A Nexus of a Strike: Kinachogombaniwa na madaktari ni jambo kubwa zaidi - tutawaliwe vipi?

Bilabaye, umma gani unaouzungumzia?. Sisi sio kama waMisri, waTunisia au Walibya!. Sisi ni watulivu, watu wa amani, wanyenyekevu na watiifu kwa serikali yetu!.

That's what wazee wa posho thought! Kumbe the missing link ilikuwa kiberiti tu. Madaktari wamewasha, serikali haonekani kuwa interested hata kujua fire extinguishers zipo ama la. Na wanavyozidi kujivuta (serikali) ndiyo moto unazidi kukulea.

Pasco mtoto wa mkulima alitoa masaa 48, tena akiwa kwenye kiyoyozi ukumbi wa Karimjee, what happened? Kashia kupiga mguu Muhimbili chini ya feni. Next time atawatafuta madaktari chini ya mwembe!
 
Kama kuna kosa la kihistoria linaloweza kufanywa na JK ni kuwa mkali zaidi na kutishia au kuamua kuwafukuza madaktari; itamjengea sifa kwa mashabiki wake lakini itamuonesha udhaifu wake! Yaani, yuko tayari kuwafukuza madaktari maelfu kwa madai yao ya kutaka uwajibikaji na kushindwa kuwatimua watendaji wawili kwa kushindwa kuwajibika!
 
Madaktari bahati mbaya sana hawana hoja isipokuwa wameamua kutumia human shield kuweza kupewa madai yao hivyo hawana tofauti na magaidi

Madaktari wanaweza kuamua kuacha kazi serikali na kwenda kuajiriwa kwenye hospitali binafsi kama maslahi na mazingira wanayopewa na muajiri hawayafurahi (soko huru). zaidi wanaweza kuanzisha hosptiali zao wakalipana if possible

Madaktari wanakosa nini waziri/naibu asipofukuzwa? na wanapata nini wakifukuzwa NONE

Madaktari wanaingilia kazi za kikatiba za Rais..je wao wanataka waziri wao awe ulimboka??? wtf

Bahati huyu JK hajui maana ya Mamlaka laiti angenipa mimi wangenikoma aisee..lol
 
Mwanakijiji,
Nikuulize huyo Mponda na Nkya wamekosea vitu gani haswa hadi watakiwe kujizuru?. Halafu hoja ya madaktari sio ya wananchi.. ni yao wao waajiriwa na ndio maana wako radhi wagonjwa wafe ili wapate wanachokidai. Ingelikuwa ni nafsi zao hatarini ya kifo wala wasingefanya maamuzi hayo kwa sababu ambazo kila kukicha zinabadilika.
 
Madaktari bahati mbaya sana hawana hoja isipokuwa wameamua kutumia human shield kuweza kupewa madai yao hivyo hawana tofauti na magaidi

Unapokuwa vitani inafikia kipindi utatakiwa kutumia silaha yeyote ili mradi umshinde adui yako, hasa adui anapokuwa anatumia uwongo, propaganda, usaliti nk. Serikali ni wasaliti, kwani hatukumsikia Pinda akiahidi kuwafukuza hao mawaziri ndani ya wiki mbili?

Madaktari wanaweza kuamua kuacha kazi serikali na kwenda kuajiriwa kwenye hospitali binafsi kama maslahi na mazingira wanayopewa na muajiri hawayafurahi (soko huru). zaidi wanaweza kuanzisha hosptiali zao wakalipana if possible

Hizo ndizo fikra potofu za kikabaila mlizonazo nyie watawala. Ndio maana na nyie mmejikita kwenye biashara za mahospitali ( refer Blandina na Uhusiano wa Linda wa muhimbili), na ndio maana mnataka hospital za serikali zife ili biashara zenu ziendelee. Je biashara ya Apollo hamuoni kuwatosha? Madaktari wamewang'amua ndio maana mnawapiga vita na propaganda zenu. Mnataka muwakatishe tamaa ili wakimbie nchi na watanzania wa kawaida wafe mbaki nyie wenyewe. Tutawapigania madaktari mpaka uozo wenu ujulikane. Tutaandaa documentary kufichua madudu yenu, na mtatushangaa.
Madaktari wanakosa nini waziri/naibu asipofukuzwa? na wanapata nini wakifukuzwa NONE

