Abdul the crook!

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Siku moja abdul alienda kuazima sufuria kubwa kwa jirani yake.Alipokaa nalo wiki moja,alilirudisha huku akiliambatanisha na kijisufuria kidogo.Jirani alipohoji imekuwaje aliazima sufuria moja na leo anarudisha mawili,abdul akajibu,'sufuria kubwa limezaa mtoto'.Yule jirani alipokea masufuria yote kwa furaha.Siku nyingine abdul aliazima lile sufuria kubwa.Baada ya wiki kupita,abdul alienda kwa jirani mikono mitupu huku akilia kwa uchungu.Jirani alipohoji kulikoni?abdul akajibu,'sufuria lako limefariki,tumezika jana!'.Yule jirani akang'aka huku akisema,'sufuria sio kiumbe hai,haliwezi kufa',abdul naye akamjibu,'kama liliweza kuzaa mtoto na ukakubali,kwa nini leo ukatae kwamba limekufa'?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom