2015: Tunahitaji Rais mwenye UWEZO!

Jambo linalonishangaza ni kwamba more than 70 ya population ya Tanzania walizaliwa baada ya uhuru, wamezaliwa na kukulia kwenye mazingira ambayo (naamini) udini, ukabila, umri havikuwa issue hasa kwenye siasa. Sasa haya maneno ya u-mkoa, ukabila, udini wametoa wapi? Na kwanini? Tanzania tunakwenda mbele au tunarudi nyuma?

Nitegemea hao wanaobudu siasa za ujana wawe wanahubiri kuhusu kutengeneza rocket, kujenga our own silicon Valley, lakini day in day out we are being subjected to this medieval politics! Inaudhi.
 
Hold on a second; kama ningetaka kumzungumzia Zitto ningemzungumzia Zitto. Mada yangu iko wazi kabisa; hatuhitaji Rais mzee au kijana, hatuhitaji Mkristu au Muislamu, hatuhitaji Mdigo au Mchagga, hatuhitaji tu yeyote isipokuwa mwenye uwezo. Hili si gumu sana kulielewa. Sitaki Rais atajwe kuwa ni "Rais Kijana" as if ujana wake unahusiana kwa namna yoyote na Urais wake! Kama kuna mtu ana hoja ya kutaka kuwa Rais wa Tanzania aitoe SIMPLY and ABSOLUTELY on merit ya uwezo wake tu. Si kwa sababu "ni kijana" au "ni mzee" au ni "Mkristu" au ni "Muislamu"...

Labda inabidi niwe natafuna kabisa kabla wengine hawajaanza kusoma nisichoandika.

Umri wa mtu ni kigezo ambacho hakiepukiki kwa kazi ambayo ni demanding kama ya urais wa nchi. Lazima tuweke tena kwenye katiba umri wa kuanzia mtu kuwa rais wa nchi na umri wa kikomo. Huwezi kunishawishi kuwa mandela anaweza akawa rais kwa sasa pamoja na uwezo wake wote tulioushuhudia. Kama sisi ni watu makini basi kigezo cha umri hakiepukiki.
 
kigezo cha umri ni kwa ajili ya eligibility tu siyo kwa ajili ya perfomance. think about it. As a matter of fact binafsi ningependa umri wa urais uongezwe kutoka 40 to 45 na mawaziri kuanzia 40! Ubunge kuanzia 35!
 
Mimi naamini hata umri wa kikomo ni muhimu, kuna mahali nilisikia mwalimu wakati anang'atuka watu walishaanza kumuita hambiliki (hashauriki) na alikuwa mkali kwa kuitwa jina hili.
 
Umri wa mtu ni kigezo ambacho hakiepukiki kwa kazi ambayo ni demanding kama ya urais wa nchi. Lazima tuweke tena kwenye katiba umri wa kuanzia mtu kuwa rais wa nchi na umri wa kikomo. Huwezi kunishawishi kuwa mandela anaweza akawa rais kwa sasa pamoja na uwezo wake wote tulioushuhudia. Kama sisi ni watu makini basi kigezo cha umri hakiepukiki.

Nakubaliana na wewe kabisa mkuu, 100%. Siyo kila umri unafaa kuwa Rais, zaidi ya miaka 70 ni tatizo tu, hata wanasayansi wanalijua hili. Umri mdogo zaidi pia ni tatizo. Kwa wanaojua Company Act, 2OO2, ukomo wa mtu kuwa Director wa Kampuni ambayo ni Limited Liability ni miaka 70! Unadhani walioweka ukomo huu hawana akili? Hatuwezi kumchagua babu awe Rais au hata kijana mdogo awe Rais wa nchi hii.
MMM asipotoshe watu kuwa umri si tija sana, ni tija sana tena sana tu!
 
Tukianza ubaguzi dhidi kundi fulani mathalalni wazee, au vijana, watafuata wanawake, kisha tutabagua walemavu, halafu kanda, ukabila, dini, rangi, mwisho tutasema Rais lazima awe na kimo cha sm 200. Ni upuuzi mtupu kuangalia mtu anayefaa kuwa Rais kwa vigezo vya kibaguzi ktk nchi ambayo Nyerere alitujengea usawa kwa wote kwa miaka mingi. Wako wazee waliovuruga nchi zao na wako vijana waliovuruga nchi zao kama huyo wa Syria naye aliingia kama kijana. Kumbukeni mafanikio yaMzee wa miaka 74, king cobra wa Zambia.

yote kwa yote zitto hafai na hatokuwa Rais wa nchi hii.

kama huo ni ubaguzi, na uwe.
 
Mnapenda ligi kweli. Kwamba kuna vijana wenye uwezo wa kuwa Rais Tanzania hilo sipingi....However,We dont give a damn about if the president is young or old.
All Tanzania need is a good man who is not afraid to step on toes and of course with a clear focus.

