Usichokijua kuhusu Samsung Galaxy A14 5G

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
View attachment 2719893

Kampuni ya Samsung iliachia simu ya Galaxy A14 iliachiwa January 12 2023 ni simu nzuri ya bei nafuu yenye muonekano mzuri kuanzia kioo ,kamera, software update support ila utendaji wake wa Kazi ni wa mashaka ngoja tuone.

Samsung Galaxy A14 5G specs:
Processor MediaTek Dimensity 700
Display 6.6 FHD + LCD + 90Hz
Ram 8Gb + Storages 64Gb / 128Gb sd extended (1Tb)
Battery 5000mah
Front Camera 13mp f/ 2.0
Rear Camera 50mp + 2mp + 2mp
Support 5G, WIFI 5, Nfc
199 up to 200

Galaxy14.jpg


Ndani ya Box
Ni simu yenye muonekano mzuri sana kwa ujumla ukiwa nayo unafurahia kwani imeundwa kwa mfumo wa Plastic sio glass. Gharama yake ni rafiki utaipata kuanzia shilingi 300k mpaka 450k.

Ubora wake unaanzia kwenye betri unaweza tumia mpaka siku mbili bila kuchaji Iko na Kasi kwenye kufungua program mbalimbali.

View attachment 2719897

Kioo chake ni kikubwa kiasi Kikiwa na mfumo wa LCD ambayo inakupa mwanga mzuri kwenye kuangalia kitu bila shida yoyote.

Kamera yake Iko poa unaweza vuta kitu mbali na kukipiga kwa ukaribu bila shida yoyote inatoa picha kali sana kwenye nyakati ya usiku pamoja na mchana

processor yake ni ya kawaida sana maana unaweza tumia muda mrefu ila sio nzuri kwa matumizi ya Game kwa matumizi ya kawaida ni nzuri maana performance yake Iko poa sana.

View attachment 2719896

Ina support android version 13 pia unaweza kupata update ya android version 14 na 15 zikitoka. speaker zake ni Mono yenye nguvu kiasi unaweza tumia tu.

Inaingia maji jihadhari ukiwa maeneo yenye mvua, inachukua masaa mawili na dakika 30 kujaa full kabisa, haijaja na chaji ndani ya Box Iko yenyewe tu.

Pia unaweza patq toleo jipya la Samsung Ui 6.0 ikitoka kwa Sasa Iko kwa watumiaji wa beta version kwa Samsung Galaxy s23 pekee.


View attachment 2719894View attachment 2719895
 
Mchawi media tek hapo yaani siku hizi nikiona simu hataiwe nzuri vipi kama ni mediatek naachana nayo! Silipendi tu hilo jina la " mediatek".
Sio MediaTek zote ni mbaya... Mbona kuna Snapdragon na Samsung Exynos Processor vimeo tu zinazidiwa na baadhi ya Processor generations za MTK au unaweza kuta uwezo sawa kabisa! Shida ni makampuni ya kuunda simu baadhi wanatumia MTK zile vimeo either kulingana na soko walilolenga ndo maana unakuta simu (hasa Samsung na Xiaomi kidogo wana michezo hii) Samsung aina hiyo hiyo inayouzwa India na baadhi ya nchi za Asia au Africa ina processor tofauti au processor yao ya Exynos au MTK ila model hiyo hiyo inayouzwa Ulaya na Marekani inakua na Qualcomm Snapdragon au Exynos ambayo ni somehow powerfull...
 
Back
Top Bottom