A way forward: Mtazamo wangu juu ya Elimu ya sekondari ya juu(A-Level) na Elimu ya ufundi(VETA)

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Kipekee kabisa nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya siku nyingine mpya katika maisha yetu. Pia, nichukue nafasi hii kumpongeza Katibu mkuu wa CCM Ndg. Daniel Chongolo kwa ushauri aliotoa juu ya wahitimu kwenda VETA kupata ujuzi wa kujiajiri. Ni ushauri mzuri na wenye kutoa picha kubwa ya ulimwengu tulionao na tunaouelekea kuhusu kujiajiri. Ushauri wa Chongolo umeangaliwa kwa mtazamo tofauti na baadhi wameuona kama ni dharau kwa wahitimu.

Mimi binafsi, ushauri wa Chongolo nimeuona Kama ni muarobaini wa tatizo ajira. Kujiajiri ni fursa ya kufikia malengo yako ya kitaalamu kwa taaluma uliyonayo na ujuzi wa kujiajira unapatikana VETA. Unapojiajiri inakuwa ni fursa ya kutumia taaluma yako mbeleni kwa sababu ukipata mtaji unaweza kujenga ofisi ya kuendeleza taaluma yako.

Nina mtazamo juu ya Elimu ya sekondari ya juu(A-Level) na Elimu ya VETA.

Ninaona ni vema Elimu ya VETA ifundishwe kwa wanafunzi wa sekondari ya juu na masomo ya sekondari ya juu yapunguzwe kutoka matatu yaliyopo sasa mpaka kufikia mawili. Mtazamo huu ni kutokana na hoja zifuatazo:

i) Kuna ulinganifu fulani katika Elimu ya sekondari ya juu na Elimu ya Diploma kwa maana ya kwamba wote wanakuwa na sifa sawa zilizo sawa za kudahiliwa kwa masomo ya Elimu ya juu. Licha ya ulingano huo kuna tofauti kubwa sana kati ya mhitimu wa Diploma na wa sekondari ya juu kwenye soko la ajira. Mwanafunzi wa Diploma ana ajirika lakini wa kidato Cha sita haajiriki. Kwa nini?

Ikitokea mwanafunzi wa kidato Cha sita kashindwa kuendelea masomo kutokana na sababu yoyote ile kwenye mfumo wa soko la ajira hatambuliki. Kwa nini?

ii) Masomo ya sekondari ya juu yamewekwa katika msingi wa masomo matatu lakini nini matokeo yake mbeleni, katika kuchagua 'course' ya kusomea Chuo Mara nyingi inahusisha masomo mawili na hata wakati wa kuchagua vyuo sharti huwa ni walau awe amefaulu masomo mawili na hapa tunaona kuna somo analisoma lakini haliji kutumika mbeleni. Kwa nini combination kwa elimu ya sekondari ya juu isiwe na masomo mawili tu na nafasi ya somo la tatu ikafundishwa Elimu ya VETA ili kumpa mwanafunzi wa sekondari ya juu ulingano katika soko la ajira baada ya kuhitimu?

A way forward:

Masomo ya sekondari ya juu yapunguzwe kutoka matatu yaliyopo sasa katika ' combination' na yawe mawili na nafasi ya somo litakalopunguzwa ifundishwe VETA.

Wahitimu wa sekondari ya juu wawezeshwe kwa mafunzo ya VETA ili kuwajengea uwezo ulio sawa kama wa wale wa Diploma sio tu katika kudahiliwa katika vyuo vikuu na masomo ya Elimu ya juu bali katika kuajirika.

Huu ndio mtazamo wangu katika kuiongezea thamani Elimu ya sekondari ya juu katika soko la ajira.

Jambo hili litasaidia kuzalisha wasomi ' competent ' wengi kwa maana ya kwamba wanafunzi wanaohitimu kidato Cha sita wanakuwa hawana sifa zozote hata za kujiajiri. Hivyo katika kukazia ushauri wa Ndg.Chongolo katika kukazia Elimu ya VETA kwa wahitimu ninaona tuanze na kundi hili la wasomi wasioajirika.

Ni Mimi Karlo Mwilapwa
0715-804-2548
 
Back
Top Bottom