Tusitumie nguvu nyingi,let Tanzanians decide!

yes let Tanzanians decide! Na watanzania ndio sisi na sio wengine na humu JF ni watanzania ambao tunatoa views zetu so msijidanganye eti watanzania waamue kwani hao watanzania mnaowataja ndio sisi ambao tumesema kwamba 2015 hatutaki Rais mnafiki na ndumilakuwili eti kisa ni kijana. Full stop
 
Umri ni kigezo,
ndiyo maana umri chini ya 40,
marufuku kugombea.

Sioni kwa nini mnajifanya hamuoni kwamba umri ni kigezo??
 
Umri ni kigezo,
ndiyo maana umri chini ya 40,
marufuku kugombea.

Sioni kwa nini mnajifanya hamuoni kwamba umri ni kigezo??

Labda unge tufahamisha na umri wa ukomo wa kugombea ni miaka mingapi? Pia rais kijana anatakiwa kuwa na umri wa miaka mingapi na rais mzee ana umri gani? Nauliza hivyo maana maneno kijana na mzee yanatumika sana katika mustakabali wa kumpata rais.
 
Wazo la leo: Tanzania haiitaji Rais kijana... kwani tunapeleka Ikulu mbeba vyuma au mtunisha misuli au atakuwa na kazi ya kupiga push ups ofisini? Na hatuwezi kumkataa mtu kwa sababu ni mzee kwani anaenda kubebeshwa viroba vya mchele au kukimbia marathon? Tena hata hatuhitaji Rais msomi wa kivile! Mwaka 2015 Watanzania wanahitaji Rais ambaye atavunjilia mbali sera zilizoshindwa za CCM, kuifumua mifumo mibovu ya kiutawala iliyodumu kwa miaka karibu hamsini sasa na kutupa uongozi wa kutufanya tujiamini kuwa tunaweza na akatuongoza katika kujenga taifa la kisasa lenye kujali utu wa watu na siyo vitu vya watu.

Tunahitaji rais na pamoja naye viongozi wenye UWEZO wa kufikiri kwa usahihi, kuamua kwa usahihi na kutenda kwa usahihi wakitambua dhamana ya uongozi ambao taifa linawapa. RAIS ajaye wa Tanzania ni lazima awe na UWEZO; UMRI wake usihusishwe kabisa na uwezo huo.

Kiongozi ajaye basi ni lazima we ni MTU WA WATU; ambaye amejitofuatisha katika mambo makubwa yafuatayo: Wazo hili litaendelea...

FACEBOOK YANGU

MKJJ..hii hoja yako nayo ipo so general...,kiufupi ukiangalia ni kama unapigia debe mtu amabye anaweza kujitangaza kuwa anazo sifa za kuwa rais ...nasema hhv kwa sababu to be honest kwa nchi yetu ilivyo sasa ni dhahiri kuwa mafisadi ndio wanauwezo wa kulipia media na kulipa waandishi pia ili wawaandike vzr hili lipo wazi...mie ninachoamini ni kuwa viongozi wazuri ambao wanaweza kusaidia nchi yetu wapo wengi ila wamebanwa na siasa chafu zinazoendeshwa sasa hivi..,wanaogopa hata kujityokeza maana watamalizwa kwa njia yeyote.

Mie ningeshauri waandishi kama wewe kama kweli na nyie mna nia ya dhati kusaidia taifa letu na hamana maslahi binafsi ni vyema kuueleza umma ukweli kuwa shv viongozi karibia wote wanaotafuta urais kwa udi na uvumba ni wasaniiii..kwa maaana ya kuwa ni wajanjawanjanja wa mjini wanacheza na mind za watu ili waweze kutimiza malengo yao tu ya kuitafuna nchi yetu. Hakuna kiongozi kama J>K>Nyerere au Karume kati ya hao wote ambao wanakimbilia huo urais shv.

na kwataarifa yako wazanzibari wameshaliona hilo kuwa utawala wa muungano umeshakuwa chaka la wasanii ndio maana unaona viongozi wenye heshima zao wa zanzibar wanataka zanzibar iliyo huru shv kwa kasi ili waendelezee zanzibar yao na watuache bara na upuuzio wetu tunashadadia tukiongozwa na vyombo vyetu vya habari. Asante
 
Rais wa 2015 asiwe ka kikwete kwenye mambo yote..kuanzia weupe kucheka kufikiri nk..mengine ninaogopa kuandika ntaonekana mdini humu afu nipewe ban..
 
