Pretty
JF-Expert Member
- Mar 19, 2009
- 2,575
- 553
Naungana nawe binhai,angalia sisi tulivyokuwa tunachapwa enzi zetu,na hapa tulipo sasa,viboko vinasaidia sana kwa watoto watukutu!!!
...........Fimbo muhimu jamani kwa watoto, haswa wale wenye umri mdogo.
Mie mwenyewe hadi kufika hapa fimbo zimenisaidia sana, nilivyokuwa mdogo nilikuwa mtundu mno baba alikuwa ananichapa na baada ya kunichapa ananiambia kwa nini amenichapa na niache kurudia hilo kosa.
Hivyo ni muhimu kuwaonya watoto kwa fimbo, samaki mkunje angali mbichi.
Kuna baadhi wazazi huwa wanakosea, mtoto anapokuwa mdogo haamchapi, ila akishakua mkubwa ndio hapo wanaanza kumpa viboko, mtoto ukija kumuonya kwa fimbo ukubwani huyu lazima atakuwa sugu tu.
Mithali 29:15A Fimbo na maonyo hutia hekima.