6 Septemba 2023 hali ni Tete Wilaya ya Kyela

Ikiwa ni siku 3 kupita tangu waziri mwenye dhamana kuwahadaa wananchi kuwa Tanzania kunamafuta ya kutosheleza.

Ikiwa ni siku 2 kabla ya mwenge wa uhuru kumulika wilaya ya kyela.

Naomba kutoa taarifa juu ya kinachoendelea kyela

1. Zaidi ya wiki mbili sasa mji wa kyela hauna umeme.

2. Ni siku ya tatu mji wa kyela hauna mafuta.

  • mafuta leo yamefuatwa mbeya na tukuyu mabaharia wanajipanga kufuata Malawi. Wauzaji holela wameuza bei ya shilling elf 5 kwa lita Asubuhi na jioni hii wamejiuzia sh elf nane hadi 10 Hatujui kesho
  • Boda Boda nyingi zimepaki. Umbali ulio kuwa ukilipa buku kwa boda boda leo imefika sh 3000.
  • ukosefu wa magari umesababisha watu washindwe kufika misibani.

NB; nisiwe mbali na wale chawa wanao muunga mkono mama. Hakika anakubalika huku Kyela. Mitano tena! Anaupiga mwingi!!!
NB; nisiwe mbali na wale chawa wanao muunga mkono mama. Hakika anakubalika huku Kyela. Mitano tena! Anaupiga mwingi!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom