ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
Samsung Galaxy S4 ndio simu ya kwanza kuwa na prosesa aina ya Exynos 5 yenye core 8 (Octa), ambayo ndio prosesa yenye nguvu kuliko zote katika soko la simu kwa sasa, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na jarida pamoja na mtandao wa teknolojia T3 ni asilimia 30 tu ya simu hizo ndio zitakuwa na prosesa hyo, na ni simu ambazo zitauzwa kwenye soko la UK, Marekani walishahakikishiwa kwamba Galaxy S4 za bara la Amerika ya Kaskazini zitakuwa na prosesa aina ya Snapdragon yenye kasi ya 1.9 GHz na core nne.
Samsung wanakhofia kwamba hawana muda wa kutosha wa kuzalisha aina hiyo ya prosesa na mauzo ya wapinzani kama vile HTC One na Sony Xperia Z yanapamba moto, hivyo ili kuongeza kasi ya uzalishaji Samsung watatumia prosesa za Snapdragon kwenye 70% ya simu hizo, zikiwemo pia zile zitakazouzwa mabara ya Ulaya na Asia.
Wadau wengi wanapata hisia kwamba Samsung wametoa tangazo la kutumia prosesa ya core 8 ikiwa kama ni sehemu ya kivutio cha mauzo ya simu yao, wakati mpango wao tangu awali si kutoa simu nyingi zikiwa na prosesa zenye core nne. Soko la Uingereza ni soko linalolipa sana hivyo Samsung wanamudu kutoa simu za gharama kubwa katika nchi hiyo. Kwa kawaida wengi kati ya wanaonunua simu za hali ya juu Uingereza hununua kwa njia ya mkataba, ambapo simu kama Galaxy S4 hutolewa bure iwapo mteja atakubali kulipa zaidi ya £30 kwa 3G au hata maradufu ya hizo kwa EE yenye huduma ya 4G kwa mwezi mmoja tu kwa muda wa miaka miwili.
Mteja huyo atanufaika kwa kuzungumza dakika kama baina ya 1000 au zaidi katika mtandao wowote, message mpaka ashindwe mwenyewe na data kwa ajili ya internet pia hazina kikomo kwa upande wa 3G ambapo 4G hupewa 8GB au pungufu kwa kila mwezi. Kampuni ya EE ambayo ni pekee ambayo inatoa huduma ya 4G nchini UK kwa sasa wameshatoa tangazo la simu ya Samsung S4 ambapo wateja watakao toa oda sasa hivi watailipia simu hiyo £79, mkataba wa miaka 2 na watapata vifaa (accessories) zenye thamani ya £54, mkataba ni miaka miwili kwa £41 kwa mwezi.
Wateja hao wataruhusiwa kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi pasipo na kikomo lakini data itaishia 1GB kwa mwezi. Hivyo mkataba huu si kwa ajili ya wenye kutmia intaneti zaidi, na hivyo faida halisi ya kutumia 4G haipo, lakini huu ni mtego kwani watakapopiliza kiwango cha data walichopewa basi watalazimika kulipia ziada ya data walizozitumia.
Hivyo bila ya shaka Samsung wanaelewa kuwa UK ni soko lenye faida kubwa ndio maana huko wanapeleka simu zenye core nane na masoko mengine ni core nne za kawaida huku wakijivunia kuwa ni simu yenye prosesa yenye kasi zaidi kama kwamba zote zina prosesa hiyo. Biashara inahitaji ujanja.
Kiutendaji tofauti baina aina mbili hizi za prosesa ni vigumu kuigundua kwa upande wa kasi au ufanisi, lakini kwa upande wa betri Exynos 5 yenye core nane inasadikiwa kuwa na ufanisi mkubwa kutokana na prosesa hiyo kuweza kutumia core zinazohitajika tu kwa aina mbali mbali za matumizi. Hii kinyume na matarajio ya kawaida ambapo ongezeko la core kimantiki ilikuwa iwe inakula betri zaidi. Hivyo ni matarajio kuwa watakaokuwa na SAmsung Galaxy S4 yenye Exynos 5 ya core nane hawatakuwa na matatizo ya kuishiwa betri kwa haraka ukilinganisha na wale watakaokuwa na S4 zenye Snapdragon.
CHANZO: http://www.gajetek.com/2013/03/30-tu-ya-samsung-galaxy-s4-kuwa-na-core.html