1st Anniversary: JF Assault

Sikuijua JF mpaka siku serikali ilipojaribu kuizima JF mwanzoni mwa mwaka jana - hicho kitendo ama jaribio la serikali kilizaa neema kubwa kwangu. Kwa mara ya kwanza nilifarijika kujua kuwa sikuwa peke yangu katika kusononeka kila nilipofikiria uongozi na hatma ya nchi yangu niliyoipenda. Kama lengo la serikali ilikuwa ni kuidhoofisha JF, basi ilishindwa na uongozi wake ulionyesha udhaifu mkubwa wa kukurupuka bila mpangilio -ila safari hii kukurupuka kwao kulileta faraja tele.

Leo naweza nikasema kwa kujiamini kuwa serikali imeipa, inaipa na itaendelea kuipa umaarufu JF kama itandeleza vitendo kama hivyo vya kijinga. Binafsi nawashukuru na kuwapongeza mzalendo/wazalendo waliokaa chini wakabuni hili jukwaa lisilo mfano wake - vizazi kwa vizazi vitawakumbuka kwa huo ujasiri wenu. Nachukua nafasi hii kuwaomba wanachama wote kila moja kwa wakati wake kuutambua mchango wa hawa wazalendo na tufikirie tuzo tunaloweza kuwapa.

Idumu JF mpaka Tanzania itakaporejesha hadhi yake si Afrika tu bali kote duniani. Tumedanganywa, tumenyanyaswa, tumedharauliwa, tumetukanwa na tumeibiwa vya kutosha na sasa JF twasema basi. Atakayedharau nguvu ya JF, atakayefikiria kuinyamazisha JF na atakayedhani moto uliowashwa na JF utazimika, anaota ndoto kama Idi Amin aliyeamini anaweza kuitwaa sehemu ya Tz na akabaki madarakani - alikuja kuikimbia nchi yake bila kuaga.

Hii inaonyesha jinsi watawala wetu wanavyohaha usiku na mchana kuminya uhuru wa kupata habari. Yaani wanatumia rungu kuua kainzi! Ila kitu kinachonifurahisha ni kuwa kupitia uvamizi wa dola dhidi ya JF ndipo wananchi wengi walijiuliza JF ni nini na waktaka kuijua na si ajabu JF imezidi kupata umaarufu kuliko mwanzoni.

Ni vema serikali ifahamu hili-the more forces it usues against JF the more stronger and popular JF become. Ni vema Watawala watulie ili tuendelee kuwapa data za mambo yanavyoendela nchini, hapa watapata dte za kuwasaidia kupamabana na Ufisadi (if they are willing na kuwakosoa pia ili wajirekebishe). Wasilogwe kuwa katika nyakati hizi watanzania bado ni walewale wa1947, Watanzania wamebadilika sana na wamezidi kuelimika zaidi.

JF idumu daima, ikiwa CCM inatawala au haitwaw
 
Mod naomba ubadilishe kichwa cha habari na kuwa-1st Anniversary after JF Assault. Nadhani itkuwa sanifu zaidi kuliko sasa.
 
Back
Top Bottom