2015: Tunahitaji Rais mwenye UWEZO!

Mzee MMM,

Naungana na wewe issue hapa si kuwa watZ wanahitaji kijana, Vijana wana nafasi yao na sisi tunahitaji rais ambaye atakuwa ni msafi kwa maana ya hana makundi wala harufu ya Rushwa na actualy waTZ au Chama chake kinaona anafaa.

Hatutaki Rais anataka urais kwa udi na uvumba, Rais anayetakka kuwa rais, bali Rais ambaye watu wanaona anafaa.

Mfano, Dk Slaa hata Ubunge hakuwahi kupigania, na wala hata kwenye kampeni hakuwa anatoa machozi wala kupiga magoti ili achaguliwe, bali alikuwa anawaambia atafanya nini endapo watamchagua kuwa Mbunge wao. Na kwa wanaokumbuka hata 2000 wakati wa uchaguzi aliwaambia wanchi wa jimbo lake kama hawatawachagua madiwani wa chama chake basi itakuwa haina maana yeye kuchaguliwa kuwa mbunge kwa sababu mambo mengi yanayohusu wananchi yako katika nganzi ya Halimashauri.

Tunakumbuka jinsi 2010 alivyishawishiwa kugombea lakini hakutaka kugombania urais ndani ya chama chake, shinikizo lilipozidi kutoka humu JF, Wasomi mbali mbali na wananchi wa Kawaida ndiyo Kamati kuu ya chadema ilipoona anafaa kugombea na kmwomba kugombea.

WaTZ ni mashahidi jinsi alivyopewa Kura nyingi na katiaka kuhujumu matokeo yale hata huyu Zito anayetaka Urais kila kikicha alikuwepo nadhani mnakumbuka gazeti la mwanahalisi liliripoti mawasiliano ya moja kwa moja kati ya wakuu wa TISS na Zito katika kuchakachua na kuhakikisha anagawa CDM katika msimamo wa kutotambua Urais wa JK

Ni bora mtu mwingine aonekane anafaa kutikoni Zito kwani amepwaya sehemu nyingi sana.
 
diector 1
thinking zako kwa zitto zinaonekana una chuki za kupindikua na zitto. Pendekeza hao waezee wako tuwaone kama hatutashuhudia ukimpendekeza el. Acha uchonganishi.

zitto hatakuwa raisi wa nchi hii hawezi na hafai .full stop
 
hivi ni rais gani mnayemzungumzia ? rais wa JF ama TFF . samahani mimi ni mgeni maeneo haya.
 
Mwl. Nyerere alishasema tumuogope sana mtu anataka kukimbilia IKULU, alisistiza Ikulu hakuna biashara, akasema
tena tumuogope mtu huyo kama UKOMA, ZITTO ni UKOMA namuogopa....
.. inategemea na mazingira husiki, mathalani mtu kupata utajiri wa ghafla (kununuliwa) na kunza kugombea uraisi. kuna watu wamestruggle kuleta maendeleo majimboni mwao, na hata michango yao bungeni ina "MASHISKO" mie sina pingamizi nao juu ya urais. isitoshe mtu kuweka nia mapema inatupa wasaa wa kukupembua ipasavyo mbali nakua unatimiza haki yako kidemakrasia. .... kwahiyo mitizamo yenu juu ya ZITO ni mizuri kwasababu ina jazia HEKIMA katika kumtathmini mtu ( kwa mazuri na mabaya yake). Mie binafsi, naona ZITO ni MCHAPAKAZI mzuri sana, ningekuwa Central Commitee ya Chadema, (CC) ninge mptisha nakumpigia debe
 
.. inategemea na mazingira husiki, mathalani mtu kupata utajiri wa ghafla (kununuliwa) na kunza kugombea uraisi. kuna watu wamestruggle kuleta maendeleo majimboni mwao, na hata michango yao bungeni ina "MASHISKO" mie sina pingamizi nao juu ya urais. isitoshe mtu kuweka nia mapema inatupa wasaa wa kukupembua ipasavyo mbali nakua unatimiza haki yako kidemakrasia. .... kwahiyo mitizamo yenu juu ya ZITO ni mizuri kwasababu ina jazia HEKIMA katika kumtathmini mtu ( kwa mazuri na mabaya yake). Mie binafsi, naona ZITO ni MCHAPAKAZI mzuri sana, ningekuwa Central Commitee ya Chadema, (CC) ninge mptisha nakumpigia debe
Zitto kanunuliwa vipi unampitisha kuwa mgombea wa URAHISSI katika nch ya Kigoma?
 