Nakubaliana na wewe kabisa mkuu, 100%. Siyo kila umri unafaa kuwa Rais, zaidi ya miaka 70 ni tatizo tu, hata wanasayansi wanalijua hili. Umri mdogo zaidi pia ni tatizo. Kwa wanaojua Company Act, 2OO2, ukomo wa mtu kuwa Director wa Kampuni ambayo ni Limited Liability ni miaka 70! Unadhani walioweka ukomo huu hawana akili? Hatuwezi kumchagua babu awe Rais au hata kijana mdogo awe Rais wa nchi hii.
MMM asipotoshe watu kuwa umri si tija sana, ni tija sana tena sana tu!

"Ujana" si tija. Umri ni kwa ajili ya eligibility tu. Hauhuusiani na uwezo wa uongozi. Hata mtu wa miaka 70 anaweza kuwa na u wezo mkubwa wa kufanya kazi ambazo zinahitaji akili zaidi kuliko mtu wa miaka 40. Lakini kama ana miaka 70 na bado ana nguvu za mwili kwanini asipewe nafasi hiyo? Wengi wetu baba zetu ndio wamefika miaka 70 hivi unafikiri kweli tunaweza kusema hawafai kufanya kazi yoyote inayohitaji hekima na uwezo wao wa kiakili?

Ninachojengea hoja hapa ni kuweka suala la umri kwenye context sahihi. Haiwezekani mtu aseme "tunahitaji viongozi vijana" au "sasa ni zamu ya vijana" halafu watu wakashangilia? Kwanini tunataka viongozi wanyanyua vyuma ili vijana washinde kirahisi?
 
Wazo la leo: Tanzania haiitaji Rais kijana... kwani tunapeleka Ikulu mbeba vyuma au mtunisha misuli au atakuwa na kazi ya kupiga push ups ofisini? Na hatuwezi kumkataa mtu kwa sababu ni mzee kwani anaenda kubebeshwa viroba vya mchele au kukimbia marathon? Tena hata hatuhitaji Rais msomi wa kivile! Mwaka 2015 Watanzania wanahitaji Rais ambaye atavunjilia mbali sera zilizoshindwa za CCM, kuifumua mifumo mibovu ya kiutawala iliyodumu kwa miaka karibu hamsini sasa na kutupa uongozi wa kutufanya tujiamini kuwa tunaweza na akatuongoza katika kujenga taifa la kisasa lenye kujali utu wa watu na siyo vitu vya watu.

Tunahitaji rais na pamoja naye viongozi wenye UWEZO wa kufikiri kwa usahihi, kuamua kwa usahihi na kutenda kwa usahihi wakitambua dhamana ya uongozi ambao taifa linawapa. RAIS ajaye wa Tanzania ni lazima awe na UWEZO; UMRI wake usihusishwe kabisa na uwezo huo.

Kiongozi ajaye basi ni lazima we ni MTU WA WATU; ambaye amejitofuatisha katika mambo makubwa yafuatayo: Wazo hili litaendelea...

FACEBOOK YANGU

Mzee Mwanakijiji unatakiwa kujua kwamba Tanzania haiko tambarare, kuna thread moja imeanzishwa na Mchambuzi imeeleza vizuri sana kuhusu urais 2015. Believe me 2015 tunaweza kuwa ovyo kuliko tulivyo sasa. Alichosema Profesa Baregu kuwa mtaji wa kisiasa wa CCM ni unyonge wa watu, hilo bado linaendelea ni kweli watanzania wengi ni wanyonge JF ni forum ya wasomi na radicals, lakini wapiga kura waliowengi wakihongwa kofia, vitenge au pilau(kwenye sehemu za pwani) watampigia kura yeyote yule.

MTU WA WATU kama JK? Hell no, we need something better. We need a capable politician who can turn things around, who can make Tanzania better, who can make Tanzania a country again, sio atakayechekelea wadini, mafisadi, wababaishaji, wauaji, sasa hivi misingi ya umoja, amani, usalama, uchumi na uhuru yote iko mahututi, tunataka mtu atakayefanya kazi ya kuimarisha misingi hiyo. Wote tunaosikia wanasema nina uzalendo naweza kuwa rais........wote wazugaji tu.
 
Akili Kubwa lazima zitawale akili ndogo (Mchungaji Msigwa). Piga kushoto au kulia, huu ndiyo ukweli.

Uzuri wa kuchagua mtu mwenye umri mkubwa ni mmoja, ".... mnamfahamu ndani na nje".

Tanzania imefikia hapa tulipo kwa kuyaficha mabaya ya viongozi kabla hawajachaguliwa. Mangula angeletwa hapa pia Membe na Kitine wakafunguka, basi hata Zomba angelibadilisha mawazo.
 
Nimeipenda sana hii hoja, kikubwa ni uwezo!. Endeleeni kuweka vigezo tena with elimination strategies, at the end of the day, tutarudi kule kule kwa the "good ones" who are capable, piga ua galagaza, mwisho wa siku tutagota mule mule!.

