Ziwa Ngosi;
Ziwa hili ni la pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya ziwa lingine la kreta lililopo Ethiopia linaakisi muonekano wa bara la Afrika katika upande wa kusini, magharibi, kaskazini na mashariki pamoja na visiwa vyake vya Unguja na Pemba.
Ziwa Ngosi linapatikana kwenye milima ya Uporoto, Mkoa wa Mbeya nyanda za juu kusini mwa Tanzania , ziwa hili linatajwa kutokana na mlipuko wa volkano hivyo ni tofauti na maziwa mengine kama ziwa victoria au ziwa nyasa.
Upekee au utofauti wa ziwa hili ni kwamba ziwa hili liko juu ya milima na katikati ya misitu na lina urefu wa km2.5, upana wake ni km 1.5 , kina chake ni mita 74 na lina ukubwa wa hecta 9332.