Hold on a second; kama ningetaka kumzungumzia Zitto ningemzungumzia Zitto. Mada yangu iko wazi kabisa; hatuhitaji Rais mzee au kijana, hatuhitaji Mkristu au Muislamu, hatuhitaji Mdigo au Mchagga, hatuhitaji tu yeyote isipokuwa mwenye uwezo. Hili si gumu sana kulielewa. Sitaki Rais atajwe kuwa ni "Rais Kijana" as if ujana wake unahusiana kwa namna yoyote na Urais wake! Kama kuna mtu ana hoja ya kutaka kuwa Rais wa Tanzania aitoe SIMPLY and ABSOLUTELY on merit ya uwezo wake tu. Si kwa sababu "ni kijana" au "ni mzee" au ni "Mkristu" au ni "Muislamu"...

Labda inabidi niwe natafuna kabisa kabla wengine hawajaanza kusoma nisichoandika.
 
Weledi hauturuhusu tena kujaribu (trial) kwenye sanduku la kura. Hatuna fursa na wala hatuhitaji kujaribisha hasa kwa vigezo vyepesi vyenye mvuto wa pipi. Kwa nafasi zote kuanzia udiwani, ubunge mpaka urais ni lazima Watanzania tuwe makini sana na werevu 2015.

Tunataka mtu ambaye hatatumia miaka 4-5 "kujifunza" ili eti tuje tumpe miaka mingine mitano ya kurekebisha na kufanyia kazi aliyojifunza. Urais sio shule wala theatre, urais ni kazi na matokeo.

Of coz JK kaashusha sana hadhi ya taasisi ya Urais ndio maana kila mtu anaona anaweza kuwa rais.

MM naunga mkono hoja 100%
 
Mnapenda ligi kweli. Kwamba kuna vijana wenye uwezo wa kuwa Rais Tanzania hilo sipingi....However,We dont give a damn about if the president is young or old.
All Tanzania need is a good man who is not afraid to step on toes and of course with a clear focus.

Tusitumie nguvu nyingi,let Tanzanians decide!
 
Tukianza ubaguzi dhidi kundi fulani mathalalni wazee, au vijana, watafuata wanawake, kisha tutabagua walemavu, halafu kanda, ukabila, dini, rangi, mwisho tutasema Rais lazima awe na kimo cha sm 200. Ni upuuzi mtupu kuangalia mtu anayefaa kuwa Rais kwa vigezo vya kibaguzi ktk nchi ambayo Nyerere alitujengea usawa kwa wote kwa miaka mingi. Wako wazee waliovuruga nchi zao na wako vijana waliovuruga nchi zao kama huyo wa Syria naye aliingia kama kijana. Kumbukeni mafanikio yaMzee wa miaka 74, king cobra wa Zambia.

...Mie mgeni mitaa hii, kwani King Cobra ana mafanikio gani zaidi ya kuwa Rais wa Zambia?au kwa sababu sasa amekuwa Rais na yeye, ndugu na rafiki zake sasa wanakula maisha kwa gharama za Wazambia?..http://www.zambianwatchdog.com/2012/06/20/more-question-satas-delegation-of-relatives/


...King Cobra so far ni walewale...http://www.newsdzezimbabwe.co.uk/2012/06/sata-attacked-as-he-leaves-for-london.html
 
Ikulu kuna biashara gani? Ikulu cyo mahala pa kukimbilia...............nyerere(1995)
 
Haya mambo sijui sasa yanaelekea wapi sasa!
Kuna kundi tuliambiwa tukiliwezesha linaweza...ina maana haliwezi lenyewe hadi liwezeshwe? matokeo yake kweli tukaamua "kuliwezesha" kila kona na kila nyanja...

