wa wanafunzi wadogo ambao kimsingi wangepaswa kuelekezwa kwa upendo badala ya kushushiwa vipigo vya kikatili.

Wanafunzi watovu wa nidhamu wapewe adhabu za mikono. VIBOKO VIFUTWE.

Waalimu wameshindwa kutengeneza taifa la wasomi imara, badala yake wamegeuka kuwa genge la wachapaji na wauaji.

JUSTICE FOR SPERIUS ERADIUS.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fimbo ni kwaajili ya watoto wa kimaskini tu. Wanasiasa wanaoshadadia fimbo watoto wao wako English Medium hata hawapigwi bakora. Wakifokewa tu na mwalimu ni kesi kubwa. Hao tu wamejaa vyuoni na ndiyo hufaulu vizuri.
Fimbo zinajenga nidhamu ya uoga na inamfanya mtu kuogopa mamlaka, ijulikane kuwa jinsi mtu anavyoshirikiana na mamlaka inaimpact kubwa sana kwenye mafanikio yake maishani. Mbaya zaidi fimbo hazisaidii chochote zaidi ya kusababisha watu kuacha shule na kuongeza utoro.
 
Pameshuhudiwa matumizi ya nguvu iliyozidi, adhabu za kutweza, na uchapaji wa viboko dhidi ya wanafunzi kwa namna ya kikatili, ya kuogofya, na isiyozingatia sheria.

Jana, tarehe 28/8/2018 Paliripotiwa mauaji ya Sperius Eradius yaliyofanywa na mwalimu kwa tuhuma batili za wizi wa mkoba.

Utoaji wa adhabu mashuleni unasimamiwa na SHERIA YA ELIMU, SURA YA 353, MAREJEO YA 2002, KIFUNGU NAMBARI 61 (1) (V) ; PAMOJA NA EDUCATION (CORPORAL PUNISHMENT) REGULATIONS G. N. 294 , 2002. (1) (2) (5).

MWANAFUNZI ATACHAPWA VIBOKO VISIVYOZIDI VINNE, NA MWENYE MAMLAKA YA KUCHAPA MWANAFUNZI NI MWALIMU MKUU TU, AU MWALIMU ATAKAYEPEWA MAMLAKA NA MWALIMU MKUU KUTOA ADHABU YA VIBOKO NA SI VINGINEVYO.

ADHABU ITATOLEWA ENDAPO TU PANA UTOVU MKUBWA SANA WA NIDHAMU, NA ADHABU HIYO ITAZINGATIA UMRI, JINSIA, NA HALI YA KIAFYA YA WANAFUNZI KISHA KUREKODI KATIKA KITABU IDADI YA VIBOKO, PAMOJA NA JINA LA MWANAFUNZI HUSIKA.

Kwasababu, inaonekana walimu wengi ni watu wasiojitambua, mamlaka yao ya kuchapa wanafunzi yafutwe kabisa.

Na kwasababu waalimu wakuu wamekuwa wazembe katika kusimamia utaratibu huu, nao wafutiwe mamlaka hayo.

Mwalimu mkuu asiwe na mamlaka ya kuchapa wala kukaimisha mamlaka ya kuchapa kwa mwalimu chini yake.

Mwalimu anaporarua wanafunzi kwa viboko awajibishwe kama muhalifu yoyote anayefanya SHAMBULIO LA MWILI DHIDI YA MWANAFUNZI (BATTERY).

WAALIMU WAMESHINDWA KUJIONGOZA NA KUGEUKA GENGE LA MIGAMBO WANAOTOA VIPIGO VYA KINYAMA PINDI WANAPOTAKA TU.

Ni walimu wachache sana waadilifu wanaozingatia uchapaji wa idadi ya viboko, na wengi wao wanatoa adhabu pasipo ruhusa ya waalimu wakuu.

Matokeo yake ni uchapaji wa kinyama, kutoa vilema, na kupoteza uhai wa wanafunzi wadogo ambao kimsingi wangepaswa kuelekezwa kwa upendo badala ya kushushiwa marungu.

Wanafunzi watovu wa nidhamu wapewe adhabu za mikono. VIBOKO VIFUTWE.

Waalimu wameshindwa kutengeneza taifa la wasomi imara, badala yake wamegeuka kuwa genge la wachapaji na wauaji.

JUSTICE FOR SPERIUS ERADIUS.

Sent using Jamii Forums mobile app
Niki expand ubongo wako ni kama unasema "Ndoa zifutwe" kwa kuwa wanandoa wnasalitiana na zaidi sana wanauana kwa wivu wa kimapenzi!!
Una hasara kubwa kumiliki akili kwa mlinganyo na jimbi.
 
Kama hutaki mwanao apewe adhabu anapokosea mfundishe mwnywe.....hyo ya kijana kwa kweli nimepondeka sana moyo....ila siungi mkono viboko kutolewa mashuleni unadhani bila ya viboko ungekuja kutusumbua na mada yako hii...........ulikuwa zwazwa sema viboko vimekutoa uzwazwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Pigeni tu ila mtakwenda jela tu

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom