Zawadi kwa wanandoa

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Siri mojawapo ya kudumisha upendo kwenye ndoa ni kununuliana zawadi. Zawadi kwa yule mtu unaeishi nae ni rahisi kuifikiria. Angalia kile kitu kinapungua katika maisha yake ya kila siku.

Wanaume wengi husahau kununua socks. Hutapenda mumeo aadhirike kisa walikwenda msibani na alipovua viatu socks zake zilikuwa na madirisha.

Pamoja na vitu vingine unafahamu kuwa majukumu ya kodi ya nyumba na ada za watoto mume awako amejitwika. Si vibaya ukimnunulia dozen ya socks kwa mwaka.

Unaweza kuzigawa, valentines unampa pair nne, Birthday yake pair nne na Christmas unampa pair nne. Mengine utaongezea mwenyewe. Asprin nilimnunulia Bible yenye Leather Cover na huwa ninapata mstari kila asubuhi. Asante mume.

Wakina kaka ukijua mke wako anapenda vitenge au handabags wengine perfumes, ndiyo mbolea yenyewe kwenye mapenzi.
Huhitaji kununua vitz au VX5 ndiyo ajue unampenda.
 
Wanandoa wakishazoeana mara nyingi huwa wanachukuliana poa tu yaani kusingekuwa na tendo la ndoa tungewaita dada na kaka wanaolala pamoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…