Wakati wa kuchagua spika pia kigezo hicho kikatumika...matokeo yake ndo haya tunayoyaona leo.
 
Mtu smart hawezi kuhusisha uongozi na umri,wala uongozi na dini,wala uongozi na anakotokea,wala uongozi na anachomiliki,bali namna anavyoweza kukabiliana na changamoto,urais na pahala panapohitaji uelewa wa juu,hekima ya kipekee,busara ya kipekee,a real comitted one,uadilifu usiotiwa shaka,upendo kwa waliokutuma i.e voters,uzalendo wa kweli,mtu mwenye uwezo wa kubuni namna na njia za kutukomboa kiuchumi n.k na akasimamia,uwezo huu definitely hautokani na anapoishi sasa,hautokani na dini yake,haupatikani ktk kabila lake bali kwa mtu mwenye sifa ya kuwa rais,na obviously mtu huyu huwa hajioni kuwa yeye ndiye bali wanakuwa naye ktk harakati mbalimbali,hajitangazi bali mwenendo na sifa zake humtangaza,hivyo tutambue kuwa muda pia ni kigezo kitachotupa mtu mwenye sifa na weledi watz tuutakao.
 
Tukianza ubaguzi dhidi kundi fulani mathalalni wazee, au vijana, watafuata wanawake, kisha tutabagua walemavu, halafu kanda, ukabila, dini, rangi, mwisho tutasema Rais lazima awe na kimo cha sm 200. Ni upuuzi mtupu kuangalia mtu anayefaa kuwa Rais kwa vigezo vya kibaguzi ktk nchi ambayo Nyerere alitujengea usawa kwa wote kwa miaka mingi. Wako wazee waliovuruga nchi zao na wako vijana waliovuruga nchi zao kama huyo wa Syria naye aliingia kama kijana. Kumbukeni mafanikio yaMzee wa miaka 74, king cobra wa Zambia.

yeah, king cobra namkubali. 2005 jk alivyoingia kwa madaraka si walisema ni kijana! nini kafanya hadi sasa?
 
Well said Mwanakijiji….lakini iwe ni rais kijana au mzee; mwenye busara au asiye na busara bado hawezi kukukabiliana na changamoto zxa msingi za taifa hili ikiwa bado atakuwa anaongozwa na Katiba inayosimamia utawala bora wa kimagharibi! Nchi yetu ina matatizo makubwa; yasiyoweza kunyanyulika kwa folk lift wala kwa winch! Kabla ya huyo rais ambae wewe na wengine wote tungependa tuwe nae kwanza anapaswa kupewa nyenzo itakayobeba matakataka makubwa kuliko yote yaliyopo nchini kwetu na kwenda kuyatupilia mbali…ikibidi hata bahari ya Pacific ili yasirejee tena nchini mwetu! Matakata haya, ni maadili mabovu ya Watanzania; ingawaje tunataka kuaminishana kwamba ni maadili mabovu ya Viongozi wa CCM! Nyenzo pekee anayopaswa kupewa rais huyo chaguo la wote ni Katiba ya Kidikteta…..Sio Kiongozi wa Kidikteta; bali ni Katiba ya Kidikteta itayaoondowa makandokando yote yaliyogubika mioyo hasidi ya Watanzania walio wengi!

Vyovyote iwavyo, hata kama Rais ajae atoke mbinguni, bado hawezi kuondoa makandokando hayo chini ya katiba inayohubiri Utawala Bora; Utawala Bora wa Kimagharibi! Mfumo ambao, moja ya nguzo zake kuu ni Utawala wa Sheria!! Mfumo ambao unatuambia kwamba mtu atabaki kuwa mtuhumiwa hadi pale itakapothibitika; beyond reasonable doubt kwamba kosa analotuhumiwa nalo kwamba ni kweli amefanya!! Kwamba; leo hii ingawaje William Mhando anatuhumiwa kufanya ufisadi TANESCO lakini bado huwezi kuwa na grounds za kumpeleka korokoroni na kumtupa jela….huwezi kufanya hivyo kwa kuwa huna ushahidi; huo ndio Utawala wa Sheria; moja ya nguzo muhimu kabisa za Utawala Bora!!! Wengine nao wanadai Maswi (Katibu Mkuu wa Nishati) ndie fisadi na ananufaika na Puma Energy….huyo nae, huwezi kumpeleka mahakamani kwavile hakuna ushahidi…na hata ukimpeleka bado atashinda kesi; huo ndio Utawala wa Sheria, ambao ndio msingi mkuu wa Utawala Bora!

Hivyo basi, tatizo sio ni rais wa aina gani, bali ni katiba ya aina gani !! Tunahitaji kwanza katiba ya kidikteta itakayo-shape maadili ya Watanzania!Tunahitaji Katiba ya Kidikteta ambayo itamafanya rais yeyote ajae 2015 kufanya si kwa kutaka bali kwa kulazimishwa na Katiba Ya Kidikteta!! Katiba ambayo, itatamka wazi, ile kutuhumiwa peke yake inatosha kabisa kumpeleka mahakamani mtuhumiwa na badala ya kutaka upande wa mashitaka ndio uthibitishe beyond reasonable doubt tuhuma dhidi ya mtuhumiwa; basi ni mtuhumiwa ndie athibitishe beyond reasonable doubt kwamba tuhuma dhidi yake si sahihi…tuhuma ninazozungumza hapa ni zile ambazo ndizo kansa kuu ya nvchi hii; TUHUMA ZA UFISADI!! Katiba ya Kidikteta ambayo pia itatamka wazi kwamba; kumzushia mtu tuhuma ambazo si za kweli; hiyo nayo ni serious crime ili kuzuia watu kuwazushia wenzao kwavile tu wanafahamu wazi kwamba Katiba Yetu Mujarabu Ya Kidikteta itamwajibisha yule anayemzushia!

Anyway, nazani hili linahitaji thread inayojitegemea lakini nihitimishe tu kwamba kwa katiba yoyote itakayoendeleza Mfumo wa Utawala Bora ambao moja ya nguzo zake kuu ni Utawala wa Sheria basi haitakuwa na msaada wenye tija kwa rais awaye yote labda tu aamue kuvunja misingi ya katiba inayohubiri utawala bora!


tukiwa na katiba safi hata mwehu anaweza kuwa Rais na tusi athirike sana...

tazama Philipines...kuna muigizaji maarufu alikuwa anaitwa Estrada akafanikiwa kuwa Rais..
sheria na katiba zikamtimua hadi jela.....

na aliemrithi nae alipoleta uhuni..
leo yupo kizimbani.....

ishu hapa ni katiba sahihi na sheria nzuri tu baasi
 
Mnapenda ligi kweli. Kwamba kuna vijana wenye uwezo wa kuwa Rais Tanzania hilo sipingi....However,We dont give a damn about if the president is young or old.
All Tanzania need is a good man who is not afraid to step on toes and of course with a clear focus.

Tusitumie nguvu nyingi,let Tanzanians decide!

Mbona maneno makali? "vijana wenye uwezo" na "wazee wenye uwezo" wote wapo Tanzania. Kama vile wapo Kina "mama wenye uwezo" na kina Baba wenye uwezo" au "Wasukuma wenye uwezo" au "Wandengereko wenye uwezo". Kwanini tusijikite tu kwa wenye "uwezo". Yeyote mwenye kuamini kuwa ana uwezo apewe nafasi yake na ajitokeze pasi ya shaka bila kutuchombezea vitu vingine irrelevant. Ujana, uzee, kabila au jinsia havina sababu kabisa ya kuingizwa katika mjadala wa Rais au viongozi wetu. Sivyo?
 
Back
Top Bottom