Zile dakika5 baada ya kuibiwa kitu cha thamani

Mwagito84

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2016
Posts
235
Reaction score
716
Umewahi ibiwa ukachoka kiasi cha kuishiwa nguvu, kukaa chini na kumwaga machozi kindezi, huelewi hata imeibiwaje licha ya tahadhari kibao ulizo jiwekea.

Binafsi nimewahi ibiwa simu kwa namna ya ajabu, simu ilikuwa na siku 5 tu mpyaaaa. Samsung J7 pro ya 660k. Nikilia kiukweli. Tafuta tafutana wewe, kibaya zaidi hela nyingine niliazima kwa msela nijazie.

Karibu namaliza deni lakini.
Siku nyingine nilipoteza vyeti vyote vya taaluma, nilikuwa nasafiri kamaa anayeshuka njiani nahisi alikiwa anafuatilia mwenendo wangu wa kupiga mbonji, akashuka nalo nafika ubungo begi silioni napo nilijikaza sikuweza. Nilijenya sana nililia tena na ilinichukua miaka 2 kuvipata Jamaa alivitelekeza morogoro wasamalia wema wakaviokota na kusambaza ujumbe kwenye magroup ya whassap ndo kuvipata. Mwenzangu umewahi pitia kisa cha namna hii?
 
Nilipoteza simu Samsung s4 nilikuwa nimetoka zangu kazini asubuhi nikapitiliza kwenda Temeke sasa wakati wa kurudi nikawa nimeishika mkononi baadae nikaiweka hapa kwenye miguu nikalala, nakuja kushtuka nimefika kituo changu cha kushukia nikakurupuka simu hata sikukumbuka nikaenda kwenye kibanda cha mpeza kudeposit hela nimtumie bi mkubwa lahaulaa simu haipo nikatoa vitu vyote kwenye pochi patupu aisee nilidataa
 

Aisee msalimie bi mkubwa
 
Pole
 
Pole dada mzuri,ungenipitia siku hiyo ninhekulinda njiani
 
Nilimkaribisha gheto classmate wangu wa primary school ambae alifukuzwa kwa dada yake akaomba hifadhi kwangu kwa siku tatu akaishia kukaa miezi 3.

Jamaa nilikuwa nampa chakula na malazi kila kitu hataki kazi. Nilipomsihi afanye mpango wa kazi au kutafuta chumba akona isiwe tabu akasafisha gheto kila kitu kuanzia boxer, notebook(sio computer ni kitabu) hadi malapa ya kuogea.

Nilikuwa nalala kwenye biashara zangu, ile narudi gheto kubadili nguo nakuta kweupe kaacha fridge, kitanda na godoro tu. Mziki na vitu vingine muhimu vya ndani na vya biashara kasomba vyote.

Nilipiga magoti na kumuombea msamaha kwa Mungu. Tangu siku hiyo maisha yake kama nilimlaani bora ningemuombea mabaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…