Wanakosa ushirikiano wa viongozi ambao walitakiwa kuboresha huduma za afya. Adala yake ni kuzididimiza. Wamewekwa kama chambo kazi kusaini cheki za kupeleka watu nje mpaka wizara imefilisika na wananchi wa kawaida hawana hata gloves. Shame on them, they are incopitent so they should go!!
Madaktari wanaingilia kazi za kikatiba za Rais..je wao wanataka waziri wao awe ulimboka??? wtf

Kama raisi anawaweka mabest zake ambao ni vilaza kwa nini wananchi wasiwakatae? Kwani wao ni nani? Yaani bila wao hiyo wizara haiwezi kufanya kazi? Rais kaajiriwa na nani mpaka asiwasikilize waajiri wake? Mnapambana na kizazi kingine si kile cha ndio mzee tu!

Bahati huyu JK hajui maana ya Mamlaka laiti angenipa mimi wangenikoma aisee..lol
Unajidai huna mamlaka wakati unayo na unajua kabisa huwezi yatumia! Tehe usinichekeshe mie!! Zinduka, halafu acha kujificha nyuma ya pazia. Kesho ni kesho, its now or never!!
 
Unajidai huna mamlaka wakati unayo na unajua kabisa huwezi yatumia! Tehe usinichekeshe mie!! Zinduka, halafu acha kujificha nyuma ya pazia. Kesho ni kesho, its now or never!!

Aisee ningekuwa na mamlaka hao madrs at least ningewashikisha adabu .mxxxxnina zao
 
Je kuna chochote kinachofanyika kuepusha utawala kama huu usijetokea tena, au tutaendana na utawala mwingine(utakaokuja) unaoweza kuwa mbaya zaidi? Sisi wananchi wa kawaida tunafanya nini zaidi ya kusubiri uchaguzi mwingine na kupiga kura bila kujua vilivyomo vichwani mwa watakaopata nafasi za kugombea uongozi?
 
Mzee Mwanakijiji, hata mimi ndio ningekuwa Kikwete, I'll would never bow down to pressure ya madaktari kumtimua Dr. Mponda na Dr. Nkya ili kuepuka kuweka precedence ya weakness dhidi ya undue pressure!. Yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu, sasa itakuwaje apokee amri kutoka kungine?. Akitekekeza hii amri ya madaktari, itafuatia amri ya walimu, then amri ya polisi, then amri ya wafanyakazi wa serikali na mwishowe amri ya wananchi na sisi kujitengenezea Taharir Squire yetu!. Sasa ndicho kitafanyika kile nilichosema ule mgomo wa mwanzo!. Kwenye thread yangu ya mazuri JK nimemsifu ni mtu mwenye upendo na watu na mwenye kukumbuka fadhila yaani appreciative person wote waliomsaidia amewakumbuka. Kwa vile Dr. Mponda ni chaguo lake binafsi, you never know walitoka nae wapi?. Hata Mama Nyoni na Jairo wanasubiri kwenda ubalozini!. Katika thread ya mapungufu ya JK nimesema JK ana upendo na huruma iliyopitiliza hivyo kugeuka weakness!, kama aliweza kuyasamehe majizi ya EPA kwa kuyahurumia tuu, kwa nini amwadhibu Mponda na Nkya?!. Itakuwa ni kuwaonea bure!. Madaktari kama wanagoma tena, na wagome tuu, watu kama watakufa na wafe tuu!, but this time cha moto watakiona na belive me someone must be held accountable!.
...Mmh, haya.
 
Pasco,

Umeandika vizuri sana ila unakosea kitu kimoja.

