2025 tukichaguana kwa U-Simba na U-Yanga, nani ataibuka mshindi?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,103
22,543
Salaam, Shalom!

CDM na CCM hoyee!

Twende haraka kwenye mada.

HOJA ya swali hapo juu ni kutaka kujadili madhara na faida za kuingiza siasa michezoni.

Tumeona hivi sasa imeibuka TABIA ngeni ambayo tangu uhuru hatujawahi kuiona ikiendelea kuzoeleka.

Michezo tangu uhuru imekuwa ni chanzo Cha UMOJA na kuunganishwa makundi yote na KUIMARISHA UMOJA na mshikamano wetu kitaifa.

Tumekuwa tukiona viongozi wa Upinzani wakiweka mbali mavazi Yao ya kisiasa na kuvaa jerzey na kufurahia burudani ya mpira bila kujali itikadi zao za kisiasa.

Ilikuwa ni kawaida kumkuta Mbowe akiwa amekaa pamoja na Rizwani KIKWETE wakishangilia timu Yao ya Yanga bila kuvaa sare zao za vyama.

Huu Utaratibu mgeni wa kuingia na mabango na picha za viongozi wa chama viwanja vya michezo unalenga nini?

Yaani mechi ya simba na yanga, unakutana na watu wamevaa sare za chama na PICHA kubwa na MABANGO ya kiongozi wa chama zenye jumbe zisohusiana na michezo, jumbe ni za kisiasa na hawakemewi wanapoingia.

Lengo la kuingiza siasa michezoni Lina faida na HASARA zipi?

Ikiwa Mdude, Dr. Slaa na Mwabukusi nao wakianza kuingia viwanja vya michezo na mabango ya kisiasa Viwanjani wataruhusiwa?

Na Hali hii ikizoekeka, katika chaguzi zijazo tukapiga kura Kwa kufuata timu zetu za Simba na Yanga, nani ataibuka mshindi?

Na Hali ikiwa hivyo, UMOJA wetu wa kitaifa utaendelea kuwa kama ulivyo?

Nani aje atukemee, Ili tujirekebishe?

Karibuni 🙏
 
FB_IMG_1698682350017.jpg
 
Ili swala hua linanishangaza Sanaa ni upumbavu siasa kwetu ni uchawa na ushabiki tu watu siasa imekua kama michezo unachagua tu upande wa kushabikia bila vigezo na wameingiza kwenye michezo na nadhan Azam wanalipwa pia kwa hili.
 
Inatakiwa TFF walisimamie hili kwa haraka sana likemewe. Mmh...! TFF ipi lakini? Daah
 
Inatakiwa TFF walisimamie hili kwa haraka sana likemewe. Mmh...! TFF ipi lakini? Daah
Wanasiasa wanajiaibisha na kuonekana washamba!!!

Unaingizaje mabango ya kisiasa michezoni, Ili iweje?
 
Kuingiza siasa michezoni, kutaongeza hamasa ya vijana kushiriki siasa na uchaguzi?

Ni zipi faida au HASARA?
 
Yanga ataibuka mshindi😂

CCM wote Yanga

Mbowe, Tundu Lisu, Halima Mdee Yanga

Abdul Nondo Yanga

Mdude Yanga😀

Wastaafu Mwinyi na JK Yanga 😀

Mo Yanga 😂😂😂😂😂🔥🔥🐼
Hujaelewa muktadha wa HOJA!!

Ikiwa uhasama wa kisiasa ukiingizwa michezoni, Mbowe na KIKWETE watakaa Kwa Amani kama zamani Simba na Yanga zikiwa zinacheza?

UMOJA wa kitaifa utakuwepo?
 
Back
Top Bottom