Trust None
JF-Expert Member
- Feb 12, 2018
- 1,260
- 4,415
Kuna mambo yanayoendelea tangu utawala wa awamu ya tano uingie madarakani ambayo hayana afya kwa mtumishi wa umma. Viongozi wa vyama vya wafanyakazi wamekaa kimya, au nanyi wamewamangelize?
—Ajira hakuna mpaka watu wameanza kujinyonga...mpo kimya.
—Kupanda madaraja ajira mpya ya 2012, 2013 na 2014 hakuna... Mpo kimya.
—Kupanda madaraja kwa mara nyingine 2016, 2017 na 2018 hakuna... Mpo kimya.
—Nyongeza ya kila Julai hakuna... Mpo kimya.
—Kupandishwa vyeo kwa walioongeza elimu hakuna... Mpo kimya.
—Kupunguzwa kwa kikokotoo toka 75% hadi 25% mpo kimya.
Ni ukweli kuwa wote hawawezi kupata ajira za serikali lakini kama kodi zinakusanywa zaidi ya awamu zilizopita, hiyo pesa ni ya miundombinu tuuuuuu. Miradi hiyo hadi izae matunda serikali ipate hela za kuwajali watumishi ni zaidi ya miaka 20.
Watumishi hawataki SUPRISE, wekeni mambo wazi. Baada ya wapinzani kuibua hoja nyie mnakuja kusema eti mlikaa na serikali ila walikataa hoja zenu, ACHENI UONGO. Wakati serikali inakataa maoni yenu, mbona hamkusema?
Kazi kuongeza vyama eti CHAKAMWATA, wana nini jipya? Wanakomaa na kupunguza asilimia kutoka 2% hadi 1%, hawana msaada mwingine?
Fanyeni kama mlivyofanya septemba 2016 wakati wa sakata la fao la kujitoa.
Tamko la Pamoja kati ya vyama vya wafanyakazi na Asasi za Kiraia kuhusu Kuzuiwa Fao la Kujitoa - JamiiForums
Nini maana ya Serikali ya wanyonge?
Nini maana ya neno wanyonge? ( )
A: Watu dhaifu; wasiokuwa na nguvu, wenye tabia ya upole na ya kunyenyekea, watu wa hali ya chini.
B: Waue, watie kitanzi, walimie meno
TUCTA ni bora mkafuta sherehe za MEI MOSI 2019 ili pesa iliyotengwa itumike kuboresha MIUNDOMBINU ya vyama vya wafanyakazi, kuliko kwenda kwenye sherehe za kuwaongezea stress watumishi.