50 Cent Ajitabiria Kifo Chake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
50 Cent Ajitabiria Kifo Chake

6175386.jpg

50 Cent
Sunday, January 08, 2012 9:22 PM
Msanii mkongwe katika anga ya muziki wa Hip Hop, 50 Cent amejitabiria kuwa hana muda mrefu duniani na kifo chake kipo karibuni.
Albamu yake ya kwanza iliitwa "Get Rich or Die Tryin" lakini pamoja na kuupata huo utajiri aliokuwa akiupigania, 50 Cent hana furaha na anafikiria kuwa kaburi linamjongea.

Nyota huyo wa Hip Hop ambaye jina lake halisi ni Curtis James Jackson III, aliweka ujumbe mara kadhaa kwenye tovuti ya Twitter akisema kuwa ana uhakika hana muda mrefu duniani.

"Kwa kusema kweli sifikirii kama nitaishi muda mrefu", alisema 50 Cent katika ujumbe aliourusha kwenye Twitter.

50 Cent ambaye ana umri wa miaka 36 aliendelea na kusisitiza kuwa itakuwa vizuri kama atafariki usiku wa leo.

Ujumbe huo umefuatia vijembe ambavyo 50 Cent amekuwa akirushiana na studio iliyokuwa ikirekodi albamu zake ya Interscope ambayo imemtema 50 Cent.

"Muziki ulikuwa ndio burudani yangu lakini hivi sasa siasa imeingia kwenye muziki kitu kinachonikera", alisema 50 Cent.

"Sijavunjika moyo lakini naamini hivi sivyo ambavyo ningetaka nikumbukwe".

50 Cent aliendelea kusema kuwa hivi sasa yuko bize kumalizia albamu yake na baadae atajishughulisha na filamu ambayo ameshirikishwa.



Ana matatizo ya
matatizo ya kisaikolojia! inaonyesha hivyo hahahahahah peas zikiwa nyingi zinakutia wendawazimu.​

 
atadanji kiukweli ye analeta masihala,bt huenda kifo chake kinanukia...
 
hivi kwanini asife kimziki wakati anabifu na wasanii wengi kama
Ja-rule
Dj Khaled
Nelly
Rick Ross
The Game
e.t.c

ila nadhani labda anazungumzia kifo kisanaa
 
hivi kwanini asife kimziki wakati anabifu na wasanii wengi kama
Ja-rule
Dj Khaled
Nelly
Rick Ross
The Game
e.t.c

ila nadhani labda anazungumzia kifo kisanaa

Ni kifo cha kweli. Anajitanguliza aonekane kidume, lakini kiukweli vitisho vya kumuondosha kutoka kwa mahasimu wake vimeongeza sana.
 
Naona ataishi muda mrefu sana huyu jamaa! Alishakoswakoswa na risasi zaidi ya mara 100 lakini bado anadunda.
 
wana jf nmependa sn post zenu zmenifurahisha wajameni ah ha ha ha ha..
 
Ni kifo cha kweli. Anajitanguliza aonekane kidume, lakini kiukweli vitisho vya kumuondosha kutoka kwa mahasimu wake vimeongeza sana.
kuna video moja Rick Ross na kundi la Tripple C wanamwambia watammaliza.,kina Gun player,Jamaa amekuwa na bifu za kijinga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom