Inga Stone; Jiwe, Mwamba wenye fumbo utata maajabu na maswali yasiyo na majibu kwa Binadamu wa kizazi hiki!

Dumas the terrible

JF-Expert Member
Jan 20, 2021
4,154
8,444
Kwema wanajamvi jukwaa la wenye kuumiza vichwa?

Basi powa twende sasa,
Huko Paiba Brazil kuna Mwamba au Jiwe kubwa lenye 250 feet in Length,

Hilo limwamba ligumu lina michoro ya kushangaza sana,
Michoro hiyo inayokadiriwa kua na umri wa miaka 6,0000 kwa makadirio ya kawaida inaacha utata mkuu mno kwa namna ilivyo na ukilinganisha na historia ya Humanoid katika Dunia hii yaani kama babu zetu walikuwepo basi walikua primitive au Nyani kabisa huku misitu ya kongo (joking)

Ila katika hali ya kushangaza michoro ya Inga stone imechorwa kwa ustadi na technology ambayo hata leo na ujanja wetu hatujaufikia bado!

Inga stone limechorwa alama mbali mbali kama wanyama wa ajabu ambao katika kizazi hiki hawaexist,vile vile kuna mimea na viumbe wa ajabu ajabu,

Kubwa kuliko yote ni michoro yenye kuhitaji sayansi kubwa kuitambua yaani mifumo nyota katika Ulimwengu huu namaanisha
Constallations kama Milkiway na Orion
Hapa ndipo penye utata!

Nani miaka zaidi 6,0000 iliyopita alijua mambo hayo?
Je ni Humanoid sisi au kuna viumbe wengine nje yetu yaani Alliens walifanya ujuzi huo wa ajabu?

Mbali na hayo maumbo mbali mbali ya Geometry pia Zoomorphic figure na celestial bodies za kushangaza sana,

Jiwe hili ni Moja ya mamia ya site zenye utata mkubwa hapa Duniani kama Mapyramids,Matemple ya miamba,mapango na Underground tunnel zinazounganisha Dunia katika hali ya kushangaza
Just imagine temple kama Kailasa lililopo huko India ni tech gani iliyotumika kuichonga katika Mwamba mgumu namna ya kushangaza vile?
Nani alijenga Spaceships grounds huko Baalbek?
Yaani miaka 6,0000 huko nyuma watu walienda space?

Wamaya na Aztec wanaacha utata hasa wanapomtaja mungu wao Quetzalcoatl aliyekua na flying machine, au Wamisri na wahindi wakisema miungu yao ilikuja kutoka juu bado ni utata!

Dunia ya kale ilipata kupitia kipindi chenye maendeleo ya kushangaza kiasi kwamba bado ni fumbo na kiza kwa watu wa leo,

Hakuna chanzo maalumu cha kutoa miongozo kwa namna gani Science na teknolojia ya kale ilifika mbali mara elfu kuliko leo kiasi kwamba inaacha utata mkubwa,
Wengi wetu tunahusisha masuala Haya na viumbe ambao ni Extraterrestrial waliodaiwa kuwepo kwenye Dunia yetu miaka Mingi nyuma kabla yetu maana kiuhalisia historia ya Mwanadamu bado changa ila mambo yaliyofanyika yanaonesha ni makongwe kuliko hesabu za uwepo wetu hapa Duniani,
Je kuna baadhi ya secret Society zinajua ukweli huu na sinaficha siri kwa ajenda zao maana hata baadhi ya taasisi kama UNESCO zenye majukumu ya kutunza mambo kale hua na majibu mepesi kwa maswali magumu juu ya baadhi ya sites wanazotunza na ukweli wa historia ya kweli uliofichwa,
Inga stone inawaumbua kwa kutotambua ustaraabu unaohusishwa na viumbe wageni kuwahi wepo hapa Duniani kwa mamilioni ya miaka iliyopita!

Bado najifunza!
Mshana Jr Artificial intelligence Maghayo Da Vinci XV zitto junior LIKUD JamiiForums
 

Attachments

  • the-inga-stone--scaled.jpg
    the-inga-stone--scaled.jpg
    317.9 KB · Views: 6
  • inga002.jpg
    inga002.jpg
    35.2 KB · Views: 7
  • ae83f89931e9b1d7d08b068c1ae42ea6.jpg
    ae83f89931e9b1d7d08b068c1ae42ea6.jpg
    134.1 KB · Views: 8
  • inga.jpg
    inga.jpg
    56.9 KB · Views: 8
Inafikirisha Sana lakn najiuliza hv vtu ni kweli vina Umri huo au ni vtu vnavyofanywa na hzo hzo secret societies kwa usiri mkubwa kwa manufaa yao tu?
Kweli mkuu mara nyingi hizo site hua zinaonekana accidentally tu,
Unajua kabla ya Tech tuliyonayo watu waliona kawaida tu ila baada ya kukua kwa tech unaona watu ndio wanashtuka aah hii mbona ni kitu fulani?
Inafikirisha Sana lakn najiuliza hv vtu ni kweli vina Umri huo au ni vtu vnavyofanywa na hzo hzo secret societies kwa usiri mkubwa kwa manufaa yao tu?
 