Nilikuwa nafuatilia habari za wizara kama hiyo ya afya nchi fulani ambapo Waziri wa afya mwishoni mwa mwaka, aliweka madudu fulani mapya na madokta wenzake (Maana na yeye ni Dokta) wakamgomea na kutishia kufanya mgomo baridi kwa kutokujaza baadhi ya information kwenye risiti za dawa jambo ambalo ingelibidi Wizara ya afya ndiyo ijaze.

Ila kwa sababu wenzetu Serikali ipo sensitive sana kwa masuala kama hayo, kabla mwaka haujakamilika, walilijadili na kulirekebisha haraka sana na mwaka umeisha, kukawa kuna mabadiliko. Baadhi ya vitu viliendelea kubadilishwa huku mwaka ukiwa umeanza ila walau Madokta walishaanza kuona kuwa Waziri wa afya yupo tayari kuongea nao.

Tanzania waliliachaniza hili kwa kuanzia akina mama Nyoni kuongea uozo kwa madokta. Swala likafikam wizarani na huko wakitegemea kuwa watalifanyia kazi, Waziri na naibu wake wakajibu utumbo. Hapo usalama wa taifa na Serikali kwa ujumla wamelala. Ilitakiwa Waziri Mkuu alichukue haraka sana swala na kuanza kulisolve ila ikawa zii. Wakatoa Onyo kuwa watagoma, wakajibiwa "Wenzenu waalimu walitishia wakaufyata, na nyie jaribuni tu mtakiona."

Madokta Wakajaribu, wakathubutu na wakasonga mbele kwa siku kadhaa hadi Pinda akaja kuzima moto. Rais na PM walikuwa baado na muda kuja kulisolve hili swala kwa kuziweka pande zote mbele na kuwapa onyo wote waache kutuniana misuli. Wao wakawa wanasubiri siku ziishe kwa kujificha kichwa kwenye mchanga kama mbuni. Sasa siku zimeisha na hawana la kusema na lawama wanaanza kuzisukumia kwa Madokta. Hakuna hata mmoja aliyethubutu kuingilia kati hili tatizo na sasa wanaanza vitisho.
Mie nafikiri Serikali haina pesa na hawajui la kufanyana sasa wanatoa vitisho ili wapate pa kutokea.

Mwisho Pasco, hakuna taifa gumu na hasa Rais wake ku-Bow kwa mtu kama USA. Hawa watu au watatumia maguvu kuliko kuongea kwa kaswala kadogo. Cuba ni mfano mdogo wa hilo tatizo kwani wangeliweza kabisa kulimaliza siku nyingi ila ubishi wao tu. Ila hili ni kwa mambo ya nje kama Cuba, Iran nk na pia mambo ya terrorism.

Ila kuna lile swala la POLISI (Mweupe) aliyemkamata Professor (Mweusi) aliyekuwa anaingia nyumbani kwake. Yule polisi aliwagomea wote kuomba msamaha na swala likaanza kuchukua sura mbaya sana. Obama kama Rais angeliweza kabisa kumuondoa maisha Prof. au Polisi ili kumaliza ubishi ila hakufanya hivyo. Aliwaita kwake, wakakaa na kuongea kama watu wazima huku wakipata Ze Bia. Swala liliisha kimyakimya bila mtu kuficha uso.
Tatizo letu sisi tumezoea "kijana, utanitambua mimi ni Mwalimu wako......" Kitu kidogo badala ya kutumia busara kidogo sana kukimaliza, tunaamini ni maguvu tu yataweza kila kitu. Haya sasa vitisho vinaanza. Haki ya nani, manesi kesho wataanza mgomo pia na Waalimu watafuata. Polisi na Wanajeshi? Labda wao pesa zitaendelea kuwepo ila hao watu wa TRA kama wanafiwa na ndugu zao, watafanya Sabotage ambayo haijawahi kutokea Tanzania.

Mdharau mwiba..... Usaha huooooo.

0730_beer-summit-600.jpg
 
Back
Top Bottom