Acha maji yaende na maji

Dr criminal

JF-Expert Member
May 16, 2022
2,278
4,272
Hey there i'm using JF.

Niliwahi kupigisha tuition madogo miaka ya nyuma kidogo kukwepa kukaaa bila kazi na kupata hela ya vocha. Siku moja naingia darasani nikakuta kama kawaida ubao umechafuliwa kwa maneno, picha na sentensi nyingi zimeandikwa, moja ya sentensi iliandikwa hivi "Acha maji yaende na maji".

Sasa wakati napitia nyuzi kadha wa kadha humu ndani ndiyo huo msemo ukanijia kichwani. Watu wanatumia nguvu na hisia nyingi kupingana na ukweli, watu hawataki kuhama kifikra wakati tushahama kimaisha. Watu hawataki kukubali uhalisia, kuukabili, kuishi nao, kuutumikia, watu wanabishana na ukweli, mtu anaishi na uhalisia wa miaka 15 iliyopita.

Ndugu yangu acha maji yaende na maji, hamna kitu unaweza fanya ndugu yangu. Hakuna namna ya kumlinda mkeo asichakatwe uko nje, akiamua mwenyewe kufanya hivyo ilihali umetimiza kila hitaji kama mume. Leo hakuna uhakika wa mahusiano yaani leo wapenzi kesho mwenzako karudi kwa mpenzi wake. Aisee ni vurugu ndugu yangu, we acha maji yaende na maji.

Hii hapa mifano ya maisha yalivobadilika leo hii na hamna kitu unaweza fanya, utajitafutia matatizo we acha tu maji yaende na maji

1. Mke/Mume kuchepuka, ndugu yangu kama we ni mwanaume timiza majukum yako kama mwanaume halafu kausha. Namaanisha timiza kweli, show kali, quality time, malezi mazuri kwa watoto, mke na watoto wanakula vizuri, saidia ndugu zake kama una uwezo, mtengeneze mazingira yakujitegemea kama mwanamke halafu kausha.

Mke wako kama hana akili ndiyo basi hivo akili hana, wataenda nje watamla na hamna kitu unaweza fanya. Usimfatilie wewe maana yake shoga zake wengi ndiyo tabia zao na yeye ataliwa tu uko nje. Mwache ndugu, acha maji yaende na maji usijizeeshe, we achana naye.

Mwanamke huyo mumeo kama ye ni chitombi, umeisha, mama umeisha. Utampa mitindo yote ila bado ataenda uko nje kuwala. Achana naye, lea watoto mama hamna kitu unaweza fanya, hakuna we acha maji yaende na maji. Utakufa na presha bure watoto wabaki yatima bila mama huku nyuma.

2. Mwanume kulea mtoto siyo wako, kama mume usijipe stress kabisa kwenda kupima DNA sijui, achana nayo. We lea na wapende watoto wote uliowazaa na mkeo, wape mapenzi, lea viumbe vya Mungu atakuja akulipe mbele kwa mbele Mungu Baba Mwenyezi na mkeo atakuja alipe kwa dhambi hiyo. Achana naye, we lea tu acha maji yaende na maji.

3. Wanaume, pesa na mapenzi, mwanaume wa leo bila pesa hakuna penzi, nukta! Yani ipo hivyo, ndiyo tulipofkia hakuna kurudi nyuma tena. Wewe tafuta hela uwanase warembo, yaani bila hela hupendwi, nukta. Yaani we acha maji yaende na maji, kupingana na hilo utaishia kujichu. Tafuta hela uwavue chupi, nukta.

4. Baadae mnaachana, hii ikae akilin hii "Dakika yeyote kutoka sasa tunaachana" (wapenzi ni sana lakini siyo wanandoa) ndiyo tulipofkia hapo. Yaani hakuna kitu utafanya kubadili hilo, siku hizi hatupendani ndugu zangu hata kidogo, kwahiyo ukimpenda mtu ujue mda wowote kutoka sasa mnaachana. iko hivyo. Iweke akilin na uishi nayo vinginevyo utakuwa unalialia Kila siku, we unga tela tu acha maji yaende na maji. We penda ukitendwa unaunga kupenda mwingine, yaani hakuna mda wa kupoteza maisha mafupi haya.

5. Wanawake kunuswa na kuachwa, ndiyo tulipofkia hapo hamna kitu unaweza fanya hata uwe wife material vipi, asilimia 90% ya wanaume wanaokusumbua wanataka kunusa tu halafu wapite hivi. Sasa jifanye unajua sana kupenda waufanyie upasuaji huo moyo, kwahiyo we acha maji yaende na maji, kubali kunuswa ila jiandae kutendwa.

6. Kubambikizwa na kudhulumiwa mimba, kama mwanaume we ni chitombi halafu huwa unaenda kavu, hapa namaanisha chitombi kweli basi umeshawahi kusingiziwa au kudhulumiwa angalau mimba moja halafu fuleshi tu maisha yanasonga na hamna kitu unaweza fanya, hakuna. Acha maji yaende na maji, ukiletewa mimba lea, ukizulumiwa watalea uko wengine.

Ndugu zangu mambo ni mengi sana, na maisha yamebadirika sana kwahiyo na wewe jaribu kubadirika. Hizi kesi za kuuwana kisa mapenzi, kujiua kisa mapenzi, sijui kupeana vichapo kisa mapenzi, sijui unakuja humu mwanaume unalia umeombwa pesa nyingi na mwanamke acheni. Ndiyo maisha yapo hivo sasa hivi, ndiyo tulipofkia ndugu zangu, we acha maji yaende na maji. Unga tela wewe twende, muda wenyewe uko wapi ndugu yangu, aah?

#OneDayYouWillBeGone
Dr criminal

Sent using Jamii Forums mobile app
 
iyo michezo ya kuibia wake za watu mfanyage Kwa mapopoma siku mtaja ingia Kweny jamii ambazo wanaume wanaweka password Kwa wake zao ukigusa tu mke wa mtu jua kabisa safari Yako imeiva tukutane siku ya kuimba mapambio Kwa sir God vijana acheni masihara na Mali za watu Kuna binadamu hawanaga mzaa kweny Mali zao kosa moja shughuli Yako kwisha.
 
iyo michezo ya kuibia wake za watu mfanyage Kwa mapopoma siku mtaja ingia Kweny jamii ambazo wanaume wanaweka password Kwa wake zao ukigusa tu mke wa mtu jua kabisa safari Yako imeiva tukutane siku ya kuimba mapambio Kwa sir God vijana acheni masihara na Mali za watu Kuna binadamu hawanaga mzaa kweny Mali zao kosa moja shughuli Yako kwisha.
Mwekee password binti uliye mzaha sasa mtoto wa watu huyo siku yeyote mnaweza kutengana ma password ya nn(kidding)

Ukwel ndo huo huna sabab ya kumfata mke mtu lakini tulipo saizi hicho ni kitu Cha kawaida sanaaa kwahiyo achaa maji yaende na maji, midawa hiyo sijui minini unapoteza mdaaaaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom