mzeewaSHY
JF-Expert Member
- Aug 31, 2021
- 8,864
- 8,512
Yaani umemalizia kwamba “ kwenda Shule ni suala moja na kuelimika ni suala jingine kabisa. “Tukio la Bukoba limenikumbusha vifo vya kuogelea vilivyochukua maisha ya Stewart na Antony miaka ile ya 1980
Stewart alifia Bwawa la Kinondoni karibu na Mahakama na Jirani na ghorofa la mama Siri Yako( Mrangi wa Ufipa unapajua)
Zimamoto walipokuja walishindwa kuuokoa mwili wa Stewart ndipo akatokea mgema mmoja wa pombe ya mnazi akaomba kusaidia. Akaweka kindoo na kisu chake pembeni akapiga mbizi, baada ya kama Dakika 10 akanyoosha mikono kuwaita askari wa Zimamoto wamfate na walipomfikia alipiga mbizi na kuibuka na mwili wa dogo Stewart
Kadhalika Anthony mtoto wa Dereva wa kwanza wa Nyerere mzee Said TANU alifia Selender bridge na mwili wake uliokolewa na Wavuvi baada ya askari wa Zimamoto kusita kuzamia wakidai eneo lile lina Chunusi
Ndio sababu kipekee nimempongeza sana Rais Samia kwa kumpa ajira Kijana Majaliwa wa Bukoba
Vyeti ni makaratasi tu
RIP Stewart
RIP Antony Kamtawa
RIP marehemu wa Precision Air
cc: Mrangi Ova