Mbona sioni hata mchoro mmoja wa maana?
Hahaha yaani hapo Mzee baba hizo Symbols ni balaa very complicated,maana nyingine utazikuta kwenye Mapyramids na Matemple ya kale,
Wanasayansi wanazijua hizo kama umefuatilia elimu ya nyota na mambo anga utaelewa hapo!

Wamaya,Wamisri,Wababylon,
Wahindi,Dogon wa kale hiyo michoro ya Constallations wanaitambua vema na ipo makumbusho huko UNESCO nk!
 
Mbona ipo wazi na wanazuoni wemgi wa Kikristo wanakiri kulikuwa na maisha kabla yetu mkuu. Katika uumbaji kwenye "mwanzo 1:1-30" pale kuna vitu havikuumbwa kwani vilikuwepo ila kilichofanyika ni kuamrishwa kutokea tu. Nchi(Ardhi na miamba) haikuumbwa ila ilikuwepo kwenye uumbaji wa mwanzo (Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi) ambao aliuharibu na kuwatowesha viumbe vyao kwenye maji na ndio maana Roho wa Bwana akatua juu ya uso wa Maji ambao ulikuwa umetandwa na giza.

Kabla ya uumbaji wetu, dunia hii ilikaliwa na viumbe vingine ambavyo vilikuwapo ulimwenguni miaka na miaka. Wao wanajua kila kitu na walishuhudia uumbaji wa kila kitu ila wameshindwa kujua namna mwanadamu alivyoumbwa hususani ile pumzi ndio hawajui siri yake.

Kwahiyo, kuanzia Pyramids za Misri hadi Michoro ya Maya ni zama zile za uumbaji wa mwanzo ambao waliteketezwa kwa maji na sasa wanaishi majini.
 
Pia kingine cha maana angalia hiyo tech ya kuichonga miamba,
Hizo Symbols zimechorwa kwa ustadi sana leo hakuna vifaa vya kuichonga miamba kwa namna ya ajabu hivyo nalo ni Moja ya ajabu!
Kuna viumbe vilikiwepo kabla yetu. Mwanzo 1;1-2 inaonesha kulikuwa na kitu kilitokea before uumbaji wa sasa na ndio maana katika uumbaji wa "Mwanadamu Mungu alihitaji ushauri"
 
Mbona ipo wazi na wanazuoni wemgi wa Kikristo wanakiri kulikuwa na maisha kabla yetu mkuu. Katika uumbaji kwenye "mwanzo 1:1-30" pale kuna vitu havikuumbwa kwani vilikuwepo ila kilichofanyika ni kuamrishwa kutokea tu. Nchi(Ardhi na miamba) haikuumbwa ila ilikuwepo kwenye uumbaji wa mwanzo (Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi) ambao aliuharibu na kuwatowesha viumbe vyao kwenye maji na ndio maana Roho wa Bwana akatua juu ya uso wa Maji ambao ulikuwa umetandwa na giza.

Kabla ya uumbaji wetu, dunia hii ilikaliwa na viumbe vingine ambavyo vilikuwapo ulimwenguni miaka na miaka. Wao wanajua kila kitu na walishuhudia uumbaji wa kila kitu ila wameshindwa kujua namna mwanadamu alivyoumbwa hususani ile pumzi ndio hawajui siri yake.

Kwahiyo, kuanzia Pyramids za Misri hadi Michoro ya Maya ni zama zile za uumbaji wa mwanzo ambao waliteketezwa kwa maji na sasa wanaishi majini.
Kwahiyo ndo majini?
 
Kwahiyo ndo majini?
Kuna ushuhuda mmoja wa mama mmoja wa kinijeria alilisema kuhusu uwepo wa viumbe vilivyokaa duniani miaka na miaka na wao wanaamini walimilikishwa hii dunia. Ukisoma "Ezekieli 28" wanapoongelea kuhusu Mfalme wa Tiro aliyekuwa kerubi ambaye alitembea kwenye mlima Mtakatifu wa Mungu kwani yeye ndiye alikuwa "mtawala wa nchi" sasa alipopewa mwanadamu nchi aitawale ndipo iliyosababisha "amjaribu na kumuangusha mwanadamu".
 
Back
Top Bottom