ACT Tanzania ni kama CCJ, nampa Zitto wiki mbili tu!

wakati chadema inaanza mihemko ya wiki mbili ilikuwa bado haijaanza au ! acha kutumia fikra za wengine, tumia zako, umetumwa sio bure.
 
Mtasubiri sana! ACT kuna vichwa si mapoyoyo mtasuburi mno hapa ni intellectuals wanaendesha chama na tunajua jinsi ya kuheshimu uhuru na mawazo ya watu..!

Saccos yenu itasambaratika mara tu baada ya uchaguzi mkuu october 2015 kwani hata diwani mtamkosa
 
Kwanza nianze kwa kukupa pole kaka yangu, uliyekuwa shujaa wa vijana wengi na Watanzania kwa ujumla(ni maoni yangu-dont take it personal) Zitto Zuber Kabwe, pole na matatizo yote yaliyokupata kisiasa tangu pale ulipo acha/ondolewa kuwa mmoja wa wateule wa Chadema, kiukweli ni mengi umeyapitia ambayo yanaweza kuwa yamekukomaza kisiasa (sina hakika kama yataendelea kukomaza-nitaeleza mwisho)
Zitto Zuber Kabwe,katika wanasiasa vijana sina uhakika kama kuna mwanasiasa kijana anayeweza kufikia record yako yakulitumikia taifa hili hasa linapokuja suala lenye masilahi kwa wananch,hata kama vingi havikufanikiwa lakini ulionyesha wapi unasimama...mfano mzuri ni Mabilioni ya Uswizi-Umeondoka na kiu ya Watanzania kutokututajia haswa ni nani wenye mabilioni hayo
Zitto Zuber Kabwe.

Si nia yangu kukuelezea ni mtu wa namna gani, lakini nataka nifikishe ujumbe huu kwako,mimi nilikuwa ni mmoja wa WAAMINI WAKO NAMBA MOJA, chochote ulichokisema nilikiamini kama neno litokalo kwa baba mchungaji, sikuwahi kuna na shaka nawe hata siku moja, sikuwahi kuwa na wasiwasi juu ya uwezo wako, uaminifu wako, utendaji wako hata siku moja, ndio maana nilazimika kukichukia chama chako cha zamani (CHADEMA) pale mlipoanza migongano..

Zitto Zuber Kabwe, nasikitika kusema NIMEFADHAISHWA SANA MOYONI MWANGU, umenikosesha amani sana,maana sasa nimekuelewa wewe ni mtu wa namana gani, kwa hakika naamini Watanzania wengi (hasa vijana) wamekuelewa kuwa wewe ni WANJANO na si MWEUSI kama walivyokuwa wanakujua, nashawishika kuamini na hakuna namna ambayo utanigeuza nikaamini vinginevyo kuwa wewe ZITTO ZUBERI KABWE NI MSALITI MKUBWA NA NI MTU MROHO WA MADARAKA na hilo ndio tatizo lako kubwa na chama chako cha CHADEMA, huna subira,huna uvumilivu,..

KITENDO CHA JANA KUJIUNGA RASMI NA CHAMA CHAKO CHA ACT-TANZANIA kimeniaminisha (kama sio kutuaminisha waaminini wako) kuwa kweli ACT -Tanzania ni chama chako ulichokiazisha toka zamani, maana haiwezekani jana tu ujiondoe rasmi CHADEMA na leo kujiunga na ACT - Tanzania?

Kwa maana tu ya kawaida haiwezekani leo umpe talaka mkeo na kesho uoe mke mwingine,,ni lazima huyo mke alikwepo toka zamani na umetoa talaka kwa mke wako kwaajili ya huyo hawala yako...

ZITTO, ACT-Tanzania ni kama hawala uliyeamua kumfanya mke,na tambua hawala ukimuoa siku zote huishi na wewe kwa tahadhari kubwa sana maana anajua kama uliweza saliti pale ni kipi kitakushinda kusaliti tena? hakika ndoa hiyo huwa ya mashaka milele,Zitto hao wana ACT wataishi nawe kwa mashaka siku zote,maana wengi wao wameamini kuwa ww ndio MM..

Naanza kuona mwisho wako wewe kufa na kuzimika kabisa kisiasa (Time will tell-Mfano wako mzuri ni ndugu Augustino Lyatonga Mlema)-umekosa washauri wazuri,umeshindwa fanya hesabu za siasa za UKAWA,ningekuwa mimi nakushauri ningekwambia upumzike kwa sasa mpaka pale utakapoona upepo wa UKAWA kama itakapofika karibu na uchaguzi wakishindwa kuendelea na MoU yao uhamie chama kimoja kati ya NCCR au CUF ili uendelee kutuamisha Waamini wako kuwa ww si mmoja waazisha ACT,wala hukutwa pamoja nao kile kikombe cha mkakati wa mabadiliko Chadema...

Nimalize kwa kusema neno langu si msahafu, yawezekana ukaja kutuonyesha upya kuwa wewe ni yule yule Zitto wa 2000-2010, lakini nikukumbushe tu kuwa umepoteza WAAMINI WAKO WENGI SANA,hivyo si rahisi kuwakusanya tena

Nikutakie safari njema huko uendako,kumbuka kusoma kile kitabu cha RISE AND FALL OF CCJ NA MPENDAZOE, pia nimalize kwa kusema ALIYEKUROGA ZITTO ZUBERI KABWE ashakufa na amezikwa Zamani,sio muda mrefu utakuwa kama yule muimaji wa bendi ya Tamu Tamu na Twanga Pepeta..amebadilishika kila aina ya music kutoka dance,taarab,rap, lakini ameshindwa fufuka na hatimaye ameishia kuwa mbeba mizigo (kuli)
Wasalaam
 
wakati chadema inaanza mihemko ya wiki mbili ilikuwa bado haijaanza au ! acha kutumia fikra za wengine, tumia zako, umetumwa sio bure.

Hakuna mwana cdm anatumwa,wanaotumwa ni machumia tumbo wa ccm na act na adc
 
Nami pia niliwahi shauri hivyo kwenye baadhi ya Post....ACT ni kachama kadogo sana sidhani ata km katadumu baada ya 2015 kwani kuna uwezekano mkubwa kakapata wabunge wawili au lah apo sasa wale uliowashawishi kwa mgongo wa maafisa usalama waliokutumia na akina Wasira ktk vikao vyenu watakapo tambua mchezo uliowaingiza kwa maslahi ya CCM...Ikumbukwe kwamba ifikapo chaguzi kuu CCM hua inakuja na mkakati dizaini hii kwakutumia watu km nyie....kila la kherikijana
 
uxi huu umetulia. waha wanasema yikuye umuvyuya nkamavyi. yeye ni muha anajua hii maana yake
 
Back
Top Bottom