Huwezi kuzuia upepo!. Mgombea wetu ni magma ya moto, saa hizi imeanza kutokota kidogo tuu, watu wanaweweseka!, jee itakapo chemka ni nini kitafuatia... ni eruption tuu!, nothing more, nothing less!, 2015 rais wa ukweli tunae na ni ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!.

Tumechoka na wagombea urais wa mazoea na ahadi, sasa tunataka mgombea sio tuu mwenye uwezo, bali pia mwenye mission na vision anataka kulitoa taifa letu hapa lilipo, atatupeleka wapi na strategies za kuimplement hiyo mission ili kuifikia hiyo vision in reality na sio ahadi hewa!. Mtu wa namna hii tunaye its only the matter of time!.
 
Jambo linalonishangaza ni kwamba more than 70 ya population ya Tanzania walizaliwa baada ya uhuru, wamezaliwa na kukulia kwenye mazingira ambayo (naamini) udini, ukabila, umri havikuwa issue hasa kwenye siasa. Sasa haya maneno ya u-mkoa, ukabila, udini wametoa wapi? Na kwanini? Tanzania tunakwenda mbele au tunarudi nyuma?Nitegemea hao wanaobudu siasa za ujana wawe wanahubiri kuhusu kutengeneza rocket, kujenga our own silicon Valley, lakini day in day out we are being subjected to this medieval politics! Inaudhi.
Ahsante kwa hoja zako nzuri. Tatizo lililopo limeanzishwa na wanasiasa na viongozi wa dini.

Hawa wametumia udhaifu wa kuelewa wa asilimia 70 kupenyeza udini na ukabila. Lakini isingekuwa tatizo kama kungekuwa na busara kwa wale waliopewa dhamana.Udini na ukabila vilikuwepo hata zamani,uzuri ni kwamba kila vilipojitokeza vilikemewa sana na kwa nguvu zote. Siku hizi mamlaka zote zinaogopa kukemea! sababu ni kuwa viongozi waliopo hawakuingia madarakani kwa hoja bali ulaghai huo huo wa ukabila na udini.

Tuna makundi matatu ya wananchi, la kwanza ni la wale wanaoelewa na kujielewa.
Kundi la pili ni wale waisoelewa lakini wanategeme busara zao.
Kundi kubwa ni hili lililopo la asilimia 70 ambalo wengi wamepikwa wakaiva nusu'half baked'. Hawa wanajua kusoma kwahiyo wanaweza kukupa majina ya viongozi na dini zao tena kwa takwimu hafifu za asilimia 60 ni viongozi wa kabila au dini fulani hata kama viongozi hao ni 5. Simple statistic hakuna analysis wala kuliangalia jambo kwa wider prism.

Hili ndilo kundi hatari sana kwasababu halijui lakini linadhani linajua. Wasi wasi wangu ni kuwa kila kukicha hili kundi la nusu nusu linazidi kuongezeka na linatumika sana na wanasiasa na viongozi wa dini

Kuhusu hoja ya ujana vs uzee,hapa tunapotoka sana. Urais ni taasisi siyo mtu mmoja kama ilivyo kwa viongozi wa kada nyingine.

Manager mzuri ni yule mwenye timu nzuri, na timu nzuri inapatikana kwa busara za manager mzuri.
Mfano, Tonny Blair alikuwa PM akiwa na iaka 45, pengine yeye ndiye alikuwa na elimu ndogo umri mkubwa au mdogo katika timu yake. Kilichomsaidia ni weledi, hekima na busara za ku-organize resorce alizonazo.

Ronald Reagan alikuwa Rais akiwa na umri mkubwa sana. Ni mmoja wa marais wa Marekani wanaotajwa kuwa bora. Kilichomsaidia ni hekima, busara na maono yake katika kutengeneza timu ya uongozi na ku-organize resource alizokuwa nazo

Kiongozi tunayemuhitaji si yule maarufu, msemaji au mwenye umri na jinsia fulani.
Tunahitaji mtu atakaye organize resource zilizopo kututoa point A kwenda B.
Tunahitaji mtu mwenye weledi, busara, hekima na maono(vision).

Mtu mwenye uthubutu wa kufikiri na kutenda, kusikiliza na kusikilizwa, atakayetuunganisha na kusimamia thamani zetu kama taifa. Kiongozi tunayemuhitaji ni yule anayeweza kusimama na kutetea anachokiamini ni sahihi kwa jamii hata kama kufanya hivyo ataudhi watu, lakini pia ni mtu anayeijua jamii anayoiongoza na dunia kwa ujumla.

Ujana au Uzee hautusaidii katika nyakati tulizonazo.
 
Back
Top Bottom